Saed Kubenea awaonya wabunge wanaoshinda mitandaoni wakiitukana Serikali

Saed Kubenea awaonya wabunge wanaoshinda mitandaoni wakiitukana Serikali

Amani iwe nanyi.

Leo wakati akichangia bajeti bungeni mbunge wa Ubungo kupitia chama cha democrasia na maendeleo (Chadema) Saed Kubenea amewaonya wote wanaoitukana serikali na kuwataka watambue dhamana kubwa walizopewa na wananchi za kuwa wabunge.

Saed Kubenea ametolea mfano kuna baadhi ya wabunge wanashinda Twitter wakibeza na kutukana hovyo serikali huku wakisahau kuwa wabunge hao wamepewa heshima kubwa na wananchi ya kuwa bungeni kuishauri na kuiunga mkono serikali.

My take .

Kwa hili pamoja na kwamba elimu ya Saed Kubenea ni ya hapa na pale lakini anaonekana ana akili nyingi mno na maarifa kuwazidi wabunge wengi wa chadema ambao badala ya kushinda majimboni wakitimiza ahadi zao ,badala yake wamegeuza Twitter ndiyo majimbo yao ya kuvurumishia matusi na kutetea mafisadi na mabeberu kama ile sinema ya tutashitakiwa MIGA.



Sent using Jamii Forums mobile app

Huyu Kubenea ni kati ya watu ambao wananunuliwa na fedha. Mwaka 2006-7 alimwagiwa tindikali na watu anaowajua. Kisha wakampoza na fedha kidgo na kumlipia matibabu India. Tusimzingatie sana kwa vile Kubenea na Mbatia wana bei kama malaya wa Kimboka Bar pale Buguruni
 
Waliotia nia kugombea ubunge kupitia CHADEMA;

Jimbo la Ubungo waliojitokeza ni saba kati yao ni mbunge wa sasa, Saed Kubenea na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye tayari ametangaza kutogombea udiwani alioutumikia kwa miaka kumi mfululizo.
 
Elimu ya hapa Na pale, serikali ikifanya ya hovyo itakosolewa tu.
 
Back
Top Bottom