wazunguwawili
JF-Expert Member
- May 29, 2019
- 3,984
- 4,132
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Kazi iendelee.
Ilikuwa ni furaha kutoka Nyanda za Juu Kusini na kuja Ukanda huu wa Kaskazini mwa Tanzania.
Jiji maarufu kabisa kwa harakati za utalii.
Yafuatayo ndiyo niliyoyaona na mengine yamenishangaza.
1. Covid 19 imeutesa sana huu mji. Mishe zilizotegemea utalii zilikumbwa na pigo kama lile la afande moroto. Ingawa hali kama inarejea.
2. Ulaji nyama na unywaji wa pombe hufanyika kwa kiasi kikubwa mnoo. Si dhani kama kuna mkoa unawazidi hawa jamaa.
3. Utii wa sheria kwa watumiaji wa vyombo vya moto ni kama haiwahusu. Madereva wapo rafu mnoo. Watu pekee wanaojitahidi ni toyo/boda ingawa ni wapo wahuni wachache.
Uendeshaji magari ni tatizo katika hili jiji. Trafiki inabidi wafanye kazi ikiwa ni pamoja na kuchora upya namna ya matumizi ya barabara.
4. Watembea kwa miguu hawa ndiyo viburi waliopitiliza. Wanajiona nao ni kama magari/pikipiki.
5. Tabia za kibepari ni nyingi mno kuliko ujamaa. Wepesi pia kupeana michongo, wanaamini nao wanaweza tokea humo.
6. Bei za milupo nadhani bado bei elekezi inafanya kazi. Ila ukiwa mgeni unaweza pewa bill kubwa. Kuwa makini, wengine bado ni wezi hawaheshimu kazi zao.
7. Changamoto katika meno ya hawa watu ni shida. Demu mkali unakuta meno yameharibika, rangi zilizopitiliza. Sijajua chanzo hasa ni nini, je ni maji wanayotumia ama ulaji nyama uliopitiliza?
Iweje mamlaka ya maji safi wanashindwa kulitatua hili,wala madaktari wetu pia wameshindwa.
Hata kama linawapa identity bado ni mbaya pale inapodhidi,ingawa inaleta urembo kwa wengine.
8. Jamaa ni waoga sana wa baridi.
Asanteni Ara Chuga, masela wa Njiro, Moshono, Chekeleni, Ngaramtoni, Unga Limited, Sakina, Morombo, Ngarenaro, Makao Mapya hata wale nilio wasahau.
Vijiwe vyenu nilivyopita ni The Don, Mopao, Kokoriko, Uzunguni, Bills River, Picnic, Empire, Annex, Redwood.
Hakika zimekuwa siku 8 za purukushani nyingi na muda mchache wa kulala.
Fantastic stay in your city.
Karibuni pia kwa wanalizombe.