Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Atakuwa alienda kutafuta pesa za kufanyia kampeni, huu mchoro inawezekana atakuwa amechomwa na mtu wake wa karibu, kosa limefanywa kuwa kubwa kwasababu ya nafasi yake aliyokuwa nayo kisiasa, hapo hakuna dhamana na ndoto za ubunge ndio zimekwisha.
 
We akili huna, hata kama wewe ni mtanzania kuna namna ya kuingia tanzania. Njia ya kuingia Tanzania ni kupotia mpaka rasmi. Sasa yeye kaingia kupitia isivyo halali, ni lazima akamatwe kwa kuwa hawajui kabeba nini
Hapa ndipo ninapokuona wewe ni wakili kanjanja, inawezekana vipi umkamate raia wa Tanzania ndani ya Tanzania na halafu umshtaki kwa kuingia Tanzania isivyo rasmi? Are you mad?

Hivi huko CCM huwa mnavutishwa bangi gani ya kuwatowa akili?
 
Ninadhani amekuwa decoyed kama Kagame alivyofanya kwa Paul Rusesabagina (Hotel Rwanda Oscar Award recipient) hivi karibuni.

Pole Camaradie Kubenea utakuwa ulikwenda kusaka pesa za kampeini, ila siku hizi hawa jamaa wameziba na kufuatilia udhibiti wa kila mwanya/njia inayoweza kutoa upenyo kwa upinzani kupata uwezo wa kuendesha kampeini zao, ingawa wao waliisha kuvuna pesa za kampeini kupitia kwa mkataba wa akina Thobias Andengenye na Lugola, pamoja na mkataba wa manunuzi ya mbolea kupitia kwa wizara ya kilimo (Japhet Hassunga anahusika).
 
Hapo shitaka ni kuingiza pesa za kigeni kinyume na taratibu.
Ndio maana nimekwambia hii ni kesi dhaifu, hakuna ushahidi wa passport ya Kubenea kutoka nje ya nchi.

Hakuna kosa lolote ndani ya Tanzania kulipana pesa kwa foreign currency.

Dpp hawezi kushinda kesi hii kwenye court of law. Ni kesi ya hisia tu kuliko uhalisia.

Mahakamani lazima uiridhishe mahakama pasi na shaka yoyote jinai iliyotendwa na mshtakiwa.
 
Back
Top Bottom