Sababu zipi zilimfanya Mwl.Nyerere kuiingiza nchi katika ujamaa na chama kimoja?

Very Correct.

Ila kuna wimbi la watu wanaotaka kupotosha ukweli.
==========

Ukweli ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa nchi ya Kikomunisti.

Ujamaa sio Ukomunisti kama watu wengi humu wanavyotaka kuaminisha

Itoshe, nyakati za the so called vita baridi(cold war) kati ya Ukomunisti wa Mashariki na Mebeberu wa magharibi, hususani wakati Urusi walivyoingia Cuba(bay of pigs saga) miaka ya 60-61 hivi, nchi nyingi zilikubaliana na kuridhia kwa kutokufungamana na upande wowote ule kati ya capitalist West na Communist East, wakihofia Vita kuu ya Tatu na Vita za kuangamizana kwa kutumia Nyuklia

Kumbuka, nchi nyingi zilikuwa kwenye nyakati na wakati mgumu kiuchumi kisiasa na kijamii baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia na hivyo hawakutaka malumbano ya kati ya Nchi ya Urusi na Marekani kuwafikia.

Kwa kifupi, hawakutaka kuchagua upande wowote ule.

Ikaundwa N.A.M Non Aligned Movement.

Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizounda movement hiyo.

Yaani, baadhi za nchi za Africa, Asia na America ya Kusini wakiwa ni miongoni mwa wanachama.

☝🏿Hiyo tunaweza kusema kuwa Tanzania hatukutaka Ukomunisti.

Na hivyo basi Mwl. Nyerere pia.

Wanaopotosha Tanzania ilikuwa ni nchi ya Kikomunisti, walaaniwe na waangazwe. Hawaitakii Tanzania mema. Ni waongo na ni wapuuzi.

Haya hivyo, Nyerere alitaka tufanane fanane kisera na kama Sweden Norway etc kwa sababu walikuwa ni wa Socialist.

Tofauti ya Ujamaa wa hizi nchi za Nordic ndio huo Mwl. Nyerere akauita African Socialism.
 
Ndugu yangu umemaliza kabisa! Mengine ni kuataka tu kumdharirisha Mwalimu.

Hata hao Kenya Mzee Jomo Kenyatta kwani alifanyaje?

Watanzania tupate akili sasa, kumlaumu Nyerere badala ya kwenda mbele na hawa wanaotukwamisha sasa hivi ni ujinga uliokithiri.

Wenzetu wakenya hawamlaumu kabisa mwasisi wao japo aliwapora karibia ardhi yote akaifanya yake binafsi. Wao wanapambana na waliopo na wanafanikiwa.

Sisi huku hata kina Lissu!! Huwa nashangaa sana...wamekosa ushawishi wa kuwaunganisha watanzania wanaishia kumlaumu Mwalimu.

Hivi wakati wa kudai uhuru mwalimu angekuwa bize kuwaponda kina mtemi Mirambo, Kimmweri, Mkwawa n.k angefanikiwa kweli??!!!
 
Alipenda sifa binafsi ndiyo maana akavuruga uandishi wa vitabu vya historia sahihi ya wapigania uhuru wa Tanganyika. Pia alivuruga uendeshaji wa vyama vya ushirika na mamlaka ya serikali za mitaa na kufuta vyama vya ushirika na mamlaka ya serikali za mitaa kwa maslahi yake binafsi.

Matokeo yake ni watawala kuendelea kufuata zile zilizoitwa fikra za mwenyekiti kama kasuku.
 
timing, wakati ule wote walikuwa communist I mean, waafrika na black people, communism ilijifanya kama ni mtetea wanyonge dhidi ya ukoloni kwa hivyo waliotawaliwa wote walikuwa attracted na communism,
☝🏿 Hayo juu hayana ukweli wowote ule. Msome Vernon McKay. Mmarekani alie andika kwa mapana kuhusu historia ya Afrika na hususani, kwanini Waafrika walikataa Ukomunisti.
nchi karibia zote za Afrika, carribean mpaka India na North Afrika walijiunga communism hivyo siyo Nyerere tu,
☝🏿Hiyo nayo sio kweli. Ni kinyume chake. Nchi za Africa, Asia, Carribean ama South Amerika waliunda kile kinachoitwa Non Aligned Movements. In essence by joining N.A.M Tanzania and many countries emphasized 'Independence and refusal to align with either Capitalist West and Communist East.'

Vernon McKay aliandika kati ya vitabu vyake na research zake kwamba "Hakuna nchi ya kiafrika itakayo kubali Ukomunisti".

Itoshe kusema hata Ethiopia, nchi moja wapo zilizo taka kukumbatia Ukomunisti, walikataa Ukomunisti.. Kama hiyo haitoshi, David Lamb katika maandiko yake "The Africans " observes, "No Doctrine, in fact, is more in conflict with the inherent character of Africa than Communism"

  • Africans are Capitalistic-kitu ambcho nimekuwa nikisema hapa mara nyingi.
  • Africans are Historically Democratic- Ukweli usiopingika mpaka pale wazungu walivyokuja kutuvuruga.
  • Africans are Individualistic
  • Africans simply do not work or produce when they are not rewarded with economic incentives-Je kuna mzungu asiyefanya hivyo? au binadamu yeyote yule?

uislamu wote au niseme nchi za kiislamu kuanzia irak, iran, syria mpaka palestina walifwata communism
☝🏿Hayo ni matango pori. Na ni propaganda za Wamarekani tu.
ndiyo maana kulikuwa na wimbi la black amerika converting to islam, kwa kifupi communism
😲😮😌
🤔 Umeyatoa wapi hayo?
iliwadanganya watu kwamba ni njia ya haki ya kujitawala.
Waafrika tulikuwa tukijitawala. Wazungu ndio walioharibu mifumo yetu. Niulize. Unarokota wapi hayo uliyoyaandika?
communism looks very good in paper lkn wengi hawajui kwamba communism ni satanic na wanaofund communism ndio hao hao wanaofund capitalism …
😮😅

Kwa kifupi ulitaka kupotosha na Propaganda.
 
Hadi leo sielewi kwann alituunganisha na zanzibar
 
Kama nilivyoandika juu huko, Nyerere alikuwa hajuwi alifanyalo, "socialism" ya Tanzania wakati wa Nyerere ni zao la Joan Wickens, Muingereza aliyekuwepo Ikulu kwa shinikizo la Uingereza, kuanzi kabla ya Uhuru mpaka kifo cha Nyerere.

Ukweli ni kuwa Nyerere alikuwa hajuwi alifanyalo, msione ile kujimwambafai mbele ya watu, alikuwa anaendeshwa na Waingereza na walikuwa na sababu zao, kumpa msishalisti ndiyo awe anamuongoza hapo Ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…