TANZIA Said Akachube (Akachube Road) ambaye ni muuza magari maarufu DSM afariki dunia

TANZIA Said Akachube (Akachube Road) ambaye ni muuza magari maarufu DSM afariki dunia

Unaweza kujadili hoja na si kunyooshea vidole mtu?
Nani kakwambia hii inamhusu yeye binafsi?
Unaijua nguvu ya kutokuwa na kauli thabiti kwa jambo lolote kweye jamii hata kama wewe si kiongozi wa juu.
Kauli ipi thabiti ya kiongozi inahitajika?
 
Tatizo watu wakivaa barakoa viongozi wa serikali wanazuia, rejea kilichotokea moshi
Kwani njia pekee ya kupambana Ni barakoa? Mbona zile measures zilizotolewa na wizara ikiwemo barakoa hazijazuiliwa? Mbona barakoa zinavaliwa huku mtaani kwa wanaohitaji na hakuna anaekamatwa kuzuiliwa?
 
Muuza magari maarufu jijini Dar es Salaam, Akachube afariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Ndugu wa karibu wamesema amefariki kwa ugonjwa wa Nimonia.

Umaarufu wake ulipelekea mpaka kupewa barabara ya Akachube iliyopo Kijitonyama.

Mungu ailaze pema peponi roho yake.
Bro hivi kansa, kiharusi, magonjwa nyemelezi, ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu yalienda likizo sasa hayaui?
 
Unaweza sema vyovyote, lakini sina uhakika kama unajua thamani ya magonjwa ya mlipuko hata kama yana dawa au hayana dawa. Ni masuala yanayohitaji umakini na si kauli nyepesi kama hizi zako.
Kauli ipi hiyo nzito waitaka?
 
Ni kiherehere chake tu,mbona kipindupindu kipo,malaria ipo,ukimwi upo,sukari ipo,kansa ipo,lakini asihusishwe navyo? Mtu huyu anahukumiwa kwa maneno yake!! Si kwa ukimya wake,anasema hakuna corona tanzania,na anajua kabisa kuwa kuna wajinga wengi sana tanzania ambao wataweza kumwamini na kuishi kama vile kweli hakuna corona,matokeo yake ni kuwa wataambukizwa na kuwaambukiza wengine,ni kama vile anavyosemaga kuwa tanzania ni nchi tajiri sana wakati tulishafundishwa kuwa tanzania ni nchi masikini na tukaridhika na kuishi kama masikini,sasa anavyotuambia kuwa sisi ni matajiri huku matumbo yana njaa na nguo zina viraka hapo ndiyo anatuamsha usingizini tuanze kudai mgao wa utajiri wa nchi yetu,ambao kiukweli wanasiasa ndiyo wanaougawana, mtu kama magufuli aliyekaa kwenye madaraka kwa zaidi ya miaka 25 akituita matajiri tunajua tu anatudhihaki,akisema hakuna corona ni kama anatutukana kwa kutuona hatuna akili na mwenye akili ni mmoja tu ambaye ndiye yeye
Hakuna corona halafu unaambiwa ujikinge nawe ulivyo bongolala unashindwa kuchanganya akili....
Nchi tajiri wa rasilimali ambazo zimeshindikana kumnufaisha kila mwananchi
 
Kwa hiyo kama wao wamekufa, wanakupa haki yako wewe pia kufa. Wewe unashindwa kutimiza yaliyo yako kwa kuwa wale wamekufa? Nafikiri unahitaji factory reset ili urudi kwenye logical thinking. Tathimini kauli zako kabla ya kuziandika.

Tunajua ni kwa kiasi gani tuko imara kwa mfumo wa miili kibailojia ukilinganisha na wenzetu kwa ugonjwa husika ingawa mifumo yao ya afya iko imara ukilinganisha na ya kwetu. Let us utilize that small difference to make better outcome by having better approach referring to my first post.
Subiri kauli uweze jikinga
 
Utatoa takwimu pasipochukuliwa takwimu halisia? Just for observation tuendelee na maisha tuone kati ya phase 1 na hii phase II, ipi itatuliza sana baada ya kwanza kujitahidi kutumia njia mbali mbali na hii tuliyokaidi.

Mwenyezi Mungu atupitishe salama pamoja na ukaidi wetu wa kushindwa kutumia akili zetu vyema na maarifa aliyotujalia ili tufanye post-mortem wote.
Ukaidi upi?
 
"Chukueni tahadhari na kufuata muongozo wa WHO kupitia wizara ya afya, Corona ipo na inaua"..

Unajua kaka, Mh.Rais amefanya hata mtu ukivaa barakoa kwa sasa uonekane kituko.?????
Chukua tahadhari achana na ukituko shaurilo
 
Kwani njia pekee ya kupambana Ni barakoa? Mbona zile measures zilizotolewa na wizara ikiwemo barakoa hazijazuiliwa? Mbona barakoa zinavaliwa huku mtaani kwa wanaohitaji na hakuna anaekamatwa kuzuiliwa?
Mzee sijakuelewa unabisha hakuna walioamua kujikinga kwa barakoa wakavuliwa?
 
Mpaka sasa sijapata historia iliyokamilika kuhusu marehemu, zaidi ya mabishano na ujirani wa makazi kwa baadhi ya wadau.
 
Back
Top Bottom