Sadaka kumpa mzazi ni bora kuliko kuipeleka kwenye nyumba za ibada

Ukigundua nyumba za ibada ni biashara, hakika utawapa wazazi hiyo pesa ya sadaka. Au masikini unaemfahamu. Sijui timefungwa akili! Kila siku naangalia hapa Tanganyika perkers, watu wanavyomiminika na sadaka zao. "Ee baba wa Mbinguni tunasue na hili janga"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka walawi wakale wapi?mana maandiko walawi walipewa kazi ya kuhudumu kwenye hekalu...pia hawakupewa urithi kati ya makabila ya wana wa Israel.

Hivyo walawi watakula madhabahuni.

Halafu injili itawafikiaje wasio amini kama injili ikinuka umasikini ?..leteni fedha makanisani ili kuisukuma injili isonge mbele wengi waokolewe na wampokee kristo.

#MaendeleoHayanaChama
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Asante kwa ujumbe huu
Makanisa ni kama matapeli wengine tu
 
Anyway swali la kujiuliza:Hizi sadaka tunazotoa kanisani uwa zinaenda wapi?Imagine,mimi nilitegemea tukitoa sadaka angalau kiasi fulani kiwasaidie wahitaji wenye shida maalumu Mf watoto yatima,wajane wasiojiweza,watoto walio ktk mazingira magumu nk. But KINYUME chake kikifika kipindi cha kuwatolea wahitaji kanisa linaomba michango mengine ili tuwapelekee wahitaji.
Tuanajenga kanisa hili kwa pesa zetu wenyewe,but sadaka inatokomea kusikojulikana,matokeo yake utamkuta mchunguzi anamiliki V8,Watoto wake wanasoma International schools wakat wa kwako unakosa unakosa hata pesa ya bajaji ili waende Kayumbaz schools.
Hii nayo ni chuma ulete
 
Kwaiyo mitume wa kileo hawana urithi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afu kuna watu wanakuunga mkono kabisaaa kua uko sahihi?
Kama hawajawahi kusoma Bible na Qurani mtakua pamoja, ila najua mtoa mada ni mpagani, vinginevyo ni wivu tu unakusumbua.
 
1. Nakubali ni vyema kuwasaidia wazazi kabla ya kuweka heshima huko kwenye nyumba za ibada.
2. Kuna wazazi ukiwapa hiyo hela wanaipeleka kanisani,/msikitini, vikoba visivyo na maana n.k
3. Kuna wale watalewa hadi wadhoofike hawa tuwe nao makini.
 
Afu kuna watu wanakuunga mkono kabisaaa kua uko sahihi?
Kama hawajawahi kusoma Bible na Qurani mtakua pamoja, ila najua mtoa mada ni mpagani, vinginevyo ni wivu tu unakusumbua.
Quran imetofautisha sadaka zaka. Zaka ni lazima na ni moja ya nguzo ya uislam. Na unatakiwa kutoa kila unapopata mavuno au kipato. Quran 17:26 na 30:38 inaelekeza zaka zipelekwe kwa wazazi maskini, ndugu maskini, watoto yatima, wagonjwa wasiojiweza, ambao hawana makazi ya kuishi. Sadaka ni hiari. Quran 9:60 inaelekeza kutoa sadaka kwa hiari . Sadaka ziende kwa wanaozikusanya hapa namaanisha wanaohudumia miskiti, kuwakomboa watumwa waliomateka, masikini walio na madeni na wahitaji wengine.
 
Mama hapewi Sadaka. Hapo unamtunza Mama yako ni wajibu.

Sadaka peleka kanisani au kwa mganga Kama unamahaba na ibrisi
 
Reactions: J C
1 Kor 15:34 Amkeni kwa njia ya uadilifu na msiwe na mazoea ya kufanya dhambi, kwa maana wengine hawamjui Mungu.
 
Kuna baraka za kumpa pesa mzazi na kutoa sadaka kanisani..

Malaki 3:10
Leteni zaka kamili nyumbani mwa Bwana...
 
Asante kwa ujumbe huu
Makanisa ni kama matapeli wengine tu
Nietoa ushauri sio k2a sababu makanisa ni wizi,bali ni kwa sababu wqzazi wanahitaji zaidi
 
Kuna baraka za kumpa pesa mzazi na kutoa sadaka kanisani..

Malaki 3:10
Leteni zaka kamili nyumbani mwa Bwana...
Kama mtu una pesa zako sio tatzo,ila tatizo ni kuwa mtu anajibana kumpa mzazi eti kisa kingine akatoe kanisani wakati huo anachompa mzazi hakitoshi.

Au mtu hampi kabisa mzazi mpaka akiomba,ila kanisani anatoa hata asipoombwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…