Safari hii Law School wafaulu 23 tu!

Safari hii Law School wafaulu 23 tu!

View attachment 2599573

Kati ya wanafunzi waliohitimu Shahada ya Juu ya Elimu ya Sheria kwa Vitendo kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) waliofaulu (first sitting) ni 23, ambapo wanaopaswa kurudia baadhi wa mitihani (Sup) ni 497 na wanaopaswa kurudia mafunzo hayo (Disco) ni 301!

Tofauti ya ufaulu wa mwaka jana na mwaka huu kwa walioweza kupita kwa mara ya kwanza ni moja tu, ambapo mwaka jana walifaulu 22!

Eatv

Hali ilivyokuwa mwaka jana - Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!

Yaani mtu ka-graduate university (chuo kikuu) halafu anakuja kufeli (at school) shuleni ??🤣🤣
 
View attachment 2599573

Kati ya wanafunzi waliohitimu Shahada ya Juu ya Elimu ya Sheria kwa Vitendo kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) waliofaulu (first sitting) ni 23, ambapo wanaopaswa kurudia baadhi wa mitihani (Sup) ni 497 na wanaopaswa kurudia mafunzo hayo (Disco) ni 301!

Tofauti ya ufaulu wa mwaka jana na mwaka huu kwa walioweza kupita kwa mara ya kwanza ni moja tu, ambapo mwaka jana walifaulu 22!

Eatv

Hali ilivyokuwa mwaka jana - Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!

Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe:

Wanafunzi Law School kulikoni kushindwa kujisimamia
 
Wamejitahidi sana aisee. Mwaka 2021 law school ya Zambia ilifaulisha mwanafunzi mmoja kati ya 495 waliofanya mtihani.
 
View attachment 2599573

Kati ya wanafunzi waliohitimu Shahada ya Juu ya Elimu ya Sheria kwa Vitendo kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) waliofaulu (first sitting) ni 23, ambapo wanaopaswa kurudia baadhi wa mitihani (Sup) ni 497 na wanaopaswa kurudia mafunzo hayo (Disco) ni 301!

Tofauti ya ufaulu wa mwaka jana na mwaka huu kwa walioweza kupita kwa mara ya kwanza ni moja tu, ambapo mwaka jana walifaulu 22!

Eatv

Hali ilivyokuwa mwaka jana - Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!
SHULE BORA KABISA HATUTAKI UJANJA UJANJA WA VYUONI
UTULETEE MAWAKILI FAKE
 
Mwaka jana 2022 - wafaulu 22
Mwaka huu 2023 - wafaulu 23
Mwakani 2024 - wafaulu ....
 
Ila sikuhizi wanafunzi nao wazito mno niliamgalia jinsi mwanasheria lugha yake aliyotumia na kuandaa mashtaka nilichoka, kingereza kibovu mashtaka hayaeleweki na hapo kaajiriwa na serikalini nikasema ndio maana law school Huwa wanafeli Hawa Kwa ukilaza wao
Tatizo sio wanafunzi. Kama ni mzito hakustahili kupokewa na kuruhusiwa kufanya mtihani. Inaelekea wanafunzi ni mtaji wa hiyo shule hivyo wanapokewa wengi iwezekanavyo bila kuangalia uwezo wao. Kama hawajui kiingereza wamewezaje kupasi masomo ya Law School mpaka wafikie hatua ya kufanya mtihani? Tatizo liko Law School na si kwengine. Na unaweza kukuta wanaona sifa wanafunzi wengi wanapofeli badala ya kuona aibu kuwa hawajawatayarisha vizuri.

Amandla...
 
