Sabaya na Makonda hawastahili kushtakiwa

Waziri nalaila kiula na katibu mkuu wake Dr. Mlingwa, sembuse Hawa simbilisi? Shida ya hao vijana wa Sasa wanokuja na comment za ajabu humu hawajui chochote. Hawa Wana uwezo wa kuchangia habari za diamond, zuchu, kiba, manara kwa Mambo ya nchi hawajui kabisa
 
Pamoja na Kina hapi Gambo

Mbona viongozi wengine hawakupora watu na kuua na bado walikuwepo? Usitake kuhalalisha uchafu kwa kisingizio cha kutii mamlaka. Huyo waliyekuwa wanamtii alikuwa ni muovu mwenye madaraka, walipaswa kufanya kazi kwa mujibu sheria, na sio boss wako anataka utende uovu gani.
 
Kwa kuwa uliwapa kazi maalumu sio?
 
Kila awamu ina namna ya kuongoza Awama iliyopita imefanya Mazuri na kuna Mabaya ni katika kuongoza hicho ndicho ambacho walikuwa wanakiamini .kila awamu ikishitaki iliyopita tutamaliza sana pesa hela huko Mahakamani na haijakaa vizuri .

Tunashukuru kwa hayo mazuri, ambayo sisi tunaona sio mazuri bali wajibu, maana walikuwa wanalipwa mishahara. Na sasa acha tuchukue hatua kwa huo uovu waliofanya kwa kisingizio cha boss wao alitaka nini.
 
Kabisa, kwa hiyo.boss wao akiwaambia waibie na kuua watu ni sawa?
 
Kwanza tunafurahi sana kujua kwamba kwa sasa takwa la KATIBA MPYA ni muhimu sana, kwa hiyo waeleze wana CCM walitambue hilo.

Pili Jinai ni Jinai tu, ni lazima kiongozi wa umma ufanye kazi kulingana na Sheria za nchi, huwezi kutesa wananchi wasio na hatia kisa tu eti umetumwa pesa na Rais, kwanza hakuna DC am RC ambaye kazi yake ni kukusanya kodi ama madeni ya serikali - kwa hiyo hao wawili moto huu upo juu yao - wajibu yote waliyoyafanya sababu Sheria kwao haina kinga kama alivyo Rais na wengineo ambao wameingizwa majuzi kuogopa moto wakishatoka madarakani.

Mwisho ndugu jiunge nasi kutangaza umuhimu wa KATIBA MPYA leo na si kesho, madhara yake yameonekana wazi - madaraka ya Rais ni kufuru, Kwa mfano Rais akiwaambia TISS kwamba hataki kukuona wewe ukiisumbua Serikali yake sasa whether unaongea ukweli, urongo aisee sijui kama utafika saa 11 jioni - haya ni madaraka makubwa mno.

Vijana walioko madarakani leo naona tayari wamejifunza jambo.
 
Reactions: RNA
Umeeleweka mkuu
 
17march tulipigwa na kitu kizito kichwani tukapoteana.
Sasa tunakusanyana wapinga maendeleo kina january na nape wamewahi kutangaza ushindi. A luta continua magufulistas vinceremos ✊
 
Wacha Makonda na Sabaya pamoja na wengine wajifunze kutumia madaraka yao vizuri, walikuwa watu hovyo sana na walifurahia utawala dhalimu uliokuwepo.
 
Nao walimpenda shetani
 
naona clouds wameelewa soma
 
Hawa wanastahili Tena adhabu iwe nzito tu waliyoyafanya Ni ya kishetani sana
 
naona clouds wameelewa soma
Hawa wanastahili Tena adhabu iwe nzito tu waliyoyafanya Ni ya kishetani sana
ni mambo ya kiutawala tu ambayo mara nyingine kuyaelewa ni kazi
 
ni kweli lakin tuanze upya hizi kesi zinatumalizia pesa tu
 
Tatizo tuna rais wale wafadhili wa nje wa ngo yake ndio anaongea nao kila siku kwa simu. Utasikia 'tony blair was here last week' wakati mtu huyo ni kibaka mtumishi wa ubeberu. Au kazungumza kwa simu na mkuu wa world bank etc.
Hatuhitaji mtu anasngalia nje jinsi ya kuendesha nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…