Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita (6) wa Tanzania mnamo Machi 19, 2021 baada ya mtangulizi wake Rais John Pombe Magufuli kufariki dunia mnamo Machi 17, 2021

Tangu kuapishwa kwake Rais Samia amefanya mengi ikiwa ni pamoja na ziara katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kukuza mahusiano na mataifa

Hizi ni Ziara alizofanya Rais Samia tangu alipopewa dhamana ya kuwa Rais wa Tanzania

Aprili 11, 2021 – Ziara nchini Uganda
Rais Samia alifanya ziara ya siku 1 – ambapo alifanya mazungumzo ya siri na Rais Yoweri Museveni na kisha kuhudhuria utiaji Saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tannga

Mei 04, 2021 - Ziara nchini Kenya
Rais Samia alifanya ziara ya siku 2 - ambapo alifanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kisha kulihutubia Bunge lilijumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili. Pia, alihudhuria na kuhutubia Jukwaa la Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania kwa lengo la kujadiliana kuhusu fursa zilizopo za biashara na uwekezaji kwa Kenya na Tanzania

Julai 16, 2021 - Ziara nchini Burundi
Rais Samia alifanya ziara ya siku 2 - ambapo alishiriki shughuli mbali mbali ikiwemo kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania

Agosti 2, 2021 - Ziara nchini Rwanda
Rais Samia alifanya ziara ya Siku 2 - ambapo alizungumza na Rais Paul Kagame pamoja na kushuhudia utiwaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari

Novemba 10, 2021 - Ziara nchini Misri
Rais Samia alifanya ziara ya siku 3 - ambapo alizungumza na Rais Abdel Fattah Al Sisi kuhusu maeneo kadhaa ya ushirikiano na Tanzania ikiwemo nyanja za dipolomasia, uchumi, elimu, utalii na huduma za kijamii. Pia, alishuhudia usainiawaji wa mkataba mmoja na hati 7 za makubaliano kati ya Tanzania na Misri

Februari 14, 2022 - Ziara nchini Ufaransa
Rais Samia alifanya Ziara - amekutana na kuzungumza na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Pia amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Aundrey Axoulay wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo. Pia, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani

Februari 18, 2022 - Ziara nchini Ubelgiji
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen leo Februari 18, 2022

Februari 24, 2022 - Ziara Falme za Kiarabu (UAE)
Rais Samia alifanya ziara ya siku 3, ameshuhudia utiaji saini hati za makubaliano ya mikataba 36 yenye thamani ya zaidi ya sh. trilioni 17.3 iliyohusisha sekta mbalimbali ikiwemo nishati, madini, miundombinu, kilimo na mawasiliano.

Pia, kuwa Mgeni rasmi na kuhutubia kwenye Siku Maalum ya Tanzania kwenye maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji Dubai Siku ya Februari 26 pamoja na Kuhutubia kwenye Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji Februari 27

Aprili 19, 2022 - Ziara nchini Marekani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo ashiriki kwenye uzinduzi wa makala maalumu iitwayo ‘Royal Tour’ jijini New York nchini Marekani.

Mei 10-11, 2022 - Ziara nchini Uganda
Rais Samia ziara ya siku 2 - atazungumza na Rais Yoweri Museveni ili kudumusha na kuimarisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii. Marais watajadili kuhusu nishati, bishara, usafiri, maendeleo ya miundombinu na sekta ya afya

Mei 23-25 - Ziara Nchini Ghana
Rais Samia ziara ya Siku 3 - atashiriki mdahalo wa Wakuu wa Nchi utakaojadili fursa zilizomo na changamoto zinazozikabili nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, kupanda kwa bei ya vyakula na matumizi ya nishati endelevu
Umesahau ile ya UN mwka jana, na hii ya juzi ya kuzindua Filamu ya Royal Tour
 
Ziara zote zina tija
Hakuna ziara ameenda kutembea bila faida
Kazi iendelee
Na hii ndio haswa kazi ya Uraisi inayompasa ,kunganisha nchi na nchi na kufungua mahusiano mema na mataifa rafiki na kudumisha urafiki na kuanzisha mikakati mipya , kwani kila nchi hubadili utawala kila baada ya miaka mitano au saba, na kwa hiyo kama Taifa tunalazimika ku ''Up To Date'' uhusiano na malengo ya kitaifa.
Ghana wanatengeneza KARATASI za Photocopy na wana viwanda vizuri tuu, mujuwe kuwa hivi sasa RIM moja ya ''photocopy paper'' hapa Tanzania ni Shs. 15,000- 25,000. Badala ya sh 6,000/ -10,000/=
Kwa wafanya biashara wa karatasi wanawez kufungua miango ya kuagiza karatasikutoka Ghana.

1653294639732.png
Ghana Product
 
Ukiwa mjinga ukaona mikwara kama hii unaweza kuamini kuwa nchi ina Rais😁😁😁
 
Anakula kwa mujibu wa urefu wa kamba yake!! Kigingi cha kamba kipo Dodoma Tz lakini kama ni ndefu hadi USA!!
 
Kumbuka usije changanya Safari Na Ziara hiyo ya Belgium na ufaransa was the same route , maana huu Uzi baadae utatumika Kama referral ya safari za Rais Ulaya , atahesabiwa mara mbili wakati ilikuwa ya Belgium na France ni same Route


Britanicca
Si ulisema unaodoka JF? Ndiyo maana mnakosa heshima JF Kama wewe Sasa hivi ulivyo.
 
Ziara ya Ghana inamatunda ya kikatiba ....anaenda kujiridhisha mchakato waliopitia sio wenu wakihuni eti akina makonda Paul wajumbe
 
Mpaka 2025, karibu Nchi zote Duniani atakuwa kashazitembelea.
Hapo tusitegemee hali nzuri ya Wananchi kiuchumi.
 
Wananchi wanakamuliwa ili kufadhili ziara za Rais.
 
Ktk list sioni safari zifuatzo.
1. Msumbiji June 22 2021
2. Malawi August 16 2021
3. Zambia August 24 2021
4. Marekani(Umoja wa mataifa) 23 sept 2021
5. Msumbiji January 28 2022
 
Back
Top Bottom