Safari yangu ya Elimu ilivyokuwa ngumu na kupata Zero mara tatu katika mtihani wa Kidato cha Nne

Safari yangu ya Elimu ilivyokuwa ngumu na kupata Zero mara tatu katika mtihani wa Kidato cha Nne

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Safari yangu ya Elimu ya Secondary niliianza Mwaka 2011 katika Shule moja Maarufu pale Bukoba Mjini ikiitwa Lake View hakika Maisha ya pale yalikuwa mazuri tulisoma na wahindi huku shule hipo beach yaani kila kitu nilikuwa Safi, hasa ukizingatia nilisoma shule za kawaida katika Elimu ya msingi.

Baada ya kusoma na kufika kidato cha Tatu kuelekea cha nne nilikwama Ada na hivyo kushindwa kuendelea na Masomo hakika Jambo hili lilini-affect kiakili sana.

Basi baada ya kukaa Nyumbani muda Mrefu niliwaza kusoma QT na hapo nyota yangu ya kupata Division Zero ndipo ilipoanza kuwaka.

Hivyo mwaka 2014 nikafanikiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kama mtahiniwa wa Kujitegemea na hapo Ndipo napata zero yangu ya 35 kwa mara ya kwanza.

Baada ya Kupata zero ya kwanza nikapata Ushauri kuwa Ni re-sit tena Mwaka 2015 nikpata tena zero na hapo safari yangu ya Kumiliki cheti Cha kidato Cha nne ikakwama .

Tena mwaka 2016 nilifanya paper la form four na nikapata tena zero hivyo nikawa jumla nime-score zero 3 ndani ya miaka 03. Mfululizo.

Je, ilikuaje nikapata degree na hapa ndo ntaleta funzo kuwa Impossible is possible?

ITAENDELEA
 
Ulipata zero Mara tatu maana yake ulipewa taarifa tumia kipaji achana na elimu ili uwe tajiri!

Wakati mwingine unafeli ili ufanikiwe kupitia kipaji au kilimo

Sema watu huwa tuna kariri njia moja ndiyo maana hatuwi matajili

I bet kama una digrii itakuwa ya mchongo na kamwe haitakupa utajili zaidi utapata hela ya kula tu
 
SEHEMU YA 2

Baada ya Kupata zero mara tatu
Niliwaza Sana nifanye Nini ili nipate cheti Cha Form four ndipo nikipata wazo la kuondoka Bukoba na kuja jijini Daslama

Wakati sijaondoka kuna Daslama nikapata kesi ya mtandao na kupelekwa police Central Bukoba Mjini na hapo ndo nilizika ndoto zangu za Kupata cheti Cha kidato Cha nne na kuanza kupambana. Na kesi

Hakika hi kesi iliharibu future yangu na kupoteza mwelekeo na ndugu na Jamaa walinitenga .

Ghafla nilitolewa police Central na kuletwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya matumizi mabaya ya mtandao hapa nilikana kosa . Bwana Hakimu Alisema Dhamana hipo wazi na Je Nani ataniwekea Dhamana jibu Ni hapana hivyo nilipelekwa GEREZANI moja kwa moja Pale Bukoba Mjini.

Jambo ili niliona Kama nipo naota kumbe Ilikuwa kweli it was real situation .

Maisha ya Gerezani yanaanza huku nikiwa Sina msaada wowote ndugu wamenikataa achilia Mbali marafiki.

Hiyo Ilikuwa mwaka 2017 ndani ya Jela nakutana na Mzungu akiitwa Robert huyu was very smart guy akipambana na Serikali wampe Ardhi yake na huku serikali ikikataa kumpa Ardhi yake na kumruhusu
Apewe (Deportation) au aendelee kukaa Gerezani na yeye aliamua kukaa ndani na kuikataa hiyo Deportation ya kurudi kwao Canada

Huyu mzungu ndugu Robert ndo alichangia kwa kiasi kikubwa mimi kutimiza ndoto ya Kupata degree baada Kuhakikisha ananikutanisha na wakongwe wa sheria na watu wa Elimu , ndani ya Jela nilianza kuiona Future na kuona Mwanga

Safari inaanza kutoka Jela kwa dhamana na kwenda kusoma hakika Kesho ni fumbo

ITAENDELEA
 
maxresdefault-2.jpg
Leta hiyo chai mchana sili
 
Najaribu kufutilia mafaili yote kaama kuna mzungu Peter alikuwa jela kipindi hicho,naona hapa kuna peter kamachumu,peter kalumuna,peter kahatano,peter ngaiza,peter bushoke.

Ntawapa mrejesho wa hii chai.
 
Back
Top Bottom