TANZIA Said Akachube (Akachube Road) ambaye ni muuza magari maarufu DSM afariki dunia

TANZIA Said Akachube (Akachube Road) ambaye ni muuza magari maarufu DSM afariki dunia

Muuza magari maarufu jijini Dar es Salaam, Akachube afariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Ndugu wa karibu wamesema amefariki kwa ugonjwa wa Nimonia.

Umaarufu wake ulipelekea mpaka kupewa barabara ya Akachube iliyopo Kijitonyama.

Mungu ailaze pema peponi roho yake.
Hivi Niminia ndo Deportivo au Ni tofauti jamani
 
Muuza magari maarufu jijini Dar es Salaam, Akachube afariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Ndugu wa karibu wamesema amefariki kwa ugonjwa wa Nimonia.

Umaarufu wake ulipelekea mpaka kupewa barabara ya Akachube iliyopo Kijitonyama.

Mungu ailaze pema peponi roho yake.
Weka picha
 
Aisee kila siku nina zidi kuhisi jinsi maisha yalivyo mafupi!
Mungu angalau ange tupa nafasi ya kuaga ndugu na marafiki!
Tuishi kwa upendo tuu, tulishaambiwa siku zetu duniani ni chache na zimejaa dhiki
 
Ni lini watu waliacha kufa kwa Nimonia hadi mlete taarifa kwa bashasha namna hii? Kipi kimewafurahisha?
 
Haya wahi malimao na tangawizi
Kama kawaida binadamu kama halijampata. Kila mtu anaogopa kifo japo kuwa tunajuwa ni lazima utakufa tu. Hakuna shujaa katika kuumwa ugonjwa wowote lazima uchukuwe tahadhari na wala hakuna aliyesema ugonjwa huu wa maajabu ni kama kipindupindu hakuna mtu anadharau na ukidharau unakubeba tu. Corona kama magonjwa mengine tatizo lake hatujui tunagombana na nini wala adui hatumuoni. Hawa wengine sijui malaria, kipindupindu tunajuwa na tunamuona adui huyu bwana mkubwa Corona hatumuoni kimya kimya.
 
sijawahi kuona umuhimu wa kuvaa hizo barakoa zaidi ya kutesana tu na kushindwa kupumua
Ndiyo maana nakueleza ujisomee kabla ya kutoa chochote. Kwa tunachokizungumzia, ulitakiwa uwe na group la watu ambao wanatumia intervention/kinga dhidi ya wale wasiotumia then remove the biases.
Hapo ndoo utazugumza una data/ takwimu. Hii ni orodha tu isiyokupa chochote kwa tunalolizungumzia hapa.
 
2017 tulienda kuchukua Harrier old model na mjomba,kwakweli maisha hayana thamani japo tunaitafuta mipesa
 
Back
Top Bottom