Kwanza tunafurahi sana kujua kwamba kwa sasa takwa la KATIBA MPYA ni muhimu sana, kwa hiyo waeleze wana CCM walitambue hilo.
Pili Jinai ni Jinai tu, ni lazima kiongozi wa umma ufanye kazi kulingana na Sheria za nchi, huwezi kutesa wananchi wasio na hatia kisa tu eti umetumwa pesa na Rais, kwanza hakuna DC am RC ambaye kazi yake ni kukusanya kodi ama madeni ya serikali - kwa hiyo hao wawili moto huu upo juu yao - wajibu yote waliyoyafanya sababu Sheria kwao haina kinga kama alivyo Rais na wengineo ambao wameingizwa majuzi kuogopa moto wakishatoka madarakani.
Mwisho ndugu jiunge nasi kutangaza umuhimu wa KATIBA MPYA leo na si kesho, madhara yake yameonekana wazi - madaraka ya Rais ni kufuru, Kwa mfano Rais akiwaambia TISS kwamba hataki kukuona wewe ukiisumbua Serikali yake sasa whether unaongea ukweli, urongo aisee sijui kama utafika saa 11 jioni - haya ni madaraka makubwa mno.
Vijana walioko madarakani leo naona tayari wamejifunza jambo.