Ujamaa wa Nyerere ni socialism derived from African communalism.kaongela ujamaa, ujamaa ni commumism …
Hakufika tu north Korea,north Korea kwa comrade Kim IL sung alitambulishwa na maoJuche Ideology in North Korea
Uchu wa madaraka na kujiona anaakili kuliko watu wote.Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.
Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Communism is the highest stage of socialismUjamaa wa Nyerere ni socialism derived from African communalism.
Mwenyewe alifafanua vizuri tofauti ya Communism na African Socialism.
Tena alisema wazi ujamaa (socialism) ulikuwepo kabla ya kuja wakoloni hapa Africa, na ulikuwa tofauti na Communism in some aspects.
Lakini hujajibu hoja hata moja iliyowasilishwa kwenye mada. Wewe unajipigia tu kivyako, pamoja na kwamba mleta mada kakusoma na 'kupenda' ulicho andika.Kwa kweli yanahitaji maelezo ya kina.
Tukisema kutawaliwa kuna mataifa kadha wa kadha yalitawaliwa na wala hayakuona kabisa umuhimu wa kufagilia siasa za kikomunisti.
Mbaya ni kwamba licha ukomunisti kuanguka na kuvurugika duniani na yeye kung'atuka kwa nchi kumshinda bado aliendelea kuamini kuwa mawazo yake yalikuwa sahihi.
Can you imagine mfadhili wake mkubwa mchina alianza mabadiliko toka miaka ya 70 ya kujiengua zaidi huko katika uchumi akaja yule mzee Deng akazidi kufanya mabadiliko zaidi na zaidi ya kuweka mambo sawa na hawa ni wakomunisti pure kabisa waliofuata mtiririko wote wa kuusimika ukomunisti katika nchi lakini walibadilika ili kuondoa taifa katika shida kubwa lakini yeye Nyerere bado aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa yupo sawa.
Hata alipo mteua mwinyi alimuona wa ajabu kwa kutotilia maanani misimamo yake.
1. Ukweli kwamba katika mfumo wowote ule wa utawala kuna watu lazima watanufaika tu na huo mfumo hauzuii ukweli kwamba uongozi una wajibu wa kuweka level playing field, kusiwe na kunufaika zaidi kwa watu fulani. Hii kanuni hata mabepari wanaodogosha habari za usawa wa watu wanaielewa, ndiyo maana hata nchi za kibepari kama Marekani serikali bado ina regulate biashara na kuweka fairness.Mkuu katika mfumo wowote ule wa utawala lazima kuna watu watanafuaika tu na huo mfumo,
Sina uhakika kama haya masuala ya ardhi yalikuwa sababu alizozitoa Nyerere katika kuwapeleka watu kwenye ujamaa, lakini pia sheria ya ardhi ya Tanzania haijuzuia matatizo na madhila huko Ngorongoro na Loliondo kwa Wamasai na sehemu nyingine nyingi tu za utalii.
Lakini pia Tanzania inaweza kuwa ni mojawapo ya mataifa yenye kesi na migogoro mingi sana ya ardhi.
You are absolutely right. Mwalimu alisoma ujamaa bahati mbaya sana yeye na kundi lake wote na makomredi wengine bado wako hai na tunawapa heshima kubwa ila wote hawakuuelewa ujamaa kabisa hadi leo!!Alikuwa hajuwi alifanyalo.
