Safari za mabasi usiku kusitishwa: Changamoto ni nini?

Safari za mabasi usiku kusitishwa: Changamoto ni nini?

gango2

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
1,956
Reaction score
2,274
Habari wanabodi!

Hivi karibuni tumeona baadhi ya watoa huduma za usafirishaji abiria kuendelea kutatuna huduma zao na kuwa wabunifu kwa kuanza safari za usiku na kufika asubuhi. Lakini ghafla tukaona safari zimesitishwa kwa taarifa wamezuiwa na mamlaka husika.

Tumeona kampuni ya KAPRICON ilitoa taarifa wamepeleka maombi LATRA kuanza safari za usiku Dar-Arusha toka mwezi Julai na wakapotea bila majibu licha ya abilia wengi kuuliza.

Wakaja KILIMANJARO wao walipotangaza tu, abiria wakawa wengi sana na wakajikuta wanaongeza mabasi mpaka 4 kila siku, na gari zikawa zinajaa na abiria wengine kukosa tiketi, lakingi baada ya siku kama 3 tukasikia wamesitisha safari mpaka watakapo julisha uma. Kama haitoshi kuna basi la MAJINJA wao walikuwa nasafari za Dar-Mbeya kila siku saa 10jioni na kufika saa 11 asubuhi (wao wanaita hakuna kulala) nao toka wiki iliyopita wamesitisha licha ya abilia kuwa wengi.

Sasa licha ya watu kuonyesha interest sana kwenya safari hizi na kuonyesha zingeweza kuinua shughuri za kiuchumi tunaona zimezuiwa, changamoto ni nin? Kwa kweli natamani kufahamu sana shida ni nini na pia je haiwezekani kutatuliwa safari hizi zikarudi.
 
Shida inaweza kuwa👇
IMG_20210827_154905.jpg
 
Pengine ni majungu ya wamiliki wa Mabus imepelekea serikali kuingilia kati
 
Kwa kweli kilio changu kilikuwa ni mabasi yasafiri usiku na kufika vituo vya mwisho asubuhi ili kuwawezesha abiria kuendelea na shughuli zao.

Kama imesitishwa inasikitisha sana.

Kilichotakiwa kuongezwa ni usalama. Trafick wawe sehemu husika kuangalia mwendo wa mabasi hayo.

Madereva kuwa wawili wawili na wakaguliwe mara kwa mara.

Hii ya mabasi kufika mwisho wa safari saa 8 usiku haina tija kabisa.
 
Usiku vyuma vinatembea, engine ya bardii ni kuvesha na kuvua tu!
 
Njia ya kaskazini ni salama sana, magari mengi mno barabarani usiku. Kuna Greenland bus toka mbeya huwa inafika Segera Tanga saa 6 usiku na Kilimanjaro inaingia saa 12 asubuhi
Mkuu hiyo Greenland ndio ile Zeland?
 
Back
Top Bottom