Hapa umefika kwa shabiki LFC.Ramovic ni mzuri kufanya high pressing
Na hii ndo mbinu imempa mafanikio coach Klopp
Binafsi simkubali sana Ramovic ila ni Bora mara 100 zaidi ya FolzHapa umefika kwa shabiki LFC.
Klopp alipata shida Sana mwanzo sababu ya udhaifu huo kujilinda.
Pili, Yanga inao walinzi wenye sifa za mpira wa Saed Ramovic?
Ramovic ndani ya msimu huu akiwa na CR beluzdad mechi 6 points 7 , usidhani hatujui.Ramovic ni mzuri kufanya high pressing
Na hii ndo mbinu imempa mafanikio coach Klopp
Hayo ni mambo ya kawaida hakuna Coach anafanya vyema kila wakati.Ramovic ndani ya msimu huu akiwa na CR beluzdad mechi 6 points 7 , usidhani hatujui.
Ramovic hana tofauti Folz wote hawana uzoefu wa kufundisha timu kubwa na nilijua tu kule Algeria hatatoboa, Miloud Hamad sijui kwanini viongozi walimuacha yule mzee!Viongozi wa Yanga tafadhari sana, tena sana msifanye kosa la kumrudisha Saed Ramovic.
Kumbukeni jinsi Yanga yake ilivyo kuwa shambolic in defense ikifanyiwa counter attacking.
Ilikuwa wapinzani wakifanikiwa kupora mpira na kupiga long balls zinazofika kwa usahihi basi lazima wakamsalimie Diarra au wawatese walinzi wa Yanga.
Ilifika kipindi Diarra akaanza kuonekana goalkeeper mbovu au kashuka kiwango.
Timu ya Ramovic nzuri ikienda mbele kushambulia, Tena dhidi ya timu ndogo dhaifu.
Bora mrudisheni Gamond au tafuteni kocha mwingine mpya.
Akirudi Ramovic sahauni kufanya vizuri mashindano ya kimataifa ya CAF.
Uko sahihi. Yule Ramovich hana tofauti na Romain Folz. Wote ni walewale tu.Yanga wakitaka kujichanganya wamrudishe Ramovic.
Kama makocha wa zamani bora Nabi,Gamondi au Miloud.
Kati ya hao watatu yoyote akirudi sawa lakini sio side mnyamwezi.
Kabisa.Uko sahihi. Yule Ramovich hana tofauti na Romain Folz. Wote ni walewale tu.
Gamond aliacha Yanga ikiwa katika kiwango cha kuridhisha, ule mpira wake ungerudi yamkini tutakuwa mbali sana.Kabisa.
Ile timu yake ilikuwa inashinda kwa hamasa tu za gusa achia twende kwao lakini kimpira timu ilikuwa nyeupe sana.
Mechi ya marudiano na Al Hilal ya Ibenge tulishinda 1 lakini mda wote tunashambuliwa.
Mechi na wale warabu oya oya MC Alger tumeshindwa kupata goli moja tena nyumbani halafu side mnyamwezi akaja na excuse ya kipuuzi eti ligi yetu dhaifu haiwezi kushindana na timu za Algeria.
Kwa kifupi kwa Ramovic mimi binafsi ni big no.
Huyu hakuwa kocha ila mbabaishaji tu. Tena aliondoka kwa kusema ligi ya Tanzania haina ushindani, hivyo hututarajii arudi.Viongozi wa Yanga tafadhari sana, tena sana msifanye kosa la kumrudisha Saed Ramovic.
Kumbukeni jinsi Yanga yake ilivyo kuwa shambolic in defense ikifanyiwa counter attacking.
Ilikuwa wapinzani wakifanikiwa kupora mpira na kupiga long balls zinazofika kwa usahihi basi lazima wakamsalimie Diarra au wawatese walinzi wa Yanga.
Ilifika kipindi Diarra akaanza kuonekana goalkeeper mbovu au kashuka kiwango.
Timu ya Ramovic nzuri ikienda mbele kushambulia, Tena dhidi ya timu ndogo dhaifu.
Bora mrudisheni Gamond au tafuteni kocha mwingine mpya.
Akirudi Ramovic sahauni kufanya vizuri mashindano ya kimataifa ya CAF.
Aheri Gamond arudi, huyu wa Madagascar sina ufaham nae sana kwa level ya club
Mi yatanishinda sio mda nisubiri 90days ban kuwa liftedHa haa haa ๐๐๐
Welcome back Princess.
Bwana Side mnyamwezi siyo kocha mzuri.watu kumbe mpo hewani na hamsemi๐
Binafsi heri Ramovic kuliko Folz.. atleast Ramovic alikua ana gusa achia! Huyu anachezesha timu vibaya jamani nilimuangalia mara 2 ile siku ya simba na Yanga, Simba tu hawakua na utulivu ! Na ile mechi ya kwanza na pamba dk ya 70 >>> bado hamna kitu yani hamna kitu jamani kuhitaji kuwa mchambuzi kujua!
Saed siku ya Al hilal alikua anashambuliwa kwa counter na brilliance ya karumugisha
Sema sasa ndo tutafanyaje ila Hersi kwenye kocha amezingua pakubwa sana! Heri hizo Pressing za Saidi mara 700 mnaweza kuibahatisha timu mkaipiga matatu mkapaki bus japo kwa Yanga ni changamoto sana. Sema kitu kizuri kwenye mpira hakunaga timu imekamilika kila kitu ndo hiko kichaka wanajificha makocha wabovu ukipata watu kama Kina Pacome wakatumia ubora wao mkashinda ukapata kina Job wakasafisha safisha mipira tunanyamaza ila mpira hauna mipango kwa Folz hatufiki popote hio 2nd yenyewe naiogopaBwana Side mnyamwezi siyo kocha mzuri.
Hizo counter attacks unazosema tutapigwa sana huko CAF Champions League au na Azam FC hapa nyumbani.
High line pressing inahitaji backline yenye defender warefu, wenye kasi na ubavu kama akina Virgil Van Djik.
Hawa ndugu zetu akina Dickson Job hawana mbio na msuli wanategemea akili pekee.
Bacca naye anajaribu nguvu lakini hawezi kuwekeana ubavu na striker lenye 75kg na kuendelea lenye kasi.
Au hawezi kupambana na winger mwenye kasi na chenga kama akina Giramugisha uliemtaja.
Kutegemea geggen pressing ya Ramovic au Klopp lazima uwe na washambuliaji wenye convertion rate kubwa ya goal chances, wasiopoteza mipira kirahisi.
Siyo akina Prince Dube wanapoteza mpira, mnafanyiwa transition ya haraka mnafungwa kwa counter attack. Kisha watu wanapaki bus.
Imeisha hiyo out of tournament!
Mzinze anajua kuulinda na ku dribble mpira lakini convertion rate yake mbele ya goal ni ndogo.
Wangekuwa wana convert vizuri zile goal chances mnashindana idadi ya magoli tu. Kama Liverpool ya Klopp ya 2018 -2019 hasa mechi UEFA CL dhidi ya Man City 2018 au mechi na As Roma.
Umeona Liverpool alivyopigwa final na Real Madrid huo msimu? Ndivyo tunavyopigwa CAF CL au CAF Confederation Cup tunaopenda kushambulia tukapoteza mpira.