Kongole mkuu. Tukitaka kukosoa Nyerere kuingiza nchi kwenye mfumo wa kijamaa lazima turudi kwenye mazingira ya wakati ule na sio kukosoa kwa kuangalia hali ya sasa. Ujamaa ulikua na faida na hasara kwa nchi yetu.Sio Tanganyika tu baada ya kupata uhuru (late 1950s - 1970s) nchi nyingi za Afrika ziliadopt African socialism ideology but in different models
Hizi ni sababu kadhaa ziliwafanya waadopt socialism iliyopelekea mfumo wa chama kimoja:
●Waliamini wakiwa chini ya mfumo wa chama kimoja watakuwa na umoja na mshikamano kwa sababu taifa zima lingekuwa chini ya single ideology. Msemo kama Zidumu fikira za Mwalimu ulitumika sana
●Kuepusha upinzani kutoka vyama vingine vya kisiasa. Hapa waliamini kukiwa na upinzani maendeleo ya taifa yatakuwa hatarini na kucheleweshwa kwa sababu ya mitazamo tofauti
●Kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe. Waliamini kuwa uwepo wa vyama vingi ingepelekea kila chama kupambana kiingie madarakani mwisho wa siku vita vya wenyewe kwa wenyewe
●Kuzuia ushawishi wa nchi za kibepari kwenye siasa za ndani. Walisema kwa kuwa multi party asili yake ni kutoka mataifa ya kibepari hivyo wanaweza kuweka vibaraka wao
●Uungwaji mkono kutoka nchi za ki-socialist kama USSR na China.
●Waliamini kuwa mfumo wa kibepari ni wa kinyonyaji
Ila mwishoni yakawashinda
Ni mada inayojadilika, ingawaje imewekwa kama chambo tu.Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.
Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Mkuu umeuliza mengi sana kuhusu soko huria lakini huu ni mfumo rahisi sana kuuelewa na kufanya kazi tofauti na ujamaa. Uelewa wa uchumi wa soko huria umefafanuliwa vizuri sana na Adam Smith kupitia dhana ya "invisible hand"Ni mada inayojadilika, ingawaje imewekwa kama chambo tu.
TANU wakati ule wa uhuru ilipata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa wananchi kuliko chama kingine chochote, hata vile vyama vilivyokuwa vikiungwa mkono na wakoloni.
Baada ya uhuru, uungwaji mkono wa TANU ulizidi kuimarika zaidi, hasa pale Mwalimu Nyerere alipo achia u-waziri mkuu na kwenda kukijenga chama.
Kwa hiyo TANU wakati ule haikuwa imeji-'impose' kwa wananchi. Chama kilipendwa na wananchi. Hili ni muhimu kuanza nalo kuondoa upotoshaji unaofanywa kwa maksudi kwa sababu zisizokuwa na maana.
Kuhusu kufutwa kwa vyama vingine vya upinzani; hili swali tunaweza kumuuliza karibu kilakiongozi wa Afrika wa wakati huo, siyo kazi aliyoibuni Mwalimu Nyerere. Ninayo maelezo ya hili, lakini nitaliachaa lilivyo.
"Uchumi wa soko huria", ulikuwa ni uchumi wa nani; nina maana ya nani aliyekuwa akifaidika zaidi na uchumi huo?
Huu uchumi huria unaozungumziwa, hasa maana yake ni nini? Pamba ikilimwa na mkulima Tanzania akauza kwa wakala katika eneo lake na kuendelea katika mnyororo wote hadi huko kwenye soko la wakubwa, "uhuria" wake upo wapi kwa huyo mkulima? Tunaposoma nadharia hizi katika vitabu, na tukaimbishwa nyimbo zake na hao hao wanaoendeleza ukandamizaji wetu; kwa nini tukose akili hta za kudadisi?
Tulikuwa tukitegemea sana mazao ya aina ile ile, kama pamba, mkonge, kahawa, 'pyrethrum, , na nini tena?Huko duniani kwenye "soko huria" ambako sisi hatukuwa na sauti yoyote ile, tungefanya nini ili tuendelee kupata manufaa ya kazi zetu hapa? Mkonge, mJapan kagundua nylon, zao bei ikabuma. Hivyo hivyo na pamba. Kahawa Brazil kateka soko,n.k., n.k,; leo hii tunakuja tunarudia nyimbo zile zile za ujamaa kuvunja "soko huria"!
Sasa leo tunapokuja hapa na kuhoji "Ni hoja zipi Mwalimu Nyerere alizitumia kuleta mabadiliko haya...", ni kana kwamba hali yetu ilikuwa inakwenda vizuri sana, hadi hapo Mwalimu alipoleta hoja zake!
