Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Sabaya ungekuwa 'Smart' usingefanya Interview na Clouds FM kipindi hiki

Upendo ni mhimu sana,
Iwe katika raha na taabu,
Iwekwe ratiba yakupeleka chai Kwa Sabaya.

2797438_FB_IMG_16220064027833658.jpg
 
Ukimuona boss yeyeto ni mkali Sana na ujifanya ni smart Sana jua kuna uhalifu anauficha.Sabaya ni jiwe type.
 
NARUDIA TENA, KWA VICHWA VILIVYOMO HUMU , NASHAURI JAMII FORUM IWE TOVUTI YA KITAIFA.

VIONGOZI WA KISIASA NA SERIKALI WAPITIE HAPA WAJIFUNZE MAMBO MBALI MBALI.

PIA IWEPO VERSION YA WANAFUNZI AU WATOTO YAANI JF KIDS ILI WANAFUNZI WAJIFUNZE MASOMO YAO HUMU. IKIWEZEKANA IINGIZWE KWENYE MITAAALA YETU

AHSANTE
Hao watoto waanze kupelekwa Uzi wa Kula Tunda Kimasihara kwanza!
 
Unless kama mamlaka za uteuzi zimekutuma ufanye Interview ile, Ila kama ni wewe binafsi umejiamulia kwenda kufanya hiyo interview basi wewe na aliyekushauri mmebugi sana.

Kubugi kwenyewe ni hivi:
1. Mnajaribu kupreempt maamuzi ya mamlaka za uteuzi kupitia propaganda.

Kwamba mnataka upande wa stori "yenu" usikike, kwamba nyinyi ni wapigania chama, kwamba yote yale ya uonevu uliyokuwa ukifanya ni kwa masilahi mapana ya chama, kwamba mkiachwa kwenye teuzi zijazo basi ni kama vile mmeonewa kwa kazi "nzuri" mliyokifanyia chama.

2. Interview yako imekaa kama promo hivi ili "mama" ajue upo na "akuelewe"
Katika tetesi hizi kuwa kuna uwezekano mama akafanya reshuffle ya wakuu wa mikoa au wilaya, timing ya interview yako ni kama vile unatuma meseji kwa rais Samia, kuwa mama nipo, nisikie, usinisahau. Sasa hii inaweza kuwa nzuri kama inafanyika kwenye nyakati za kawaida, lakini siyo timing ya sasa ambayo mama amehint kuendelea kuisuka serikali yake. Ulichokifanya ni kama mtoto anayejiimbilisha muda karibu na msosi ili Mama ajue ana njaa!. Wazazi wengine huchukia hii tabia kwa sababu ni manipulative

3. Mama Samia siyo mpenda kiki na Macamera kwa kiwango cha Mtangulizi wake, Na hii sifiasifia uliyoifanya ya "Mama atatuvusha" ni muendelezo uleule wa wateule kumsifu mteuaji ili wapate teuzi au kulinda teuzi zao. Sasa Samia ana experience ya kutosha juu ya wateule waliokuwa wakikazana kumsifu Magufuli lakini alivyokufa tuliona walivyokuwa wakishindana kuponda, na kama wasingewekeana breki hali ingekuwa mbaya sana.

4. Timing ya Interview yako na hasira za wananchi juu ya Benzi la mzee Mwinyi na kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga ni mbaya kwa aina ya viongozi kama wewe! —Nakuhakikishia Bwana Sabaya, Samia asingependa kutengeneza mtu wa aina ya Makonda alivyokuwa kipindi cha Magufuli. Sababu mojawapo ya Magufuli kupoteza mvuto wa kusiasa mwishoni mwa waka 2016 hadi mwishoni mwa mwaka 2018 ni kwa kumkubatia Makonda. Sasa Samia keshaonja hasira na shombo za wananchi katika matukio hayo mawili niliyoyataja, Sasa mtu wa rekodi zako itamfanya Samia afikirie mara mbilimbili kukuteua maana keshaijua hasira ya wananchi inaweza kuwa kali kiasi gani.

Siku nyingine, Ukitaka kufanya Interview kama hii ya kujikosha, hakikisha unaleta na mtu mwingine wa kuzugia ili mhojiwe nyote, ungeleta hata mkuu wa wilaya mwingine mkahijiwa nyote wawili lakini focus ikawa kwako, La sivyo Interview yako ni pure propaganda, ni nanipulative na ni ya kutafuta kiki.

Clouds nao watumiage akili wakati mwingine wasitumike kisiasa, wanajishusha sana
Clouds wamekosa weledi sababu ya kuendekeza njaa
 
Hovyo kabisa, sielewi ni kwanini wameporomoka hvyo mwanzo walikua wana weledi katika kazi zao. Sitaki kuamin kua Ruge ndio alikua kila kitu pale.
kaondoka na clouds yake. ni kama creativity na weledi umesepa nae
 
Siamini lipi? Unapokuwa na utaalamu wa Management, la kusimamishwa Sabaya linakukoseshaje raha? Ila umeona utofauti? JPM alikiwa anaondoa kabisa! Huyu anataka kupendezesha kote. Ataweza!?
kwamba sabaya kushtakiwa ni kupendezesha watu?
utawala huu unafuata sheria. uliopita haukua una favour sheria zilizopo. ni mtu ana amua tu. tawala haziwez fanana kimaamuzi
 
Sabaya ni mjinga..hana mtoto,hana mke hana makazi ya kudumu. He is just a foolish young man. Kajimaliza
 
Hao nao ninawsiwasi wapo wanufaika wa hayo mauzauza. Wachunguzwe kwa rushwa
 
Hao nao ninawsiwasi wapo wanufaika wa hayo mauzauza. Wachunguzwe kwa rushwa
wapo watangazaji 3 wa clouds 360, PJ, Sasali na Kija sasa kati ya hao unadhani nani anaweza akawa amevuta mpunga ili mahojiano na sabaya yakafanyika?
tusije tukawa tunawalaamu kumbe hakuna kitu.
 
Mwisho wa siku anaweza kuhamishwa wilaya tu, au ndio atapewa mkoa kabisa, CCM ni ile ile.
Hakuna kitu kama hicho mkuu, huyo ndio mwisho wake wa kisiasa. Madam Sasha hawezi kujitia doa kumpa nafasi yeyote ile.
 
Back
Top Bottom