Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Nimeipenda sana hiyo trip,sema kumbe ist ni gari ya kazi kihivyo? Napenda sana hiyo style will try one day

umeimaliza mikoa mingi sana.
 
Kwa kuwa ni utalii nadhani hamna haja ya kusafiri usiku

Lakini kuna njia usalama mdogo kwa mfano kasulu - kibondo kuanzia saa 2 usiku inakuwa ni hatari
Kweli kabisa huko Kibondo warundi wamepiga kambi. Hivi vibao vya spidi 50 vinachosha sana na sipendi kubembeleza traffic wana tabia za kike sana. Unaomba weeh kama unatongoza na atakaa hapo anakuskiliza lakini bado anakupiga fine.
 
Watu wengi hawapendi adventures,kwa sisi tunaopenda adventures huwezi Kuta ligi ya kushindanisha miji nk tukakosekana.
 
Je kuna part itayakayoonekana kwenye sredi ya Rikiboy?

Au hukuonja kabisa njia nzima?
 
Safari ndefu kama hizo inatakiwa pia uwe na hela ya kutosha,ili pale unapopumzika angalau ule,unywe na kulala vizuri...
 
Mzee huwa napenda sana stori zako,hasa kwenye ule uzi pendwa wa MMU,ubarikiwe sana,umenikosha sana pale stalike,majimoto adi mlowo,hakika we ni noma saaaana
 
Simple sana yani lakini inatoa shule kubwa ukiwa barabarani

Mimi hua natoka na Starlet Karatu ambako ni kazini kwenda Mwanza ambako ni nyumbani kwangu, nenda rudi ya kila mwezi au baada ya miezi miwili,kiukweli usafiri binafsi unakupa uhuru na kutalii vyema sana,pia unakupa marafiki huko kwenye vituo unavyo amua kusimama kwa malazi au chakula,au kujifunza mambo kadhaa

Mimi nililima shamba Singida kwa kupewa ramani na mdada tu aliyeniuzia wali kuku kwenye mgahawa humo barabarani

Watu wanaweza kudhani ni anasa lakini ni sehemu ya kupanua mawazo kichwani
 
40 Days 2022/2023 adventure around Tanzania main land.

1. Gari ipo, Land Rover Defender 110 / 2021 Station Wagon.

2. Wanao hitajika ni wadau watano (5), wanawake watatu (3) na wanaume wawili (2) na mimi mwenyewe jumla tuwe watu sita (6).

3. Wakijitokeza watu wengi zaidi utaratibu wa kupata (ma)gari (me)ngine utafanyika.

4. Tutatembea zaidi ya kilomita 6,000 kwa siku 32, siku 8 zitapotelea katikati kadri tutakavyo amua.

5. Makadirio ya gharama ya mafuta ni 1.8M hadi 2m.

6. Mchango kwa kila mdau itahitajika 1.5m ambayo itagharamia mafuta, chakula, malazi na utalii.

7. Mchango haukusanywi bali kila mmoja ajiwekee akiba benki au popote pale kuanzia sasa hadi mwezi October 2022 panapo majaaliwa ambapo tutafanya kikao na kupanga safari yetu, lengo liwe hadi kufikia 5 Disemba 2022 tuwe tumemaliza mzunguko wetu.

Mawazo chanya, yanakaribishwa, kuhusu Route, gharama, usahihi wa umbali, usalama, nk.

8. Mapendekezo yangu ya route iwe ni kuzunguka pembezoni mwa Tanzania kama ifuatavyo:-

Day 1
Dar - Lindi - Mtwara, almost 600km.

Day 2
Mtwara - Masasi - Mtambaswala, almost 320km.

Day 3
Mtambaswala - Masasi - Songea, almost 500km.

Day 4
Songea - Mbinga - Mbamba bay, almost 180km.

Day 5
Mbamba bay - Songea - Njombe, almost 420km.

Day 6
Njombe - Makete (via Kitulo) - Mbeya, almost 170km.

Day 7
Mbeya - Kasumulu, almost 120km.

Day 8
Kasumulu - Mbeya Tunduma, almost 230km

Day 9
Tunduma - Sumbawanga - Kasanga, almost 350km

Day 10
Kasanga - Sumbawanga - Muze - Lake Rukwa, almost 180k.

Day 11
Lake Rukwa - Muze - Namanyele - Kibaoni - Majimoto, almost 180km.

Day 12
Majimoto - Kibaoni - Stalike - Mpanda, almost 150km

Day 13
Mpanda - Uvinza - Kigoma town, almost 320km.

Day 14
Kigoma - Kasulu - Nyakanazi, almost 350km

Day 15
Nyakanazi - Lusahunga - Nyakahura - Kobero border, almost 150km.

Day 16
Kobero border - Nyamiyaga - Rusumo border, almost 70km.

Day 17
Rusuma - Nyakasanza - Mtukula, almost 250km.

Day 18
Mtukula - Bukoba town, almost 90km.

Day 19
Bukoba - Biharamuro - Geita - Mwanza, almost 450km.

Day 20
Mwanza - Bunda - Musoma - Migori, almost 300km.

Day 21, 22, 23, 24
Migori - Tarime - Serengeti, almost 200km + other 200km.

Day 25, 26
Serengeti - Ngorongoro, almost 70km + 200km.

Day 27, 28
Ngorongoro - Karatu - Arusha, almost 200km.

Day 29
Arusha - Segera - Tanga - Horohoro, almost 550km

Day 30
Horohoro - Tanga town, almost 70km + 50km.

Day 31
Tanga - Pangani - Sadani, almost 200km.

Day 32
Sadani - Bagamoyo - Dar es Salaam, almost 180k.

Karibuni kwa mawazo chanya kwenye uzi wa link hii.
40 days 2022/2023 road trip adventure around Tanzania



___________
JBourne59
 
Mkuu umetisha sana

Nakuja na maoni muda si mrefu
 
Picha nyingi hapo nimeona za Kigoma! Hongera kwa utalii mkuu! Niliona daraja la mto Malagarasi kwa barabara ya Kasulu - Kibondo nikatamani kurudi Kasulu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…