Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Hongera kutalii.

Siku nyingine jaribu route hizi

1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Mbamba bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.

2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.

Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.

Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
Siku ukipita Sitalike- Majimoto( maji ya moto) zamani waliita hivyo, uniambie nikuagizie kitu kinaitwa (MADIMU) ila angalizo mmm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaahahah ulivyosikia umeme ukajua Tanesco.....haya
Ukisikia gari inatumia umeme 100% ujue haitumii mafuta, mfano Kenya wanazo 50% umeme, yaani inaanza na umeme kisha inaendelea na mafuta, gari zinazotengenezwa siku hizi ni 100% umeme, unaanza na umeme na utamaliza kwa umeme haina injini ya mafuta japo unaichaji fasta kwenye kituo cha mafuta, hizo ndiyo gari za umeme na wanachaji kwa kutumia umeme wa Tanesco.
 
Daaaa bwana PGO ulichofanya ni Zaidi ya yaliyo katika PGO
(People General Order)
ya kitaa yaani umeupiga mrefu sana mpaka umepitiliza
Jambo ambalo wengi linawashinda,
Hongera mkuu wangu!
You are
Inspiration!
 
Ukisikia gari inatumia umeme 100% ujue haitumii mafuta, mfano Kenya wanazo 50% umeme, yaani inaanza na umeme kisha inaendelea na mafuta, gari zinazotengenezwa siku hizi ni 100% umeme, unaanza na umeme na utamaliza kwa umeme haina injini ya mafuta japo unaichaji fasta kwenye kituo cha mafuta, hizo ndiyo gari za umeme na wanachaji kwa kutumia umeme wa Tanesco.
Hebu soma Tena nilichoandika
 
Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.

Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.

Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.

Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.

Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.

Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.

Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.

Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.

Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....

Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.

Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.

Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.

Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.

Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.

View attachment 2050099

View attachment 2050102

View attachment 2050103

View attachment 2050106

View attachment 2050107

View attachment 2050109

View attachment 2050110

View attachment 2050112

View attachment 2050113

View attachment 2050114

View attachment 2050115

View attachment 2050116

View attachment 2050118

View attachment 2050121
Kwanza hongera kwa safari ya kuona ukubwa wa nchi.

Watanzania wengi kutembea wanaona kama wanapoteza hela. Ndio maana maswali Yao niende Serengeti kufanya nini? Kumwona Simba tu? Ananisaidia nini?

Wapo wengi watanzania hawaijui nchi hii. Anafika sehemu kwa sababu ametumwa kikazi. Yeye mwenyewe hawezi kufanya adventure.

Mimi likizo yangu Septemba na octoba nilitembea Peke yangu kwa xtrail. Nilizunguka robo kipande Cha Tanzania. Nilivyosoma andiko lako ni kama nilikuwa najiona vile. Kasoro uliamua kuacha njia ya Mbeya, Sumbawanga, Katavi hadi Kigoma. Ungepita ungejua nchi hii ni kubwa sana.

Nimezunguka njia hiyo. Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Runzewe- Bwanga-Katoro-Geita-Mwanza. Mwanza - Geita- Katoro- Runzewe- Nyakanazi- Kakonko- Kibondo- Kasulu- Kigoma- Mpanda-Sitalika nikapitia mbugani- Namanyere- Sumbawanga- Tunduma-Mbeya - Ubaruku-Makambako-Njombe-Songea. Songea-Njombe-Iringa-Moro-Dar. Dar-Dodoma- Manyoni-Itigi - Tabora- Kaliua-Uvinza-Kigoma. Mwaka huu nimezunguka kwa private hadi raha halafu Peke yangu. Lakini nilichoka sana.

Nawahamasisha wengine kufanya route za kujionea nchi. Nahitaji kuifanya route ya Musoma to Arusha nikipumzika Serengeti panapo majaliwa
 
Back
Top Bottom