Ni wapi mimi nimekataa maelezo ya Kubenea? nimekwambia maelezo yake hayo ndiyo yamesababisha apelekwe mahakamani sababu yanatofatiana na ushahidi wa nyaraka alizokutwa nazo na upelelezi uliofanywa na Polisi. Ugumu uko wapi kuelewa hapo?
Nani kakuambia sijaelewa?! Mjadala wetu ulianzia hapa, kwa kauli yako mwenyewe ulisema:-
Wakati mwingine mnajitoa ufahamu. Mtuhumiwa ameingia na kutoka nchini Kenya bila taarifa zake kuwapo mpakani. Ushahidi ni risiti ya Hotel aliyolala Nairobi, Memorandum of Understanding iliyosainiwa Nairobi na tiketi ya basi alilopanda toka Nairobi kwenda Namanga, unashangaa nini? maana yake Usafiri wake wa kwenda na kurudi ulikuwa ni wakuishia Namanga na kisha kuvuka kutumia njia za Panya, njia haramu.
Nikakuuliza ina maana risiti, tiketi na MoU zinaweza kuwa ushahidi kwamba aliingia na kutoka KE kinyemela?! Nikakuuliza what if hizo risiti na tickets alikuwa nazo in advance ili tu baadae avute mpunga ofisini kuonesha alisafiri hadi KE na kulala hotelini lakini hakwenda KE na badala yake hata hiyo MoU na fedha aliletewa na mtu from KE hadi mpakani?!
Baada ya kukuuliza hayo, wewe mwenyewe tena ukadai:-
Kumbuka Kubenea ametoa maelezo Polisi. Hayo uyasemayo siyo maelezomaliyotoa Polisi. Don't make speculations
Nami nikakuambia unachosema wewe sio maelezo ya Kubenea bali ni maelezo ya DPP kwa sababu Kubenea amesema hakwenda Kenya, lakini "uchunguzi" wa DPP ndio unadai alienda Kenya kwa kutumia kigezo cha risiti na tiketi kama ulivyokuwa umesema wewe!
Ni maelezo ya Kubenea aliyotoa polisi au ni maneno ambayo DPP anadai ni matokeo ya uchunguzi wao?
Kwa maana nyingine, unapohoji "...
Ni wapi mimi nimekataa maelezo ya Kubenea?" Hapo tayari inaonesha umekana maelezo ya Kubenea ambayo anasema hajaenda KE lakini unachukua maelezo ya DPP ambae ndie anasema Kubenea alienda Kenya!!!
Maelezo yake anadai alifikia Hotelini na kisha kwa kaka yake, hotelini aliyotaaja hakuna rekodi yake kwenye register na kaka yake hana taarifa.
Bado hiyo haithibitishi kwamba alienda Kenya!QUOTE="Chige, post: 36615451, member: 12993"]Kuna nyaraka za hotel aliyofikia Nairobi na tiketi yenye jina lake aliyosafiria toka Nairobi. [/QUOTE] Again, tiketi na risiti peke yake havithibitishi kwamba alienda Kenya! Aidha, wakati DPP anaeleza kwa kujiamini kabisa kwamba:
1. Mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA hakufikia katika hoteli aliyoitaja Arusha mjini, wala kulala kwa Kaka yake kama alivyoeleza.
Kwa upande mwingine ameshindwa kusema kama SAED AHMED KUBENEA alifikia katika hotel ya kule Nairobi, na badala yake ameishia kusema:-
Mara baada ya upekuzi, mtuhumiwa huyo alikutwa, pamoja na vitu vingine.... Risiti ya malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya yenye jina la Kubenea, Saed Ahmed kama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020 hadi 5/9/2020 na. Pasi yake ya kusafiria (Passport).
Hapo inaonesha wazi wala hawana ushahidi kwamba alilala kwenye hiyo hotel zaidi tu ya ku-assume kwavile walimkuta na risiti ya hoteli husika basi alilala kwenye hiyo hotel!Lakini pia hakuna taarifa mpakani ya yeye wala mgeni wake anayedai kumletea pesa kuwa alivuka mpakani.[/QUOTE] Sasa taarifa zake zitakuwa vipi mpakani wakati anasema hakwenda Kenya?! Na kuna wakati nilikuuliza kama huyo jamaa wa Kenya alifunga pesa na docs zingine sehemu moja, kisha alipofika mpakani upande wa KE, hicho kifurushi alikirusha upande wa TZ alikokuwa Kubenea, ina maana hapo Kubenea atakuwa aliingia Kenya hadi mtake kukuta taarifa zake mpakani?
Hutaki kuamini ya wataalam waliopeleleza bali unatulazimisha tuamini ya mtuhumiwa na assumptions zako !!!
Weka hapa maelezo ya hao watalaamu yanayothibitisha kwamba alilala kwenye hiyo hotel huko Kenya!
tusubiri maamuzi ya Mahakama tuache kutengeneza dhania, ati alitaka kuwaingiza mkenge wabia wake.
Acha kufanya exaggeration... nimekuambia what kama hizo risiti alitaka ku-claim malipo kutoka kwa wabia wenzake?! Issue ni kwamba, kuwa na risiti HAKUTHIBITISHI kwamba alilala kwenye hotel husika, na kuna possibilities nyingi tu zinazoweza kumfanya awe na hiyo risiti lakini bila kulala hotel husika!!!