Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Hiki kituo kimekosa mkurugenzi wa vipindi,tangu Boss Ruge afariki,kituo kimeyumba sana,
Nakumbuka ishu ya shirawadu walipotakiwa warushe mahojiano Kati ya mwanamke anayedai alizaa na Gwajima,harafu akatelekezwa,Ruge aliwauliza vijana wa shiradu kama 'wamebalance story kwa kuhoji upande wa pili,yaani Gwajima mwenyewe,vijana wakasema hawajaweza kuongea na Gwajima,Ruge akawashauri wasirushe kipindi hewani mpaka story ibalance,kwa kumuoji Gwajima,kipindi hakikurushwa mpaka mweu mmoja Makonda alipovamia kituo na kulazimisha
 
Screenshot_20210514-160817_1620998521648.jpg

Hio trela tu
 
Hiki kituo kimekosa mkurugenzi wa vipindi,tangu Boss Ruge afariki,kituo kimeyumba sana,
Nakumbuka ishu ya shirawadu walipotakiwa warushe mahojiano Kati ya mwanamke anayedai alizaa na Gwajima,harafu akatelekezwa,Ruge aliwauliza vijana wa shiradu kama 'wamebalance story kwa kuhoji upande wa pili,yaani Gwajima mwenyewe,vijana wakasema hawajaweza kuongea na Gwajima,Ruge akawashauri wasirushe kipindi hewani mpaka story ibalance,kwa kumuoji Gwajima,kipindi hakikurushwa mpaka mweu mmoja Makonda alipovamia kituo na kulazimisha
Walichemka sana kufanya ile intavyuu juzi. Kwanza wakati haikua sahihi kwa fukuto lililopo na pia hawakubalance sijui walikua na lengo gan
 
Unless kama mamlaka za uteuzi zimekutuma ufanye Interview ile, Ila kama ni wewe binafsi umejiamulia kwenda kufanya hiyo interview basi wewe na aliyekushauri mmebugi sana.

Kubugi kwenyewe ni hivi:
1. Mnajaribu kupreempt maamuzi ya mamlaka za uteuzi kupitia propaganda.

Kwamba mnataka upande wa stori "yenu" usikike, kwamba nyinyi ni wapigania chama, kwamba yote yale ya uonevu uliyokuwa ukifanya ni kwa masilahi mapana ya chama, kwamba mkiachwa kwenye teuzi zijazo basi ni kama vile mmeonewa kwa kazi "nzuri" mliyokifanyia chama.

2. Interview yako imekaa kama promo hivi ili "mama" ajue upo na "akuelewe"
Katika tetesi hizi kuwa kuna uwezekano mama akafanya reshuffle ya wakuu wa mikoa au wilaya, timing ya interview yako ni kama vile unatuma meseji kwa rais Samia, kuwa mama nipo, nisikie, usinisahau. Sasa hii inaweza kuwa nzuri kama inafanyika kwenye nyakati za kawaida, lakini siyo timing ya sasa ambayo mama amehint kuendelea kuisuka serikali yake. Ulichokifanya ni kama mtoto anayejiimbilisha muda karibu na msosi ili Mama ajue ana njaa!. Wazazi wengine huchukia hii tabia kwa sababu ni manipulative

3. Mama Samia siyo mpenda kiki na Macamera kwa kiwango cha Mtangulizi wake, Na hii sifiasifia uliyoifanya ya "Mama atatuvusha" ni muendelezo uleule wa wateule kumsifu mteuaji ili wapate teuzi au kulinda teuzi zao. Sasa Samia ana experience ya kutosha juu ya wateule waliokuwa wakikazana kumsifu Magufuli lakini alivyokufa tuliona walivyokuwa wakishindana kuponda, na kama wasingewekeana breki hali ingekuwa mbaya sana.

4. Timing ya Interview yako na hasira za wananchi juu ya Benzi la mzee Mwinyi na kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga ni mbaya kwa aina ya viongozi kama wewe! —Nakuhakikishia Bwana Sabaya, Samia asingependa kutengeneza mtu wa aina ya Makonda alivyokuwa kipindi cha Magufuli. Sababu mojawapo ya Magufuli kupoteza mvuto wa kusiasa mwishoni mwa waka 2016 hadi mwishoni mwa mwaka 2018 ni kwa kumkubatia Makonda. Sasa Samia keshaonja hasira na shombo za wananchi katika matukio hayo mawili niliyoyataja, Sasa mtu wa rekodi zako itamfanya Samia afikirie mara mbilimbili kukuteua maana keshaijua hasira ya wananchi inaweza kuwa kali kiasi gani.

Siku nyingine, Ukitaka kufanya Interview kama hii ya kujikosha, hakikisha unaleta na mtu mwingine wa kuzugia ili mhojiwe nyote, ungeleta hata mkuu wa wilaya mwingine mkahijiwa nyote wawili lakini focus ikawa kwako, La sivyo Interview yako ni pure propaganda, ni nanipulative na ni ya kutafuta kiki.

Clouds nao watumiage akili wakati mwingine wasitumike kisiasa, wanajishusha sana
Mkuu wa wilaya unafanyaje interview as if unauza sera kama mwanasiasa? DC sio mwanasiasa ni mtendaji wa serikali anafanyaje Ile interview? Ni ujinga umemponza na ujangili wake.
 
Clouds kituo kisichosoma Alama za nyakati....Ruge was best pale. ..zamani vituo vingine vilikuwa vinacopy ubunifu wa clouds lakini wao wamegeuka mabingwa wakucopy kutoka vituo vingine. Wanapwaya Sana...wawasukuru watangazaji wachache Kama akina masoud otherwise hiyo media ingekuwa taabani zaidi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom