Mhe. Rais alienda SADC kama mjumbe siyo kama mgeni, aidha, Msumbiji na Malawi kwa nyakati hizo hazikuwa na official state visit toka Tz; ambayo ni bilateral (nchi na nchi) badala yake multilateral (SADC/nchi 16). Tumtendee mama haki anayostahili, hivyo basi hesabu za 8 kwa 10 (idadi ya miezi ya kutamalaki nchi dhidi ya idadi ya ziara) inaweza isiwe hoja yenye ushawishi.
Katika ziara 10 alizofanya, ziara 4 ni za mikutano ya jumuiya za kimataifa (UN, Uskochi, SADC X2), ni ziara 6 tu ndizo za mahusiano ya kimataifa (za kiserikali) kati ya nchi na nchi (Tz na UG, RW, KE, ZM, BI & EG). Tangu aingie madarakani miezi 8 sasa, Mhe. Rais SSH amefanya ziara moja tu ya mbali ya kiserikali ambayo ni hii ya Egypt. Ziara zingine 5 za kiserikali alizofanya ni za kujitambulisha kwa majirani ambayo hii haikwepeki. Rais hajafanya ziara ya kiserikali nje ya bara la Afrika. Tija ya ziara hizi 6 alizofanya Mhe. Rais naamini inazidi matumizi yake. #Tumtendee haki Mhe. Rais.