Ni mtazamo potofu mno.
Nimejifunza kuwa karibu nchi nzima wanaiogopa Arusha bila sababu yoyote.
Nimeishi Arusha more than 10yrs na sijawahi ona ukatili unaozidi mikoa mingine.
Ni sehemu ndogo yenye wahuni mfano Unga ltd na Ngarenaro.
But the rest of Ar. watu wako peace sana, ni wakarimu na wanapenda wageni mno.
Note; watu wa Arusha hawapendi dharau, ukiwaletea dharau huna bahati hasa kabila la Wameru.
1. Warusha wanalaza mizigo stand ikisubiri kupelekwa sokoni hasa wafanyabiashara za alfajiri na hakuna wa kugusa.
2. Sehemu nyingi wanaanika nguo na zinalala nje haziguswi...sio sehemu zote lkn.
3. Watu wanaheshimiana mno na hawajui utani kama watu wa Pwani, ukileta matusi na mizaha pia huna bahati.
4. Katika yote 70% ya wakazi wake wamestaarabika na wana maendeleo binafsi.
Naongea kwa uzoefu kwani kwa nature ya kazi yangu nimeishi mikoa yote.
Jiji la Arusha ndilo limestaarabika kuliko mkoa au jiji lolote Tanzania.
Naruhusu unipinge kwa hoja na uniambie wewe unalipa jiji/mkoa gani credit zaidi ya Arusha.
Nitajie na sifa zake mkuu.
Arien
Unahisi haya nayo mahaba mkuu?