Tatizo jingine elimu ya sasa imekuwa ya mwendokasi toka shule ya msingi, na hii ni kutokana na serikali kuitelekeza elimu ya umma na kuacha elimu bora itolewe na shule binafsi. Watoto wa wanyonge ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia private wanajikuta wameangukia kwenye shule za serikali ambako elimu kwa sasa inatolewa kwa kiwango duni kulinganisha na awamu za mwanzoni, enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa na hata Kikwete. Awamu ya tano na ya sita imekuja kuizika elimu ya umma......kwa hiyo matokeo ya law school yana reflect ubora duni wa elimu tokea huku chini kwenye elimu ya msingi na sekondari, THINK BIG!!​
 
practical kwa kawaida mtu hapaswi kufeli!! Tatizo law school hawafanyi practical japo ilipaswa kuwa practical! Wanapigwa mitihani ya theory as if wako chuoni wakiiga digrii!! Huu ni uharibifu mkubwa!
 
practical kwa kawaida mtu hapaswi kufeli!! Tatizo law school hawafanyi practical japo ilipaswa kuwa practical! Wanapigwa mitihani ya theory as if wako chuoni wakiiga digrii!! Huu ni uharibifu mkubwa!
Utamudu vipi practical bila kujua theory?

Amandla...
 
Kwa hiyo kiingereza ni shida siyo eeee?!!!!

Sorry for them[emoji120]

My take:

Wadogo zetu mnaosoma sheria na ambao mko mwaka wa 1 hebu jitahidini haya ninayowaambia:-

LEGAL MAXIMS....

Huwezi kuwa "lawyer" mzuri bila kujua KIINGEREZA...hususani JAGGONS....tafuteni DICTIONARY ya "legal maxims"....nyingi ziko kwa kilatini ila kwa ninyi ni bora mkazipata zenye "English translations".....waambieni na wenzenu hili.....BUMU la BOOKS & STATIONERY japo dogo ila mnapata bwanaa... jisukumeni na jiongezeni hivyohivyo.....WAAMBIENI NA WENZENU WASIOKUWA HAPA[emoji1666]

Unasomaje LEGAL MAXIMS?!!!

Enheeee hivi mmeshawahi kuwaona wale watoto wa shule ya elimu ya dini ya kiislam?!!!

MADRASA MADRASA MADRASA

Hapa nisikilizeni....hawa watoto huwa wanarudiarudia kukariri maneno ya kiarabu....unaweza ukaona kama mfumo wa ajabu ili UBONGO unase vitu ni lazima UVIRUDIERUDIE ukiuhusisha wenyewe ,moyo wako(tranquility) na midomo......waigeni hawa watoto na muwe kama machizi vile [emoji1787][emoji1787]

Mathalani kwa mnaosoma chuo kikuu Mlimani unaweza kuweka ratiba na kutembea kutoka hapo hosteli zenu mpaka kimara ukiweka ratiba ya kurudia JAGGONS 5 na maana zake kwa wiki mara 3 hiviii....mkijizoeza hivi kwa miaka 4 mtatisha kama njaa....yaani mtakuwa kama wale vijana wa "CAMBRIDGE & HARVARD SCHOOL OF LAWS".

Kusoma masomo haya haihitajiki utani,ublazameni &usisteri uliopitiliza bali inahitaji uusukume "ukuta na uuangushe"[emoji1787]

1)Medicine
2)Law
3) Engineering

Allah Yehova Yahweh awatangulie ,aaamin aaamin[emoji120]

#YetzerHatov
#DoNotDoHarm

#SiempreJMT[emoji7]
#MamaHuyooooKaja[emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Now medicine na engineer imekua soft na Kuna wahitimu vilaza kibao
 
View attachment 2599573

Kati ya wanafunzi waliohitimu Shahada ya Juu ya Elimu ya Sheria kwa Vitendo kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) waliofaulu (first sitting) ni 23, ambapo wanaopaswa kurudia baadhi wa mitihani (Sup) ni 497 na wanaopaswa kurudia mafunzo hayo (Disco) ni 301!

Tofauti ya ufaulu wa mwaka jana na mwaka huu kwa walioweza kupita kwa mara ya kwanza ni moja tu, ambapo mwaka jana walifaulu 22!

Eatv

Hali ilivyokuwa mwaka jana - Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!
Hao 23 wengi watakua wanatoka SAUT mwanza na TUDARCO Kwa mbali UDSM na Mzumbe.......

Alisikika advocate mmoja from High Court
🤓🤓🤓🤓

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Back
Top Bottom