Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Acheni woga. Mwanaume awe tayari muda wote for Roses and gunsWazee wa kazi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acheni woga. Mwanaume awe tayari muda wote for Roses and gunsWazee wa kazi
Asante sana [emoji23][emoji23]Karibu Kiteto, Kongwa, Ilala, Ngorongoro, Ileje, Ikungi, Masasi na Korogwe, Kikwajuni na Nairobi
Siku ukipita Sitalike- Majimoto( maji ya moto) zamani waliita hivyo, uniambie nikuagizie kitu kinaitwa (MADIMU) ila angalizo mmmHongera kutalii.
Siku nyingine jaribu route hizi
1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Mbamba bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.
2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.
Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.
Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
Nilitegemea hili jibu toka kwa vijana wa chadema [emoji23][emoji23].Sasa hii inahusiana vipi na safari yako? hapa ndio umeharibu
Ukisikia gari inatumia umeme 100% ujue haitumii mafuta, mfano Kenya wanazo 50% umeme, yaani inaanza na umeme kisha inaendelea na mafuta, gari zinazotengenezwa siku hizi ni 100% umeme, unaanza na umeme na utamaliza kwa umeme haina injini ya mafuta japo unaichaji fasta kwenye kituo cha mafuta, hizo ndiyo gari za umeme na wanachaji kwa kutumia umeme wa Tanesco.Hahahaahahah ulivyosikia umeme ukajua Tanesco.....haya
Hebu soma Tena nilichoandikaUkisikia gari inatumia umeme 100% ujue haitumii mafuta, mfano Kenya wanazo 50% umeme, yaani inaanza na umeme kisha inaendelea na mafuta, gari zinazotengenezwa siku hizi ni 100% umeme, unaanza na umeme na utamaliza kwa umeme haina injini ya mafuta japo unaichaji fasta kwenye kituo cha mafuta, hizo ndiyo gari za umeme na wanachaji kwa kutumia umeme wa Tanesco.
Tunaishi mara moja Kaka. Karibu sanaDaaaa bwana PGO ulichofanya ni Zaidi ya yaliyo katika PGO
(People General Order)
ya kitaa yaani umeupiga mrefu sana mpaka umepitiliza
Jambo ambalo wengi linawashinda,
Hongera mkuu wangu!
You are
Inspiration!
OhoooNilitegemea hili jibu toka kwa vijana wa chadema [emoji23][emoji23].
For Roses and GunsAcheni woga. Mwanaume awe tayari muda wote for Roses and guns
Kwanza hongera kwa safari ya kuona ukubwa wa nchi.Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.
Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.
Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.
Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.
Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.
Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.
Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.
Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.
Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....
Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.
Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.
Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.
Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.
Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.
View attachment 2050099
View attachment 2050102
View attachment 2050103
View attachment 2050106
View attachment 2050107
View attachment 2050109
View attachment 2050110
View attachment 2050112
View attachment 2050113
View attachment 2050114
View attachment 2050115
View attachment 2050116
View attachment 2050118
View attachment 2050121
Tuombe Mungu next timeKwa hiyo mwanangu ulipita hadi Runzewe!!!??dah ungenistua tule monde
Aina noma kamandaTuombe Mungu next time
Shukrani sanaUkipita tena manyoni nishtue nije nikupe kampani ya kula vyuku