Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.
Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Ni mada inayojadilika, ingawaje imewekwa kama chambo tu.
TANU wakati ule wa uhuru ilipata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa wananchi kuliko chama kingine chochote, hata vile vyama vilivyokuwa vikiungwa mkono na wakoloni.
Baada ya uhuru, uungwaji mkono wa TANU ulizidi kuimarika zaidi, hasa pale Mwalimu Nyerere alipo achia u-waziri mkuu na kwenda kukijenga chama.
Kwa hiyo TANU wakati ule haikuwa imeji-'impose' kwa wananchi. Chama kilipendwa na wananchi. Hili ni muhimu kuanza nalo kuondoa upotoshaji unaofanywa kwa maksudi kwa sababu zisizokuwa na maana.
Kuhusu kufutwa kwa vyama vingine vya upinzani; hili swali tunaweza kumuuliza karibu kilakiongozi wa Afrika wa wakati huo, siyo kazi aliyoibuni Mwalimu Nyerere. Ninayo maelezo ya hili, lakini nitaliachaa lilivyo.
"Uchumi wa soko huria", ulikuwa ni uchumi wa nani; nina maana ya nani aliyekuwa akifaidika zaidi na uchumi huo?
Huu uchumi huria unaozungumziwa, hasa maana yake ni nini? Pamba ikilimwa na mkulima Tanzania akauza kwa wakala katika eneo lake na kuendelea katika mnyororo wote hadi huko kwenye soko la wakubwa, "uhuria" wake upo wapi kwa huyo mkulima? Tunaposoma nadharia hizi katika vitabu, na tukaimbishwa nyimbo zake na hao hao wanaoendeleza ukandamizaji wetu; kwa nini tukose akili hta za kudadisi?
Tulikuwa tukitegemea sana mazao ya aina ile ile, kama pamba, mkonge, kahawa, 'pyrethrum, , na nini tena?Huko duniani kwenye "soko huria" ambako sisi hatukuwa na sauti yoyote ile, tungefanya nini ili tuendelee kupata manufaa ya kazi zetu hapa? Mkonge, mJapan kagundua nylon, zao bei ikabuma. Hivyo hivyo na pamba. Kahawa Brazil kateka soko,n.k., n.k,; leo hii tunakuja tunarudia nyimbo zile zile za ujamaa kuvunja "soko huria"!
Sasa leo tunapokuja hapa na kuhoji "Ni hoja zipi Mwalimu Nyerere alizitumia kuleta mabadiliko haya...", ni kana kwamba hali yetu ilikuwa inakwenda vizuri sana, hadi hapo Mwalimu alipoleta hoja zake!
Ni nchi zipi Afrika, (actually siyo Afrika pekee), ambazo zilibadili mifumo ya kiuchumi, hata kama siyo kama huo "Ujamaa" wa Nyerere tunaouongelea leo. Ni nchi zipi hazikuunda Mashirika ya Umma?
Sasa hata huko kwa wakubwa, wote walishikilia huo "uchumi huria" kwa sura ile ile iliyotumika katika kila nchi. Kulikuwa na "mwongozo (Blue Print) ya kwamba uchumi huria ni lazima ufanyike katika njia moja hii?
Ndiyo: hata katika yaliyofanyika hapa kwetu katika huo ujamaa hayakuwa 'perfect', na hapakuwa na shinikizo kwamba hakuna kinachoweza kubadilishwa kufuatana na hali iliyopo ili kupata ufanisi mkubwa kwa manufaa ya waTanzania (wote); na hakuna popote palipokatazwa kwa mtu kufanya bidii za ziada kwa manufa zaidi kwake.
Huo mfano wa China sasa watu wanauvungavunga tu kukidhi matakwa yao. China hadi leo ni nchi ya kikomunist. Kuwa na "soko huria" haina maana ya kuondoa lengo la watu kunufaika na uchumi wa nchi yao.