Tetesi: Saed Ramovic ndiyo kocha mpya wa Yanga

Mpira sifuatiliagi Sana me Mambo yangu Mapenzi tu lakini mbona mtoa mada yupo smart Sana amewachambulia kila kitu
 
Wewe mpira hujui, sio siku nyingi ulikuwa unamsifia Manqoba kwa nyuzi mfululizo wakati watu tunashaona dalili mbaya tokea mechi na Gaborone na Geita ila wewe ulituona sisi hatujui mpira. Mechi na TRA ukaja kugeuka maneno kuwa Manqoba umeshindwa kumtetea. Ni wazi bado mchanga sana kwenye haya mambo ya uchambuzi wa mbinu na kiufundi. Au pengine umeletwa hapa utetee kwa kila wanachofanya viongozi wako. Muda utaongea kama nilivyokwambia kwa Manqoba narudia tena kwa huyu Saed Ramovic hamna kocha hapa wa kuipa Yanga mafanikio
 
Wewe unafuata mkumbo hebu nipe facts tatu zinazokufanya umkatae German machine saed ramovic
Mkumbo wa nini sasa?

Kwani ni mimi peke yangu ndio ninayemkataa Ramovic?

Mashabiki wengi wa Yanga wanaona kocha sahihi kurudi Jangwani ni Nabi,Miloud au Gamondi.

We unafikiri hawamuoni huyo tapeli wako Saidi mnyamwezi?

Haya facts tatu zangu kwanini Side mnyamwezi sio kocha sahihi kwa Yanga ni hizi hapa.

1.Mbinu duni za kizifungua timu zinazopaki basi.

Kocha wako alishindwa kuja na mbinu za kucheza na MC Alger ambao walijilikana kabisa kwamba wanakuja Dar kujilinda zaidi kuliko kushambulia.

Na kweli walijilinda kwa dakika zote 90 bila ya Yanga kupata hata goli moja hali iliyopelekea Yanga kutolewa klabu bingwa hatua ya makundi.

2.kuamini kwenye rigid system,high intensity football na high pressing wakati wachezaji wa Yanga aliowakuta na ambao mpaka sasa wapo wameshazoea possession based football kuanza mashambulizi kutokea nyuma(build up) na ku exploit open spaces(vishimo) vinavyoachwa na wapinzani.

Ndio maana mtu kama Miloud alichukua wiki 2 tu kuirudisha timu makali kwa sababu mfumo wake ndio huo huo wa Gamondi na Nabi wachezaji waliopo wamejengwa kwenye mfumo huo na wameuelewa na kuuzoea.

3.Sio muwajibikaji na anayekataa makosa yake kwa sababu za uongo.

Baada ya Yanga kutolewa na MC Alger kwenye klabu bingwa kocha wako kiande akaibuka na kuanza kusema ligi ya Tanzania ni dhaifu haina ushindani hivyo tusingeweza kuzifunga timu za Algeria zenye ushindani.

Huu ni zaidi ya uongo na kukwepa uwajibikaji.

Yanga chini ya Gamondi alimfunga CR Belouzdad goli 4 kwa 0 hapa hapa Dar na kutinga robo fainali kibabe sana.

CR Belouzdad ni timu kutoka Algeria.

Simba alimfunga Cs Constantine goli 2 kwa 0 kwa mkapa msimu huo sisi tunatolewa na MC Alger.

Simba alimaliza kinara kwenye kundi lake akiwa na point 13 licha ya Cs Constantine kuwepo na ni timu kutoka Algeria kwenye ushindani.

Mpaka hapo umeshamuona kocha wako ni mtu wa namna gani.
 

Kwenye siasa upo vizuri Ila facts huna nimekuuliza hayo maswali hujajibu hata moja.mimi kwenye porojo nimeshavuka huko lete facts nikijibu Mimi nikikuuliza unajibu Sasa unaleta porojo za kina manqoba tena
 
Huyu yupo kwaajili ya kutetea anayofanya boss wake wake, alipoona boss wake kamtimua Manqoba akaacha kuleta uzi wa kumsifia Manqoba. Saivi boss wake kamleta failure mwingine anajitahidi kutuonesha boss wake kafanya maamuzi sahihi. Utafikiri mpira anaangalia yeye na boss wake pekee.
 
Ndio maana nimemwambia kama sio Hersi mwenyewe basi atakuwa kibaraka wake wa karibu sana.

Yule kocha labda abadili wachezaji lakini kwa aina ya mpira wa Saed na wachezaji waliopo Yanga anatimuliwa mapema tu.
 
