Kwenye msiba mimi sina lawama.
Na hata hizo safari nyingine zinazoweza kuwa na tija, zikifanywa vizuri, siwezi kumlaumu.
Rais hatakiwi kutapanya fedha kwa safari zisizo na tija.
Lakini pia, rais si mwali ajifungie nyumbani tu.
Unaweza kulalamika rais kafanya safari ya kutumia dola milioni moja, ukasema hizo ni pesa nyingi sana. Lakini, kama hiyo safari imeleta faida ya dola bilioni moja, then it is justified.
Kuna namna ya ku balance kusafiri na kukaa ndani.
1. Safari ziwe na cost benefit analysis nzuri. Tujue rais anaenda kufanya nini, anaenda ku represent intetests gani za kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia.
2. Safari ziwe na uwazi. Tujue gharama, tujue sababu, tuweze kupima.
3. Safari ziwe na jumbe ndogo zinazolipiwa na serikali, zikiruhusu wajumbe wengine watakaoandamana na rais, kama wafanyabiashara walioidhinishwa, kuwa katika msafara wa rais, kwa kujilipia wenyewe gharama zote.
Mimi huwa namsema sana Magufuli, vibaya. Lakini, katika hili la tatu, Magufuli aliweza kudhibiti vizuri sana ukubwa wa jumbe za Tanzania hususan kwenye mikutano ya UN New York City.
Jumbe za Tanzania nje kabla ya Magufuli zilikuwa zinafanya kufuru.
Nakumbuka niliona ripoti moja ya TV ya New York City (local news), walifanya expose ya mabalozi wa nchi/ UN delegations za kiafrika walivyokuwa wanatanua kwenye hoteli za bei mbaya za New York City, na kufanya shoppings za kufa mtu.
Lakini, walitoa mfano mmoja mzuri wa ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri Augustine Mahiga ulivyokuwa mdogo na ulivyokaa kwenye hoteli za bei nafuu sana.
Tunaweza kufanya hizi safari kwa tija tukakataa rais kutokuwa na safari kabisa kwa upande mmoja na kusafiri sana kwa upande mwingine.
Tatizo moja naliona Tanzania tunakuwa sana watu wa "all or nothing at all".
Mtu kama Magufuli aliona tatizo la rais kusafiri sana, akatuletea tatizo lingine la rais ambaye hasafiri kabisa.