View attachment 1749075
Habari za Kazi wana JamiiForums,
Katika thread hii nategemea tutaangazia ziara mbalimbali(Za nje ya nchi) za Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na manufaa kwa taifa.
Leo tarehe 11 April 2021 Mhe Samia anafanya ziara yake ya kwanza nje ya Tanzania na ziara hii ina lengo la kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.
Tarehe 4 mei2021 Mhe Samia amezuru nchi ya Kenya na kuwahitubia wananchi wa Kenya.
Ni ziara yenye tija kwa uchumi wa Nchi. Aidha ikumbukwe mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mpenzi wa ziara za nje ya nchi na mara nyingi alimtuma Mhe Samia Suluhu kumuwakilisha.
TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.