Ni nchi zipi Afrika, (actually siyo Afrika pekee), ambazo zilibadili mifumo ya kiuchumi, hata kama siyo kama huo "Ujamaa" wa Nyerere tunaouongelea leo. Ni nchi zipi hazikuunda Mashirika ya Umma?
Sasa hata huko kwa wakubwa, wote walishikilia huo "uchumi huria" kwa sura ile ile iliyotumika katika kila nchi. Kulikuwa na "mwongozo (Blue Print) ya kwamba uchumi huria ni lazima ufanyike katika njia moja hii?
Ndiyo: hata katika yaliyofanyika hapa kwetu katika huo ujamaa hayakuwa 'perfect', na hapakuwa na shinikizo kwamba hakuna kinachoweza kubadilishwa kufuatana na hali iliyopo ili kupata ufanisi mkubwa kwa manufaa ya waTanzania (wote); na hakuna popote palipokatazwa kwa mtu kufanya bidii za ziada kwa manufa zaidi kwake.
Huo mfano wa China sasa watu wanauvungavunga tu kukidhi matakwa yao. China hadi leo ni nchi ya kikomunist. Kuwa na "soko huria" haina maana ya kuondoa lengo la watu kunufaika na uchumi wa nchi yao.
Hiki ulicho andika hakina tofauti na hiki "Democratic People's Republic Of Korea".China hadi leo ni nchi ya kikomunist
Na hapa ndipo tatizo kubwa linapoanzia katika ujamaa. Hii huwa inasababisha ubunifu kuwa mdogo, bidii ndogo na matumizi mabaya ya rasilimali za raia/nchi.2. Kanuni moja kubwa kabisa ya Ujamaa ni kuweka control ya means of productions kwa wananchi.
Ujamaa sio communism ni Socialism...kumbe hata unachokiongea haukijui !??kaongela ujamaa, ujamaa ni commumism …
Kitabu kilicholeta utajiri wa Ulaya na Marekani kinachoelezea capitalism kinaitwa The Wealth of Nations by Adam Smith (1776). Ni bahati mbaya sana viongozi wetu hawasomi kitabu hiki, au labda wanasoma na hawaelewi.Mkuu umeuliza mengi sana kuhusu soko huria lakini huu ni mfumo rahisi sana kuuelewa na kufanya kazi tofauti na ujamaa. Uelewa wa uchumi wa soko huria umefafanuliwa vizuri sana na Adam Smith kupitia dhana ya "invisible hand"
Hilo si tatizo la ujamaa.Na hapa ndipo tatizo kubwa linapoanzia katika ujamaa. Hii huwa inasababisha ubunifu kuwa mdogo, bidii ndogo na matumizi mabaya ya rasilimali za raia/nchi.
HeeeeeHEEEE!Mkuu umeuliza mengi sana kuhusu soko huria lakini huu ni mfumo rahisi sana kuuelewa na kufanya kazi tofauti na ujamaa. Uelewa wa uchumi wa soko huria umefafanuliwa vizuri sana na Adam Smith kupitia dhana ya "invisible hand"
Majibu yapo ukisoma THE RISE OF SOCIALISMWakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa nchi ya vyama vingi na uchumi wa soko huria kabla Nyerere hajabadilisha mfumo ni kutupeleka kwenye chama kimoja na ujamaa mwaka 1965 na 1967.
Ni hoja zipi Mwl Nyerere alizitumia alipofanya hayo mabadiliko makubwa hivyo ambayo yalitegemewa kuwa na hatimaye yamekuwa na matokeo mengi mchanganyiko kwa taifa hili?
Huu mfano uliutoa tokea jana au juzi, lakini nikakueleza ni mfano'superficial' kabisa unaoonyesha mtu asiyekuwa na upeo wa maswala kama haya.Hiki ulicho andika hakina tofauti na hiki "Democratic People's Republic Of Korea".