Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Clouds kosa lao ni lipi?

Mnapigania uhuru wa kuongea ila hamtaki wenzenu waongee.

Tabia za kidkteta hizo...mtu mnataka ahukumiwe bila kujitetea.

Clouds wakihoji msiowapenda inakuwa radio mbaya.

Haya ya Sabaya ni matokeo ya uongozi dhaifu unaocheza ngoma za mitandaoni.

Kiongozi anaeshinda insta kufatilia udaku ni bomu linalosubiri kulipuka.
Bora kiongozi anayeshinda mitandaoni kwani anapata first-hand information na kujua majority ya raia wanasema nini na wanataka nini na upumbavu kiongozi kutegemea kuletawa taarifa zilizochujwa na zilizopikwa hivyo kushindwa kujua ukweli wa mambo on the ground.
Mwendazake alifikia mpaka kuwa anajifanya ameoteshwa kumbe hitmen wake wanavyokuwa kwenye mizunguko yao humletea habari watakazo na ambazo zinawalida na kuwafaidisha wenyewe.
Nchi inaenda vizuri sana kwa sasa ndiyo maana majority ya watu wana furaha sana.
 
Saa hizi unameza sweettablet huko ujue, huamini
Siamini lipi? Unapokuwa na utaalamu wa Management, la kusimamishwa Sabaya linakukoseshaje raha? Ila umeona utofauti? JPM alikiwa anaondoa kabisa! Huyu anataka kupendezesha kote. Ataweza!?
 
Siamini lipi? Unapokuwa na utaalamu wa Management, la kusimamishwa Sabaya linakukoseshaje raha? Ila umeona utofauti? JPM alikiwa anaondoa kabisa! Huyu anataka kupendezesha kote. Ataweza!?
Bora uondoshwe kabisa lakini sio alivyosimamishwa Sabaya.Sabaya akikutwa na Tuhuma si inabidi aanze kuhudhuria Kisutu
 
Mwisho wa siku anaweza kuhamishwa wilaya tu, au ndio atapewa mkoa kabisa, CCM ni ile ile.
C imesemwa anasimamishwa maana kuna tuhuma nying juu yake, au ndo anaeza pigwa jik nn 🤣🤣✔️
 
Bila shaka wakati unaponda interviews za akina Sabaya , utakuwa hapo hapo unasifia interviews za Tundu Lissu anazozitumia kujidharirisha!
Hapo kwenye kujidharirisha, ni utambulisho wa upush wako, Kwa hiyo endelea ‘kudharirika’!
 
Siku hizi hukumu zinatoka mitandaoni then zinafanyiwa maamuzi na viongozi tuliowapa dhamana.
Mambo ya ajabu kabisa kuwai kutokea duniani.
Tumetoka mbali mkuu! Kutoka malaika mkuu kutaka kuzima mitandao, hadi kuwa mahakama, Viva Melo!
 
Siku hizi hukumu zinatoka mitandaoni then zinafanyiwa maamuzi na viongozi tuliowapa dhamana.
Mambo ya ajabu kabisa kuwai kutokea duniani.
Kwaio we use watu tukupost ukiwa una halafu Mamlaka zikuache unawaza kwa kutumia matako
 
Hata yule wa Iringa pamoja na RC na RC wa Ntwara hovyo kabisa
Mama Samia akimrudisha huyu na Jerry Muro nadhani atakuwa ameshusha Imani ambayo wengi wanayo juu yake. Kuna watanzania wengi sana wanaweza hiyo ofisi sio hao wapuuzi pekee.
 
Na ndiyo maana Bwana Mungu akachukua maamuzi mapema alipoona habadiliki alipoona anazidi kuumiza watu wake. Ndipo Bwana Mungu alipoamua kung'oa mzizi mkuu kisha matawi yanyauke yenyewe na kupukutika kwa kukosa maji kutoka ardhini.

Kazi iliyobaki kwa mpanzi mpya ni kupukutisha matawi yote na kuchoma mkaa yale magogo ya mti mwovu kisha kupanda mti mpya utakao toa kivuli kwa watu wa Bwana Mungu.

