Sababu za wanafunzi wa kizazi hiki kufeli masomo ni hizi hapa

Wa kwanza kulaumiwa ni mzazi

Wazazi wengi hawafatilii maendeleo ya watoto wao, hawapekui madaftari ya watoto, hawawasiliani na walimu kujua mtoto anafika shule au la

Wazazi wameacha majukumu yao na kuikabidhi serikali ie kununua vitabu vya kiada na ziada, uniform, chakula etc

Mazingira ya nyumbani hayako kiurafiki kwa mtoto.

Serikali inakuja mwishoni kwenye swala la siasa, serikali inataka kura, hivyo itafanya lolote ili iweze endelea tawala.
 
Walimu wengi (SANA) hawana uwezo na ujuzi wa kufundisha somo alilopangiwa! Wewe umekazania wanafunzi - mimi naona Walimu wengi kama sio wote ni substandard!
 
Walimu wengi (SANA) hawana uwezo na ujuzi wa kufundisha somo alilopangiwa! Wewe umekazania wanafunzi - mimi naona Walimu wengi kama sio wote ni substandard!
Sasa walimu waliopata dision four unadhani watakuwa na uwezo gani wa kufundisha mkuu? Tatizo ni serikali kuruhusu watu waliofeli masomo kuwa walimu kwa kuwa hawajipeleki wenyewe kwenye ualimu bali huchaguliwa kulingana na vigezo dhaifu vilivyowekwa na serikali tukufu ya CCM.
 
Umetumia approach ipi kwenye study yako?, ni quantitative au qualitative?

Tuambie design iliyotumia kufanya utafiti wako.

Tueleze sample yako ilikuwaje

Methods of data collection and analysis

Tueleze pia ethical consideration kwenye study yako.
 
Nimekuelewa mtoa mada. Bila kufanya mabadiliko ya Serikali, tutaendelea kulia na kulia lakini hakuna kitakachofanyika.

Tuiweke madarakani Serikali itakayokuwa serious na Elimu.
 
Nimekuelewa mtoa mada. Bila kufanya mabadiliko ya Serikali, tutaendelea kulia na kulia lakini hakuna kitakachofanyika.

Tuiweke madarakani Serikali itakayokuwa serious na Elimu.
Hili nalo neno na ndilo la msingi hasaaa!
 
Serikali imekazania kurahisisha mitihani ili vilaza waingie sekondari. Matokeo yake ndio haya
 
Upo sahihi mkuu ✔️
 
Sitaki kulalamika moja kwa moja ninashauri tuache kukariri mitaala;
1.) Kwa sekondari mtoto mwenye wastani wa A-D ndiyo alipiwe ada na serikali (kuleta userious na kujituma) ukifeli lipa ada iingie halmashauri isaidie teknolojia mashuleni asiyelipa asifukuzwe adaiwe atapohitaji cheti kidato channe.
2.) Walimu wasimamiwe vyema wasiotimiza wajibu walimwe faini mf. Faini ya utoro,kutosahihisha kazi, kutomaliza mada etc. (Kuleta userious na kujituma)
3.) Wanafunzi wooote wale shuleni asielipia chakula aondoke shuleni saa saba kamili (asimalize vipindi vyote maana nikuwasababishia maradhi)
4.) Bweni zijengwe kwenye mashule mengi (kwani hata zamani sekondari nyingi zilikuwa na bweni)
5.) Masomo/vipindi boora hasa ya sayansi na hisabati yapatikane online kiurahisi mada mpaka mada (kurahisisha rejea za wanafunzi na walimu pia).
6.) Walimu wooote wa kiingereza mtaani waajiriwe shule za msingi na Kiingereza kifundishwe na walimu mahiri na kipewe vipindi viingi zaidi kwa shule za msingi huwezi fafanua mambo kwalugha usiyoijua na unayoiogopa).
8.) Shule zooote masomo yaanze saa mbili kamili mpaka saa tisa nanusu kila kipindi kiwe saa moja.
7.) Kidato cha nne wafanye mitihani mitatu mmoja wa wilaya mwezi wa saba, wa mkoa mwezi watisa mwisho wa taifa mwezi wa 11 kisha wastani ndiyo utumike kama matokeo ya mwisho!!
8.) Ijumaa iwe nisiku ya kujifunza Dini (woote), pia ifundishwe sanaa na michezo,ufundi,teknklojia,kilimo na stadi mbalimbali za kazi na maisha. Na vipindi viishe saa sita na nusu nchi nzima!!!
 
1.) Kwa sekondari mtoto mwenye wastani wa A-D ndiyo alipiwe ada na serikali (kuleta userious na kujituma) ukifeli lipa ada iingie halmashauri isaidie teknolojia mashuleni asiyelipa asifukuzwe adaiwe atapohitaji cheti kidato channe.
Kumbe wenye ufaulu wa D nao wanaenda sekondari? Hii nchi aliyeiroga kafa.
 
5.) Masomo/vipindi boora hasa ya sayansi na hisabati yapatikane online kiurahisi mada mpaka mada (kurahisisha rejea za wanafunzi na walimu pia).
Mkuu vitabu vyote vinapatikana haoa TIE Library: TieLibrary
 
6.) Walimu wooote wa kiingereza mtaani waajiriwe shule za msingi na Kiingereza kifundishwe na walimu mahiri na kipewe vipindi viingi zaidi kwa shule za msingi huwezi fafanua mambo kwalugha usiyoijua na unayoiogopa).
Hili neno mkuu. Zamani walimu wote wa Kingereza walikuwa wanapelekwa kupigwa msasa Uingereza; wakirudi nchini wanakuwa mahiri kweli kwenye somo hili. Nashangaa siku hz walimu wa Kingereza wanaokotwa majalalani halafu wakiingia darasani wanafundisha English kwa Kiswahili. Inauma sana.
 
Asante kwa nyongeza mujarabu mkuu. I hope wadau wa elimu wamekuelewa barabara.
 
Kumbe wenye ufaulu wa D nao wanaenda sekondari? Hii nchi aliyeiroga kafa.
Namaanisha mitihani ya sekondari wenye wastani wa F wasilipiwe ada ninaamini ni matumizi mabaya ya kodi zetu hawa washauriwe wakasomee ufundi nk.

Nb. Wenye ufaulu wa D huenda sekondari lakini private schools nadhani hawachaguliwi serikalini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…