Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Ni dhahiri kuwa mchakato wa kupata Katiba mpya umekwama.
Ili tuweze kupata Katiba, kama hoja italetwa tena siku zijazo, basi ni vema kuamua kwanza kuhusu mfumo wa Muungano.
Tukumbuke kuwa, kama ilivyo kwa Zanzibar, leo hii nasi tungekuwa na serikali ya Tanganyika basi tusingekubali kuivunja.
Hivyo suala la msingi ni kuamua kati ya serikali 3 au serikali 1.
Mkuu mchakato wa kupata Katiba mpya kwa maoni yangu umewekwa akiba kwa muda tu "PAUSE" na ukirejea utakuja na kasi ya ajabu mpaka tutashangaa, kama unakumbuka vizuri BMK lilishamaliza kazi yake ilibakia tu kuipigia kura, na hapa katikati kama unavyojua taifa letu limekua na mambo kibao likiwemo suala la uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu ili kuhakikisha kuwa wote wenye sifa za kupiga kura wanatumia haki yao kikatiba kuamua mustakabali wa taifa lao, isingekua busara kuharakisha upigaji wa kura kabla ya kundi kubwa la vijana ambao nao wametimiza umri wa kupiga kura wangeachwa eti kwa sababu tu ya kukosekana kuwepo kwenye daftari la wapiga kura!
Mungu ni mkuu, Zoezi hili linaendelea naamini kura itapigwa Tu maadam kazi imebaki kwetu kuipa ridhaa!