Watashindana lakini hawatashinda
Amejisahau sana,unaweza kufikiri ana nia njema kumbe ni unafiki tu.
KIONGOZI ALIYEWATEUA ALIWAJENGEA KIBURI SANA.
Vitendo anavyo vifanya vya kudhalilisha,kunyanyasa kudhulumu haki za wengine,ni Kuidhalilisha mamlaka iliyomteua,bahati mbaya aliyemteua alikuwa hajali Sheria,kanuni na taratibu.
 
Au apatikane na hatia, aende gerezani, waza hilo pia!
Si utaratibu wa sisi wanaccm na serikali yetu kuwatupa wenzetu gerezani Kumbuka yule ni mwenzetu.

Kuna reference yyte ya mwanaccm kuhukumiwa na kutupwa gerezani.
 
Unless kama mamlaka za uteuzi zimekutuma ufanye Interview ile, Ila kama ni wewe binafsi umejiamulia kwenda kufanya hiyo interview basi wewe na aliyekushauri mmebugi sana.

Kubugi kwenyewe ni hivi:
1. Mnajaribu kupreempt maamuzi ya mamlaka za uteuzi kupitia propaganda.

Kwamba mnataka upande wa stori "yenu" usikike, kwamba nyinyi ni wapigania chama, kwamba yote yale ya uonevu uliyokuwa ukifanya ni kwa masilahi mapana ya chama, kwamba mkiachwa kwenye teuzi zijazo basi ni kama vile mmeonewa kwa kazi "nzuri" mliyokifanyia chama.

2. Interview yako imekaa kama promo hivi ili "mama" ajue upo na "akuelewe"
Katika tetesi hizi kuwa kuna uwezekano mama akafanya reshuffle ya wakuu wa mikoa au wilaya, timing ya interview yako ni kama vile unatuma meseji kwa rais Samia, kuwa mama nipo, nisikie, usinisahau. Sasa hii inaweza kuwa nzuri kama inafanyika kwenye nyakati za kawaida, lakini siyo timing ya sasa ambayo mama amehint kuendelea kuisuka serikali yake. Ulichokifanya ni kama mtoto anayejiimbilisha muda karibu na msosi ili Mama ajue ana njaa!. Wazazi wengine huchukia hii tabia kwa sababu ni manipulative

3. Mama Samia siyo mpenda kiki na Macamera kwa kiwango cha Mtangulizi wake, Na hii sifiasifia uliyoifanya ya "Mama atatuvusha" ni muendelezo uleule wa wateule kumsifu mteuaji ili wapate teuzi au kulinda teuzi zao. Sasa Samia ana experience ya kutosha juu ya wateule waliokuwa wakikazana kumsifu Magufuli lakini alivyokufa tuliona walivyokuwa wakishindana kuponda, na kama wasingewekeana breki hali ingekuwa mbaya sana.

4. Timing ya Interview yako na hasira za wananchi juu ya Benzi la mzee Mwinyi na kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga ni mbaya kwa aina ya viongozi kama wewe! —Nakuhakikishia Bwana Sabaya, Samia asingependa kutengeneza mtu wa aina ya Makonda alivyokuwa kipindi cha Magufuli. Sababu mojawapo ya Magufuli kupoteza mvuto wa kusiasa mwishoni mwa waka 2016 hadi mwishoni mwa mwaka 2018 ni kwa kumkubatia Makonda. Sasa Samia keshaonja hasira na shombo za wananchi katika matukio hayo mawili niliyoyataja, Sasa mtu wa rekodi zako itamfanya Samia afikirie mara mbilimbili kukuteua maana keshaijua hasira ya wananchi inaweza kuwa kali kiasi gani.

Siku nyingine, Ukitaka kufanya Interview kama hii ya kujikosha, hakikisha unaleta na mtu mwingine wa kuzugia ili mhojiwe nyote, ungeleta hata mkuu wa wilaya mwingine mkahijiwa nyote wawili lakini focus ikawa kwako, La sivyo Interview yako ni pure propaganda, ni nanipulative na ni ya kutafuta kiki.

Clouds nao watumiage akili wakati mwingine wasitumike kisiasa, wanajishusha sana
Hahaha. Aisee umeona mbali sana bro . Ubarikiee
 
Screenshot_20210514-155004.png
 
Back
Top Bottom