Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Angola ni moja ya nchi muhimu zaidi ambayo Marekani na China zinashindania ushawishi barani Afrika. Marekani imewekeza sana katika njia ya Lobito yenye umuhimu wa kimkakati nchini Angola, ikijenga reli ya kuunganisha bandari ya Lobito na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia. Reli hiyo itaipa Marekani njia ambayo inaamini inaweza kupata usafirishaji wa madini muhimu kutoka kwa nchi hizo. Hadi sasa, Marekani imewekeza dola milioni 553 za kimarekani katika mradi huu.
Mradi wa bandari ya Barra do Dande ni hatua nyingine muhimu katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Angola. Pia umeleta swali moja: wakati Marekani ikijaribu kwa nguvu kubwa kushindana na China katika ushawishi nchini Angola na nchi nyignine za Afrika kupitia mipango ya kimkakati kama reli ya Lobito, ni kwa nini haiwezi kutikisa nafasi ya China katika ushirikiano wa ujenzi wa miundombinu barani humo?
Labda jibu liko katika tofauti ya mifumo ya nchi hizo mbili ya ushirikiano na Afrika.
Mfumo wa Marekani ni mfumo unaolenga rasilimali na ushawishi. Kwa kuangalia mkakati wa hivi karibuni wa Marekani barani Afrika, mantiki yake ya kimsingi ni wazi: kwanza ni madini muhimu, na pili ni kuondoa ushawishi wa China barani Afrika. Kuanzia mradi wa utawala uliopita wa Marekani chini ya rais Joe Biden wa reli ya Lobito hadi mipango ya muungano wa madini iliyotolewa na rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump, lengo la sera ya Marekani kwa Afrika halijawahi kwenda mbali ya kupora rasilimali. Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (DFC) lililoanzishwa kwa lengo la kukabiliana na ushawishi wa kiuchumi wa China duniani, liliwekeza dola milioni 553 katika mradi wa Lobito. Kupitia njia kama vile makubaliano ya manunuzi na dhamana za kifedha, Marekani inatafuta kutumia mtaji kuhamisha madini ya Afrika ikiwemo shaba na kobalti hadi minyororo ya usambazaji nchini Marekani.
Kwa upande mwingine, mfumo wa China katika ushirikiano wa miundombinu na Afrika ni jumuishi, na kulenga kusaidia Afrika kujenga msingi imara wa ukuaji wa muda mrefu.
Mfano ni mradi wa Bandari ya Barra do Dande. Mradi huo si mradi wa miundombinu pekee, bali pia ni sehemu muhimu ya mkakati wa kiuchumi wa Angola unaolenga kuongeza mauzo ya nje kwa eneo lake la kaskazini. Mradi huo unajumuisha uboreshaji wa bandari, na ujenzi wa eneo la biashara huria na bustani ya viwanda. Utakapokamilika, utatosha kupokea meli za tani 80,000 na kutarajiwa kuongeza kiasi cha biashara cha kila mwaka kinachozidi dola bilioni 10.
Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Angola mwaka 1983, uhusiano huo umeendelezwa kuwa wa wenzi wa kimkakati katika pande zote. Makampuni ya China yamejenga bwawa kubwa zaidi, uwanja wa ndege wa kimataifa, na miradi ya kupunguza ukame, pamoja na Jiji Jipya la Kilamba nchini Angola. Mwezi Januari mwaka huu, mradi wa alumini wa kielektroniki wa Huatong Angola ulianza uzalishaji, ukijaza pengo katika tasnia ya alumini nchini humo.
Vyombo vya habari vya Marekani vilitoa kauli “kugawanya Afrika”, ambayo ni maneno yaliyotumiwa wakati wa ukoloni. Mantiki ya msingi iliyofichuliwa na maneno kama hayo inapingana kabisa na pendekezo la China la “kushauriana, kujenga kwa pamoja, na kunufaika kwa pamoja”. Ikiwa ushirikiano wa Marekani na Afrika utaendelea kuweka kipaumbele kwa maslahi yake ya upande mmoja, badala ya kuzingatia matakwa ya Afrika, basi hautakubaliwa wala kuaminiwa na nchi za Afrika.