Sahihi kusema Arusha ndio Jiji bora Tanzania?

Point zote za juu ni kanjanja. Bora ungebaki na ile hali ya hewa na foreign community katika jiji ilo.

Ukweli kaskazini mmejaliwa hali ya hewa nzuri. Arusha wakae makini dom ikiendelea kuwezeshwa itamkuta hapo.

Jiji bora litabaki dar, mwanza
Kwa ile hali ya hewa ya Dodoma hata iwe na ghorofa kama za Dubai tayari imeshapoteza sifa za kulinganishwa na Arusha au Mwanza. Yaani mji utadhani chini ya Ardhi kuna watu wamewasha Moto, juu napo unakutana na Vumbi la ajabu, hata jua nalo sijui limeshuka
 
Watu wengi mna jadili kwa mihemko & mahaba badala ya kutoa hoja stahiki 😄
 

Nimecheka
 
Ni jiji la kitalii
Ni mtazamo potofu mno.
Nimejifunza kuwa karibu nchi nzima wanaiogopa Arusha bila sababu yoyote.
Nimeishi Arusha more than 10yrs na sijawahi ona ukatili unaozidi mikoa mingine.
Ni sehemu ndogo yenye wahuni mfano Unga ltd na Ngarenaro.
But the rest of Ar. watu wako peace sana, ni wakarimu na wanapenda wageni mno.
Note; watu wa Arusha hawapendi dharau, ukiwaletea dharau huna bahati hasa kabila la Wameru.
1. Warusha wanalaza mizigo stand ikisubiri kupelekwa sokoni hasa wafanyabiashara za alfajiri na hakuna wa kugusa.
2. Sehemu nyingi wanaanika nguo na zinalala nje haziguswi...sio sehemu zote lkn.
3. Watu wanaheshimiana mno na hawajui utani kama watu wa Pwani, ukileta matusi na mizaha pia huna bahati.
4. Katika yote 70% ya wakazi wake wamestaarabika na wana maendeleo binafsi.

Naongea kwa uzoefu kwani kwa nature ya kazi yangu nimeishi mikoa yote.
Jiji la Arusha ndilo limestaarabika kuliko mkoa au jiji lolote Tanzania.

Naruhusu unipinge kwa hoja na uniambie wewe unalipa jiji/mkoa gani credit zaidi ya Arusha.
Nitajie na sifa zake mkuu.
Arien
Unahisi haya nayo mahaba mkuu?
 
Ila kwa kweli Dodoma bado sana kuilinganisha na Arusha. Labda wivu wa watu tu. Arusha hailinganishwi na Mbeya, Tanga na hata Mwanza.
 
Arusha ina Mahotel ya maana, ina majengo makubwa ya biashara, ina barabara nzuri, Arusha-Moshi/Nairobi, Arusha-Babati -Dodoma na Barabara ya By-Pass ni barabara bora kabisa kwa sasa hapa nchini. Na sijaona mji mwingine ambao barabara za mitaa zina lami kwa Arusha.
 
Mwanza haina uzuri na sifa xa Arusha
Fact
kila mtu anayejielewa lazima atakubaliana na mada hapo juu
Arusha iko mb
Ila kwa kweli Dodoma bado sana kuilinganisha na Arusha. Labda wivu wa watu tu. Arusha hailinganishwi na Mbeya, Tanga na hata Mwanza.
wivu tatizo wanadhani wakisifia watakua ni weak kusifia ndio ishara halisi ya strength ndo maana wageni kutoka nje wakija kwetu wanafurahia walichokikuta ila hawa wenzetu wanajua Arusha iko mbali sana wanaona wakisifia watakua inferior na hio ndio inaitwa inferiority Complex hasa😢
 
hao wanaosema vibaya Arusha ni wahuni tu ambao hata hela ya kutembea kuja Arusha hawana🤣
sasa hivi tunavoongea sheikh amri abeid pale kunaendelea mashindano ya wabunge wa nchi zote eac yani watu na wakarimu mno wabunge wanajichanganya na watu wa kawaida mno mtaani huko unakutana na wabunge wanatembea kwa miguu bila bugudha yoyote
lakini utashangaa mtu anasema Arusha ni ya kikatili lakini mkoa anaotoka ndio unaongoza kuuwa albino na vikongwe sad😢
 
ukiwaambiaga wapinge kwa hoja hapo ndio wanapoanza kukimbia kimbia
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]umechana vibaya mno mkuu
 
Mkuu Arusha sawa ni mji mzuri! Ila kuhusu watu kuja kutembea arusha issue ya hela sio tija! Unataka waje kufanya ni I Arusha? Halafu ujie hela ipo popote pale ila sema nyie mnatabia za kishamba za kuvimba kisa una milioni mbili mfukoni! Nenda hata njombe au kahama utaniambia vijana gani wana hela arusha kuzidi wa kahama au njombe!
 
akikutumia hio picha nitag[emoji1787][emoji1787]
Msijidanganye,Mwanza sio level ya Arusha.
Arusha ipo chini sana katika viwango vyote kulinganisha na Mwanza na hata Dodoma kwa sasa.
Miji mingine inakuwa lakini Arusha imebaki kama ilivyo miaka 10 iliyopita.
Poor Arusha na viongozi wake
 
Umezungumzia Jiji ama Mkoa?
Duh
 
Stendi kuu mpya ya mabasi ya nyamhongolo ilemela Mwanza....


 
Hata Dubai ilikuwa na hali mbaya zaidi ya Dom ila leo ni tamu kuliko Dar au Nairobi..

Ni hivi Dom itawakimbiza Sana hizo Jiji uchwara.By 2030 Dom ndio itakuwa second City baada ya Dar kwa kila kitu.
 
Msijidanganye,Mwanza sio level ya Arusha.
Arusha ipo chini sana katika viwango vyote kulinganisha na Mwanza na hata Dodoma kwa sasa.
Miji mingine inakuwa lakini Arusha imebaki kama ilivyo miaka 10 iliyopita.
Poor Arusha na viongozi wake
Viwango vyote kama vipi? Mwanza si inaizidi Arusha kwa slums na poor people au kuna kingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…