Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, kusingehitajika shule yoyote kujua hilo. Hata ya chekechea. Kila mtu angejua Mungu huyo yupo, angejua hilo tangu anazaliwa, angejua kwa hakika bila shaka yoyote.
Kila kiumbe angejua hilo, bila shaka, bila mjadala.
Na tusingeweza kuulizana kuhusu uwepo wa Mungu.
Ukiona swali lolote kutoka kwa kiumbe chochote kuhusu uwepo wa Mungu huyo, maana yake ni kwamba Mungu huyo hayupo.
Kwa sababu, angekuwapo, kwa tabia zake hizo ( mjuzi wa yote, muweza yote, mwenye upendo wote), Mungu huyo si mkatili wa kuwanyima viumbe wake ujuzi kamili utakaoondoa shaka yoyote kuhusu uwapo wake.
Ukiona swali lolote kuhusu uwapo wa Mungu huyu, maana yake ni kwamba Mungu huyo hayupo.
Huelewi wapi?