Sababu zinazofanya nisiamini uwepo wa Mungu ni hizi

1. Mungu anapenda kusifiwa kama Mhaya.
Kwahiyo kama anapenda kusifiwa basi hayupo? Na pia ni wajibu wetu kama wanadamu kumsifu Mungu.
2. Mungu hana huruma (hukumu kwa wasiokuwa na hatia, vita sehemu nyingi za dunia, watu kufa kwa njaa na umaskini).
Kama ni kufa kila mtu atakufa haijalishi kwa njaa ama kwa magonjwa. Na pia wanadamu wanaingia vitani kwa tamaa zao wenyewe Mungu hausiki hapo.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, kusingehitajika shule yoyote kujua hilo. Hata ya chekechea. Kila mtu angejua Mungu huyo yupo, angejua hilo tangu anazaliwa, angejua kwa hakika bila shaka yoyote.

Kila kiumbe angejua hilo, bila shaka, bila mjadala.

Na tusingeweza kuulizana kuhusu uwepo wa Mungu.

Ukiona swali lolote kutoka kwa kiumbe chochote kuhusu uwepo wa Mungu huyo, maana yake ni kwamba Mungu huyo hayupo.

Kwa sababu, angekuwapo, kwa tabia zake hizo ( mjuzi wa yote, muweza yote, mwenye upendo wote), Mungu huyo si mkatili wa kuwanyima viumbe wake ujuzi kamili utakaoondoa shaka yoyote kuhusu uwapo wake.

Ukiona swali lolote kuhusu uwapo wa Mungu huyu, maana yake ni kwamba Mungu huyo hayupo.

Huelewi wapi?
 
Rudia tena kusoma hiyo paragraph yangu ya pili...
Utakuwa umepata majibu au ungeomba ufafanuzi kuanzia hapo
 
Rudia tena kusoma hiyo paragraph yangu ya pili...
Utakuwa umepata majibu au ungeomba ufafanuzi kuanzia hapo
Hakuna popte ulipojibu. Hakuna ulipothibitisha Mungu yupo. Hakuna ulipoeleza kimantiki kama Mungu yupo kwa nini watu wote wasijue uwepo wake bila kuhitaji kufundishwa wala mjadala.

Umeweka hadithi za imani tu.

Nachelea kwamba si tu huna majibu, bali hata maswali huyajui na hata ukielezwa sina hakika kama una uwezo wa kuyaelewa.
 
1. Mungu anapenda kusifiwa kama Mhaya.

2. Mungu hana huruma (hukumu kwa wasiokuwa na hatia, vita sehemu nyingi za dunia, watu kufa kwa njaa na umaskini).

Kuna sababu nyingi ila leo tuishie hapo.
Umetoa sababu za kutoamini uwepo wa Mungu, wanao amini nao wana sababu zao za kuamini. Nyote mnaunganishwa na imani. Huna na wao hawana uthibitisho. Imani ni kukubali au kuamini uwepo wa dhana au kitu ambayo huwezi kuthibitisha kisayansi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…