Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John
Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.
Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.
Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande...