JBourne59
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 946
- 8,640
Uandae na MNG'ANG'ASiku ukipita Sitalike- Majimoto( maji ya moto) zamani waliita hivyo, uniambie nikuagizie kitu kinaitwa (MADIMU) ila angalizo mmm
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uandae na MNG'ANG'ASiku ukipita Sitalike- Majimoto( maji ya moto) zamani waliita hivyo, uniambie nikuagizie kitu kinaitwa (MADIMU) ila angalizo mmm
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeipenda sana hiyo trip,sema kumbe ist ni gari ya kazi kihivyo? Napenda sana hiyo style will try one dayHabari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.
Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.
Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.
Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.
Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.
Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.
Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.
Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.
Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....
Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.
Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.
Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.
Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.
Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.
View attachment 2050099
View attachment 2050102
View attachment 2050103
View attachment 2050106
View attachment 2050107
View attachment 2050109
View attachment 2050110
View attachment 2050112
View attachment 2050113
View attachment 2050114
View attachment 2050115
View attachment 2050116
View attachment 2050118
View attachment 2050121
MNG'ANG'A ndiyo nini jamani msamiati huu kwangu tafadhali![emoji23]Uandae na MNG'ANG'A
Kweli kabisa huko Kibondo warundi wamepiga kambi. Hivi vibao vya spidi 50 vinachosha sana na sipendi kubembeleza traffic wana tabia za kike sana. Unaomba weeh kama unatongoza na atakaa hapo anakuskiliza lakini bado anakupiga fine.Kwa kuwa ni utalii nadhani hamna haja ya kusafiri usiku
Lakini kuna njia usalama mdogo kwa mfano kasulu - kibondo kuanzia saa 2 usiku inakuwa ni hatari
Pistol v/s AK-47!???Ukiwa na 4x4 na silaha usiku ni muda mzuri kusafiri. Hamna traffic wala magari mengi unatumia muda mfupi kufika eneo husika.
Waulize watu wa KakonkoUsiku Wala hakuna hatari yoyote, hakikisha tu huna uchovu, gari Ina taa zenye mwanga wa kutosha na acha ku-overtake kijinga
Amejibu post no. 102Bajeti ya ziara nzima ilifikia sh. ngapi?
Watu wengi hawapendi adventures,kwa sisi tunaopenda adventures huwezi Kuta ligi ya kushindanisha miji nk tukakosekana.Kwanza hongera kwa safari ya kuona ukubwa wa nchi.
Watanzania wengi kutembea wanaona kama wanapoteza hela. Ndio maana maswali Yao niende Serengeti kufanya nini? Kumwona Simba tu? Ananisaidia nini?
Wapo wengi watanzania hawaijui nchi hii. Anafika sehemu kwa sababu ametumwa kikazi. Yeye mwenyewe hawezi kufanya adventure.
Mimi likizo yangu Septemba na octoba nilitembea Peke yangu kwa xtrail. Nilizunguka robo kipande Cha Tanzania. Nilivyosoma andiko lako ni kama nilikuwa najiona vile. Kasoro uliamua kuacha njia ya Mbeya, Sumbawanga, Katavi hadi Kigoma. Ungepita ungejua nchi hii ni kubwa sana.
Nimezunguka njia hiyo. Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Runzewe- Bwanga-Katoro-Geita-Mwanza. Mwanza - Geita- Katoro- Runzewe- Nyakanazi- Kakonko- Kibondo- Kasulu- Kigoma- Mpanda-Sitalika nikapitia mbugani- Namanyere- Sumbawanga- Tunduma-Mbeya - Ubaruku-Makambako-Njombe-Songea. Songea-Njombe-Iringa-Moro-Dar. Dar-Dodoma- Manyoni-Itigi - Tabora- Kaliua-Uvinza-Kigoma. Mwaka huu nimezunguka kwa private hadi raha halafu Peke yangu. Lakini nilichoka sana.
Nawahamasisha wengine kufanya route za kujionea nchi. Nahitaji kuifanya route ya Musoma to Arusha nikipumzika Serengeti panapo majaliwa
Ulitumia siku ngapi jumla ya kilom eter,bajeti ya mafuta tu ilikuwa sh ngapi lavda kesho ntaokota hela na mimi niingie roadHahahaa sikua na haraka Iko poa kabisa labda brake pads tu
Mzee huwa napenda sana stori zako,hasa kwenye ule uzi pendwa wa MMU,ubarikiwe sana,umenikosha sana pale stalike,majimoto adi mlowo,hakika we ni noma saaaanaHongera kutalii.
Siku nyingine jaribu route hizi
1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Mbamba bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.
2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.
Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.
Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
Kuna adventure route nitaipendekeza very soon, usikose.Mzee huwa napenda sana stori zako,hasa kwenye ule uzi pendwa wa MMU,ubarikiwe sana,umenikosha sana pale stalike,majimoto adi mlowo,hakika we ni noma saaaana
Alafu mtu mmoja aizungumzie ist vbayaNiliwaza kutumia Nissan Xtrail nikahofia kama nikipata breakdown, zile gari ni umeme 100% na mafundi wetu wa mkoani hawa
Simple sana yani lakini inatoa shule kubwa ukiwa barabaraniShukrani sana, nilitumia takribani siku kumi, sio za kusafiri. Nazungumzia safari nzima, Kuna sehemu nilikua napumzika kidogo na kuonana na wadau.
Mafuta Nina baadhi ya risiti haifiki 700,000....kwa Mafuta.
Njiani nilikua nakula matunda zaidi Ili kubalance tumbo, ndizi, maepo (apples) [emoji519][emoji520] za Makete, Karanga etc . Gharama halisi Sina ila haikuzidi 1.2m.
Mkuu umetisha sana40 Days 2022/2023 adventure around Tanzania main land.
1. Gari ipo, Land Rover Defender 110 / 2021 Station Wagon.
2. Wanao hitajika ni wadau watano (5), wanawake watatu (3) na wanaume wawili (2) na mimi mwenyewe jumla tuwe watu sita (6).
3. Wakijitokeza watu wengi zaidi utaratibu wa kupata (ma)gari (me)ngine utafanyika.
4. Tutatembea zaidi ya kilomita 6,000 kwa siku 32, siku 8 zitapotelea katikati kadri tutakavyo amua.
5. Makadirio ya gharama ya mafuta ni 1.8M hadi 2m.
6. Mchango kwa kila mdau itahitajika 1.5m ambayo itagharamia mafuta, chakula, malazi na utalii.
7. Mchango haukusanywi bali kila mmoja ajiwekee akiba benki au popote pale kuanzia sasa hadi mwezi October 2022 panapo majaaliwa ambapo tutafanya kikao na kupanga safari yetu, lengo liwe hadi kufikia 5 Disemba 2022 tuwe tumemaliza mzunguko wetu.
Mawazo chanya, yanakaribishwa, kuhusu Route, gharama, usahihi wa umbali, usalama, nk.
8. Mapendekezo yangu ya route iwe ni kuzunguka pembezoni mwa Tanzania kama ifuatavyo:-
Day 1
Dar - Lindi - Mtwara, almost 600km.
Day 2
Mtwara - Masasi - Mtambaswala, almost 320km.
Day 3
Mtambaswala - Masasi - Songea, almost 500km.
Day 4
Songea - Mbinga - Mbamba bay, almost 180km.
Day 5
Mbamba bay - Songea - Njombe, almost 420km.
Day 6
Njombe - Makete (via Kitulo) - Mbeya, almost 170km.
Day 7
Mbeya - Kasumulu, almost 120km.
Day 8
Kasumulu - Mbeya Tunduma, almost 230km
Day 9
Tunduma - Sumbawanga - Kasanga, almost 350km
Day 10
Kasanga - Sumbawanga - Muze - Lake Rukwa, almost 180k.
Day 11
Lake Rukwa - Muze - Namanyele - Kibaoni - Majimoto, almost 180km.
Day 12
Majimoto - Kibaoni - Stalike - Mpanda, almost 150km
Day 13
Mpanda - Uvinza - Kigoma town, almost 320km.
Day 14
Kigoma - Kasulu - Nyakanazi, almost 350km
Day 15
Nyakanazi - Lusahunga - Nyakahura - Kobero border, almost 150km.
Day 16
Kobero border - Nyamiyaga - Rusumo border, almost 70km.
Day 17
Rusuma - Nyakasanza - Mtukula, almost 250km.
Day 18
Mtukula - Bukoba town, almost 90km.
Day 19
Bukoba - Biharamuro - Geita - Mwanza, almost 450km.
Day 20
Mwanza - Bunda - Musoma - Migori, almost 300km.
Day 21, 22, 23, 24
Migori - Tarime - Serengeti, almost 200km + other 200km.
Day 25, 26
Serengeti - Ngorongoro, almost 70km + 200km.
Day 27, 28
Ngorongoro - Karatu - Arusha, almost 200km.
Day 29
Arusha - Segera - Tanga - Horohoro, almost 550km
Day 30
Horohoro - Tanga town, almost 70km + 50km.
Day 31
Tanga - Pangani - Sadani, almost 200km.
Day 32
Sadani - Bagamoyo - Dar es Salaam, almost 180k.
Karibuni kwa mawazo chanya kwenye uzi wa link hii.
40 days 2022/2023 road trip adventure around Tanzania
___________
JBourne59
Haiku00 at£Bajeti ya ziara nzima ilifikia sh. ngapi?
Karibu sanaPicha nyingi hapo nimeona za Kigoma! Hongera kwa utalii mkuu! Niliona daraja la mto Malagarasi kwa barabara ya Kasulu - Kibondo nikatamani kurudi Kasulu!