Kwenye siasa upo vizuri Ila facts huna nimekuuliza hayo maswali hujajibu hata moja.mimi kwenye porojo nimeshavuka huko lete facts nikijibu Mimi nikikuuliza unajibu Sasa unaleta porojo za kina manqoba tena
Chief mimi ni mtu wa mpira, na ukumbuke ulinifuata hadi PM kwaajili ya kutaka nikupe darasa kuhusu mpira katika angle ya kiufundi kuhisu Manqoba, nikakupa darasa plus maono ya nini kitakachotokea kama Yanga wataendelea na huyo Manqoba mwisho wa siku ulisadiki kwa kinywa chako baada ya mechi ya T.RA. Kuhusu mapungufu ya Saed Ramovic nimeshakupa huko juu na mifano kabisa. Hydroxo pia sasaivi amerudia kukupa ni kwanini tunamkataa huyo kocha aliyeletwa na boss wako.
 

Nimepita sababu zako za kumkataa kocha saed ramovic umesema

Kocha saed ramovic anpenda kupiga pasi nyingi Tena back pass daaaah

Kwa sababu hiyo tu nimejidhihiriahia kuwa mpira unaangalia kwa ushabiki Sana

Hivi Kama anapiga back pass Sana hayo magoli 33 kwenye mechi 13 kafungaje Sasa Kama alikuwa anapiga back pass nyingi mechi 6/6 za ligi kashinda zote . HIYO sabau yako Ni uongo unawadanganya Watu ambao hawajui mpira Kama hao wakina Hydroxo

Wakati saed ramovic alikuwa anakabia juu afanya high pressing kiufundi Ni turn over ndiyo maana alicheza mechi chache na kufunga magolinmengi kuliko makocha wote waliopita yanga
 
Ndio maana nimemwambia kama sio Hersi mwenyewe basi atakuwa kibaraka wake wa karibu sana.

Yule kocha labda abadili wachezaji lakini kwa aina ya mpira wa Saed na wachezaji waliopo Yanga anatimuliwa mapema tu.

Nimekuambia nipe facts tatu zinazokufanya umkatae German machine saed ramovic hujanipa hata moja tatizo lako wewe Ni unafuata mkumbo sana
 
Nimekuambia nipe facts tatu zinazokufanya umkatae German machine saed ramovic hujanipa hata moja tatizo lako wewe Ni unafuata mkumbo sana
Kwamba hujasoma nilichokuwekea au unakurupuka kama kawaida yako?
 
Ndio maana nimemwambia kama sio Hersi mwenyewe basi atakuwa kibaraka wake wa karibu sana.

Yule kocha labda abadili wachezaji lakini kwa aina ya mpira wa Saed na wachezaji waliopo Yanga anatimuliwa mapema tu.

Hizi ndy sababu zako
 
Jamaa aliwahi mtia Pacome Bench kwenye serious match ili Yanga ifuzu.
 
Yule Miloud sujui yupo wapi, Nabi ana defensive game zaidi na kutegemea counters, napenda total football kama ya Gamondi.
 
Saed Ramovic kaiongoza Yanga michezo 6 ya ligi kuu na mmoja wa FA. Vs Namungo, Kagera, Coppo, Dodoma, Mashujaa, prisons na Fountain gate. Je katika hizo timu unaiona timu ipi ilikuwa na ubora kulinganisha na wachezaji wa Yanga?
Katika klabu bingwa mechi ya mwisho ambayo Yanga ilihitaji ushindi wa aina yeyote lakini kashindwa kuifanya Yanga ifuzu kwa kushindwa kuchanga karata ipasavyo. Leo hii ndio mnaona anaweza kuivusha timu mbele ya Zamalek, Mc Alger na Club Africain? Wakati mwenzie Gamond mechi ya nyumbani ya maamuzi alimtandika Belouzdad chuma 4 na Pacome ndiye aliyekuwa ni mmoja ya mkombozi katika mpango wa Gamond ila Saed akamuweka benchi Pacome halafu unataka ushindi. Hajui kupiga hesabu huyo Saed wenu.
 
Moja ya makocha ambao siwakubali japokua tulimfunga al hilal ugenini tukiwa nae ila kwangu mimi bado simukubali wala, kocha sahihi kwangu mimi ni miloud sijajua nini kilitokea mpaka yanga wakaachana nae
 
Hadi sasa mashabiki wa Yanga wanamuona mleta mada kama ms.eng.e vileee. Mtu gani unakataa facts za waziwazi kabisa.

Nimecheka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…