Sababu za wanafunzi wa kizazi hiki kufeli masomo ni hizi hapa

Namba 7 naungana na wewe, bongo kila kitu siasa!

Nijazie tu kuna issue ya nyongeza za mishahara
 
Acha uongo we mzee
 
Kuna vitu vingi sana huvielewi mzee ,unapoona mambo yanabadilika sio kwamba serikali haioni ,ila kuna mikakati ya kimataifa iliyowekwa kila nchi lazima itimize kifikia mwaka uliokusudiwa kwahiyo kama unataka elimu bora peleka mtoto private tu
 
Ni sera ya Serikali kwa sasa kuwa Elimu ya Sekondari hadi Kidato cha nne ni universal. Kwamba kila mwanafumzi nchi anafika Kidato cha nne whether anajua kusoma au la.
Kwa hiyo hayo ya kusema ufaulu unashuka darasa la Saba au Kidato cha nne haina mashiko unless kama hujui Sera ya Elimu ya nchi yako. Ndiyo maana Serikali imeanza kupractice Sera ya Elimu bure hadi Kidato cha nne na kuwa na Shule ya Sekondari kila Kata nchi hii.
 
Kwa hiyo unataka kusema kwamba sera ya serikali ni kuswaga wanafunzi tu waende mbele bila kuangalia ubora wa elimu mkuu?
 
Kwa hiyo unataka kusema kwamba sera ya serikali ni kuswaga wanafunzi tu waende mbele bila kuangalia ubora wa elimu mkuu?
Ubora wa elimu ,watajuana mwanafunzi na mzazi wake huko majumbani kwao.
 
Ubora wa elimu ,watajuana mwanafunzi na mzazi wake huko majumbani kwao.
Hee 😳 😳 Sasa itakuwa serikali gani hiyo inayoswaga watu kama mbuzi kwa namna hii?🙄🙄🙄
 
Namba 7 naungana na wewe, bongo kila kitu siasa!

Nijazie tu kuna issue ya nyongeza za mishahara
Karibu sana tujadiliane kuhusu mustakabali wa elimu katika nchi yetu pendwa ya Tanzania.
 
Namba 7 naungana na wewe, bongo kila kitu siasa!

Nijazie tu kuna issue ya nyongeza za mishahara
Nimekupata vizuri kiongozi wangu. Hili nalo serikali inapaswa ilichukue ikalitizame.
 
Inasikitisha sana wanafunzi wa sekondari kutojua kusoma na kuandika,. CCM imetufikisha mahali pabaya sana.
 
Hii ndio aina ya wanafunzi wanaoandika matusi kwenye mitihani ya NECTA na bado wanafaulu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika. Nchi ngumu sana hii.
 
Namba 7 ndiyo mzizinwa fitna.
 
Elimu ya hii nchi ni majanga tokea zamani..
Umadikini tuliotiwa na CCM, ilikuwa ufaulu unapigiwa mstari kwenye idadi ya wanafunzi waliopasi kutokana na idadi ndogo ya shule za sekondari na kusababisha wengi kuonekana wamefeli wakati ukweli kulikuwa na uchache wa shule za sekondari, na hii pia ilienda mpaka kwenda vyuoni,
 
Lakini pamoja na shule za kata kuongezeka, mitihani ya kubet imesababisha wasiojua kusoma kupenya hadi sekondari.
 
Lakini pamoja na shule za kata kuongezeka, mitihani ya kubet imesababisha wasiojua kusoma kupenya hadi sekondari.
Sasa itakuwaje unasema shule zimeongezeka, wakati utafiti wako unasema kuna msongamano wa wanafunzi zaidi ya 200 kwa darasa moja ?
 
Sasa itakuwaje unasema shule zimeongezeka, wakati utafiti wako unasema kuna msongamano wa wanafunzi zaidi ya 200 kwa darasa moja ?
Ni hivi, shule kweli zimeongezeka ukilinganisha na ilivyokuwa zamani miaka ya 1980 na 1990. Kwa lugha nyingine shule zimeongezeka arithmetically lakini idadi ya wanafunzi imeongezeka geometrically. So, ,bado hazijatosha. Kwa hiyo, mrundikano bado upo palepale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…