Huu ni upotoshaji tuu wa Raia Mwema, hakuna kitu kama hicho, ukweli ni huu
Mkuu
Makonyeza , asante sana kwa bandiko hili. Kiukweli baadhi ya wetu wana ushetani wa ajabu, watu wamehamanika binadamu wenzetu wanapopata matatizo, wanashangilia afikishwe kwa Pilato.
Kitu cha ajabu sana kuhusu gazeti la Raia Mwema, Mwenyekiti wa bodi ya uhariri ni mwanasheria, hivyo anaelewa kila kitu lakini sijui kwa nini anaacha gazeti lake lipotoshe!.
Kuna jinai za aina mbili,
1. Public criminal liabilities, kufanya jinai ya umma, ambazo lazima ziwe prosecuted na public prosecutor.
2. Kuna jinai za Private, or personal criminal liabilities, hizi ni jinai binafsi, kama wizi, kubakwa, kuvamiwa, personal injury, criminal trespass etc, hizi hatua ya kwanza ni kwa mtendewa kulalamika kwa kwenda kuripoti polisi na kufunguliwa RB.
Mwanamke akibakwa, asiposhitaki kwamba amebakwa, then atahesabika ameridhia, unless she is a minor.
Kitendo alichofanya Makonda kuvamia CMG ni criminal trespass, ili iwe ni jinai ilibidi Clouds wakaripoti polisi, walalamike. Ni jukumu la ofisi ya DPP kushughulikia malalamiko hayo na kuyafanyia uchunguzi.
Lakini kwa uvamizi ule, Clouds TV hajalalamika popote, hajaripoti polisi wala kufungua mashitaka yoyote.
Iwapo Clouds wangeripoti polisi na kupewa RB, kisha polisi na DPP wakaona hakuna jinai, then Clouds ndio wakaamua kumuajiri a private prosecutor, na kumfuata Kubenea, then hapo ndipo Kubenea angekuwa na locus stand to apply to institute a private criminal investigation na kuleta private criminal case against Makonda.
Ili mtu uwe ni private investigator lazima utumwe na kuajiriwa kama wafanyavyo kwa mawakili. Sasa kwenye hili la Kubenea, katumwa na nani?.
Kama Kubenea ni raia mwema wa JMT, na ameona jinai imetendeka na serikali imeshindwa kuchukua hatua, Kubenea would have made a lot of sense kama ange launched a private prosecution kwa niaba ya Shambulio la Lissu.
Watu wamehamanika bure, hakuna lolote la maana kwenye shauri hili, linapigwa chini day one ya kusikilizwa!.
Hivyo hoja zangu kwenye bandiko hili
Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!. bado ziko valid and still stands