Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini

Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini

Juzi Bi. mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe huwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
Tatizo mnaolalamikia sana sadaka hamtoi sadaka, ila waganga wanawakamueni kichizi
 
Wanakuaga kama wamepumbazwa akili. Huwaambii kitu hadi aje kushtuka it's too late
Halafu wakitoka huko wanarudi na wese, maji na chuvi wamevinunua kutoka vibaraza vya upako.
Wanajimaliza juu chini.

Demi tuanzishe kanisa, wewe mhubiri mie mhesabu sadaka😇
 
Natoa Rai kuw msingatieni Sana mwamposa msimpuuze Kuna kitu ndani yake ambayo wengi hawana

Mm Sina neno nao Kama Ni wa mungu bas sawa Kam si nabii wake ni tapeli ila nijuacho mm anakitu ndani yake
Shuhuda zake azielezeki maelfu humfata je Ni Nani huyu
ana nguvu kumzidi aliyemuumba..
 
kuna mke wa mtu huko kigamboni dar es salaam alipewa ahifadhi milioni kumi 10 ya maendeleo, mwanamke akaenda kujimaliza na milioni 10 kwa mwamposa, mumewe alipoitaka pesa akaambiwa nimejimaliza baada ya siku tatu ntarudishiwa, jamaa akafura kama Mamba, akazama kwa mwamposa akapiga bonge la mkwara akarudishiwa pesa yake, ni habari very recent
Aiiseee
 
Halafu wakitoka huko wanarudi na wese, maji na chuvi wamevinunua kutoka vibaraza vya upako.
Wanajimaliza juu chini.

Demi tuanzishe kanisa, wewe mhubiri mie mhesabu sadaka[emoji56]
Unadhani rahisi hivyo..halafu wengi mnajisema huku hajakutana na matatizo..siku ukipata majanga ya dunia ndio utajua hujui utatafuta msaada popote pale.

#MaendeleoHayanaChama
 
manabii wa kula keki na kukanyaga mafuta ya nazi , halafu wanashushia na maji ya canadian, duh hatari sana kweli wajinga wameendelea kuwa wengi sana nchini
Wewe hapo ndio unajiona mjanja...ukute na wewe kina mahali wajanja wanakutafuna vzr tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Juzi Bi. mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe huwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
😁😁😁 bi mkubwa aliulizwa : Mama na wewe huwa unajimaliza

akajibu: ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka 😁😁😁

yanafurahisha ila yana huzunisha
 
Unadhani rahisi hivyo..halafu wengi mnajisema huku hajakutana na matatizo..siku ukipata majanga ya dunia ndio utajua hujui utatafuta msaada popote pale.

#MaendeleoHayanaChama
Imani haiuzwi.
Mungu hakutudai fidia yeyote kwa kifo cha Mwanae aliyejitolea uhai wake kwa ajili yetu.

Kwa nini shida za wagu zitumike kama kigezo chabkujikusanyia faida?

Mathayo 10:8
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
 
Naamini iko siku serikali yetu itamchukulia,hatua huyu mchungaji sijui Nabii! Kwani sasa kaingia kwenye utapeli kwa kujificha kwenye Neno la Mungu, au afanye ziara Rwanda akakutane na mkono wa Chuma wa Kagame
Haitakaa itokee huyo ana nguvu za ajabu. Ni Mungu tu atamuadhibu
 
Ila wewe jamaa bhana[emoji3] Mbn unakuwa kama Konda unawadanganya wenzako kama upo nao pamoja wakishapanda gari wewe unaenda grocery kuvuta sigara kusubiria gari ijae[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Yaani mtu akikufuata wewe kapotea huku anajiona maana unashawishi huku kichwani unajua kinachoendelea[emoji16][emoji16]

#Maendeleo yana Chama....
Hahahahah konda anakwambia siti zipo za kukaa, jichanganye sasa utajua hujui. 😂
 
Nilienda kwa Mwamposa miaka michache iliyopita nilikuwa.....

Kule nilikutana na slay queens wa zamani, wadada waliowahi kujichubua, waliovaa kwa stara ila wana tattoo likely from their previous lifestyle, wavaa ushungi. Mambo ya uongo na kweli ya kutosha kule. Natamani nirudi nione kinachoendelea

hukuomba namba?....kama hukuomba namba wewe ni bwege.
 
kuna mke wa mtu huko kigamboni dar es salaam alipewa ahifadhi milioni kumi 10 ya maendeleo, mwanamke akaenda kujimaliza na milioni 10 kwa mwamposa, mumewe alipoitaka pesa akaambiwa nimejimaliza baada ya siku tatu ntarudishiwa, jamaa akafura kama Mamba, akazama kwa mwamposa akapiga bonge la mkwara akarudishiwa pesa yake, ni habari very recent
Mimi namuacha kbsa kama mke ni wa namna hii
 
Kwanini serekali ipisige marufuku haya mavitu

Kuna nini nyuma ya Panzia?
 
Imani haiuzwi.
Mungu hakutudai fidia yeyote kwa kifo cha Mwanae aliyejitolea uhai wake kwa ajili yetu.

Kwa nini shida za wagu zitumike kama kigezo chabkujikusanyia faida?

Mathayo 10:8
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Kumbe kuna wenye uwezo wa kuwafufua wafu?! Kama nani aliwahi kufanya hivyo?
 
Imani haiuzwi.
Mungu hakutudai fidia yeyote kwa kifo cha Mwanae aliyejitolea uhai wake kwa ajili yetu.

Kwa nini shida za wagu zitumike kama kigezo chabkujikusanyia faida?

Mathayo 10:8
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Acha kukariri maisha..unataka hiyo ministry ijiendeshe vipi usawa huu wa magari..ambapo kila kitu ni pesa..Yesu kristo alikua na wahasibu kwajili ya kutunza mfuko wa fedha ili kuwezesha injili...au hufahamu kazi ya Yuda iskariote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom