kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hakuna siku wanaume wamekaa na kuamua kuwakataza wanawake wasiwe viongozi, kwenda shule, wasifyatue matofali, wasiangue madafu kwenye minazi, kuendesha bodaboda, kufanya biashara Wala kuwinda.
Tangu enzi hizo za kale kulikuweko na wanawake wanaopambana na biashara huko tabora, queen of Sheba huko Ethiopia, Cleopatra huko Misri, nk.
Mama yangu tangu enzi hizo alilima kahawa kuuza na kusomesha wanawe wote mwenyewe bila kuhamasishwa na mtu Wala chombo chochote. Alikuwa na haki zake zote. Akina mama Ana Abdalah, bibi titi, Mama Mongela, Bi Kidude, nk hawakuhitaji mkakati wa kuwainua ili wawe vile walivyo.
Hizi jitihada za Sasa ni kuzidi kuwadhoofisha wanawake badala ya kuwaimarisha na upigaji wa pesa kupitia wanawake. Ni jitihada za kufanya mwanamke azidi kuwa delicate kupindukia.
Kama unataka kuipua mwanamke mwenye nguvu na imara kifikra mwache mwanamke ajitokeze mwenyewe kwenye uongozi, biashara, kazi mbalimbali na kwenye elimu.
Ukomnozi wa mwanamke uko kwa mwanamke mwenyewe. Hizi harakati za kumwinua mwanamke haziwezi kufua dafu kama ujasiri hautaanzia kwenye mioyo Yao.
Watoto wangu wa kike ni imara kuliko wale wa kiume kwakuwa sikuwa na upendeleo wa aina yoyote kwao. Sio eti kwakuwa huyu ni mwanamke ni mpe mahitaji zaidi ya kaka yake. Niliacha kila mtoto ajitambue mahitaji yake ili apange matumizi yake kulingana na mahitaji yake.
Mwanaume atumie akijua Kuna kwenda salon kunyoa na mwanamke atumie akijua kuwa Kuna mapedi, kwenda salon kuweka dawa au kunyoa na wote lazima wamalize homeworks zao kwa mazingira Yao.
Hii ya Sasa ya malkia wa nguvu, super woman, nk ni udhalilishaji wa wanawake na upigaji pesa TU.