Sababu zipi zilimfanya Mwl.Nyerere kuiingiza nchi katika ujamaa na chama kimoja?

Sababu zipi zilimfanya Mwl.Nyerere kuiingiza nchi katika ujamaa na chama kimoja?

Mtu mjinga huwezi mpa uhuru wa kujiamulia kabla hajastaarabika.

Angekosea tuu hapo ,Ardhi ya Nchi hii ingekuwa ya wachache sana
Tanzania ina ardhi kubwa sana hata matajiri wangechukua isingeisha na mpaka leo naandika hapa kila siku serikali yako inaomba watu hasa vijana kuwekeza kwenye ardhi

Na kama swala lingekuwa ardhi si angebadilisha sheria ya ardhi peke yake kama mchangiaji mmoja alivosema. Yani ni sawa na kusema boxer imechanika unavua na susruali na shati vyote unabadili
 
Tanzania ina ardhi kubwa sana hata matajiri wangechukua isingeisha na mpaka leo naandika hapa kila siku serikali yako inaomba watu hasa vijana kuwekeza kwenye ardhi

Na kama swala lingekuwa ardhi si angebadilisha sheria ya ardhi peke yake kama mchangiaji mmoja alivosema. Yani ni sawa na kusema boxer imechanika unavua na susruali na shati vyote unabadili
Hujielewi wewe na ushamba unakusumbua.Unajua ni Ardhi ya ilimradi au? Arable land unajua ni kiasi gani? Hifadhi kiasi gani?
 
Nyerere hakutaka ushauri na zile safari zake za awali kwenda china na nchi za communist ndio zilimpa nguvu kujiona yupo sahihi.

Miongoni mwa mambo mengi Nyerere alificha moja wapo ni kuunganisha zenji na Tanganyika , yeye alisema ni ishu ya kiusalama ila hoja hii ni dhaifu sana . jamaa kwa kweli alificha mengi mpaka akaona nchi inaenda kushoto akang'atuka .
 
Hata washauri wake wa kisera za kiuchumi na kujenga taifa wa mwanzoni baada ya uhuru hawakuwa kutoka mataifa yenye mlengo wa kikomunisti bali ni huko Uk, France lakini baada ya hiyo 1965 Nyerere alibadilika katika namna ya kushangaza
 
yanyerere yanakuhusu nini? wakati hata ulikuwa haujazaliwa
 
Ila kiukweli aina hii ya siasa zimetuathiri sana siku ikitokea tukapata mabadiliko itakuwa kazi kubwa sana kuibadili mifumo mingi iliyo athirika maana tatizo ni kubwa kila sehemu.

Na ndio maana watu wa mataifa mengi ya kikomunisti ukiwaambia warejelee mfumo huo hawakuelewi kabisa.

Kuna kitu hakipo sawa.
 
Sio Tanganyika tu baada ya kupata uhuru (late 1950s - 1970s) nchi nyingi za Afrika ziliadopt African socialism ideology but in different models

Hizi ni sababu kadhaa ziliwafanya waadopt socialism iliyopelekea mfumo wa chama kimoja:

●Waliamini wakiwa chini ya mfumo wa chama kimoja watakuwa na umoja na mshikamano kwa sababu taifa zima lingekuwa chini ya single ideology. Msemo kama Zidumu fikira za Mwalimu ulitumika sana


●Kuepusha upinzani kutoka vyama vingine vya kisiasa. Hapa waliamini kukiwa na upinzani maendeleo ya taifa yatakuwa hatarini na kucheleweshwa kwa sababu ya mitazamo tofauti


●Kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe. Waliamini kuwa uwepo wa vyama vingi ingepelekea kila chama kupambana kiingie madarakani mwisho wa siku vita vya wenyewe kwa wenyewe


●Kuzuia ushawishi wa nchi za kibepari kwenye siasa za ndani. Walisema kwa kuwa multi party asili yake ni kutoka mataifa ya kibepari hivyo wanaweza kuweka vibaraka wao


●Uungwaji mkono kutoka nchi za ki-socialist kama USSR na China.

●Waliamini kuwa mfumo wa kibepari ni wa kinyonyaji


Ila mwishoni yakawashinda
 
Back
Top Bottom