GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wala yeye haelewi kuwa humpendi na maisha yake yanaendelea kama kawaida.
Chuki ya wengi kwa Maulid Kitenge ni kwamba wanaona kuwa ' Jamaa ' hana Elimu yoyote kubwa kulingana na wao ( Wasomi ) waliopo humu JF lakini Yeye ( Maulid Kitenge ) ni maarufu, ana Pesa na maendeleo makubwa mno Kimaisha kitu ambacho pamoja na huo Usomi wao bado hawajamfikia na kuna hatari pia hata wasije kumfikia. Huo ndiyo ukweli Mkuu.
Jamani tunaojiita Wasomi tukumbuke kuwa kusoma sana hadi kufikia ngazi mbali mbali za ' Kitaaluma ' siyo ' justification ' ya Wewe kuwa tajiri au na mafanikio makubwa maishani ILA tu tukumbuke kwamba katika maisha ya Binadamu pia kuna suala la ' Bahati ' na pia kujua ' kuzichanga ' vizuri ' Karata ' zako za Kimaisha.
Na Mwenyezi Mungu alivyo wa ajabu kadri tunavyozidi ' kumnanga ' Maulid Kitenge kwa ' roho ' zetu za ' husuda ' basi ndiyo kwanza Mungu anamzidishia Yeye na vile ambavyo pengine alikuwa anataka kutupa anaghairi na vyote anavielekeza kwake ( Maulid Kitenge ).
Habari ndiyo hiyo!