Said Issa Mohamed aliyeishtaki CHADEMA atimuliwa rasmi Uanachama kwenye chama hicho

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
1780826823645.png

TAARIFA KWA UMMA​

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pemba kinaujanisha umma na wanachama wake kuwa Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba iliketi katika kikao chake cha dharura tarehe 06 Juni 2026 katika Ukumbi wa Pride ya Zamani, Chake Chake, Pemba. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kanda, Mheshimiwa Omar Nassor, kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za Chama.

Ajenda ya kikao ilikuwa ni kujadili suala la nidhamu linalomhusu Ndugu Said Issa Mohammed. Kamati ilipokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa mbele yake na kufanya tathmini kwa kuzingatia masharti ya Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama.

Baada ya kujiridhisha kuwa Ndugu Said Issa Mohammed amekiuka Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama, Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba imeazimia kumfukuza uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuanzia jana tarehe 06 Juni 2026.

Kutokana na uamuzi huo, Chadema Kanda ya Pemba kinautaarifu umma na wanachama wote kuwa kuanzia tarehe tajwa, Ndugu Said Issa Mohammed si mwanachama wa Chadema na hatambuliki tena kama kiongozi au mwakilishi wa Chama katika ngazi yoyote. Hivyo, kauli, matendo au shughuli zozote atakazozifanya baada ya tarehe hiyo zitakuwa ni za kwake binafsi na hazitahusishwa na Chama.

Imetolewa leo Jumapili tarehe 07 Juni 2026 na:

Pia soma: CHADEMA Zanzibar watoa Tamko, Wasikitishwa na madai ya Said Issa Mohamed kuwa aliishtaki CHADEMA kwa niaba yao
 
Kuna mapungufu machache katika huu waraka.
1.Ingawa inasema amefukuzwa na kanda ya Pemba, letter head ni ya Unguja.
2.Walitakiwa wataje vifungu vilivyokiukwa.
Barua kama hizi zinapaswa kuandikwa kwa umakini ama sivyo
mambo kama haya yataweza kumpa nafasi ya kuwasumbua tena.

Amandla...
 
View attachment 3602875

TAARIFA KWA UMMA​

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pemba kinaujanisha umma na wanachama wake kuwa Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba iliketi katika kikao chake cha dharura tarehe 06 Juni 2026 katika Ukumbi wa Pride ya Zamani, Chake Chake, Pemba. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kanda, Mheshimiwa Omar Nassor, kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za Chama.

Ajenda ya kikao ilikuwa ni kujadili suala la nidhamu linalomhusu Ndugu Said Issa Mohammed. Kamati ilipokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa mbele yake na kufanya tathmini kwa kuzingatia masharti ya Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama.

Baada ya kujiridhisha kuwa Ndugu Said Issa Mohammed amekiuka Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama, Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba imeazimia kumfukuza uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuanzia jana tarehe 06 Juni 2026.

Kutokana na uamuzi huo, Chadema Kanda ya Pemba kinautaarifu umma na wanachama wote kuwa kuanzia tarehe tajwa, Ndugu Said Issa Mohammed si mwanachama wa Chadema na hatambuliki tena kama kiongozi au mwakilishi wa Chama katika ngazi yoyote. Hivyo, kauli, matendo au shughuli zozote atakazozifanya baada ya tarehe hiyo zitakuwa ni za kwake binafsi na hazitahusishwa na Chama.

Imetolewa leo Jumapili tarehe 07 Juni 2026 na:

Pia soma: CHADEMA Zanzibar watoa Tamko, Wasikitishwa na madai ya Said Issa Mohamed kuwa aliishtaki CHADEMA kwa niaba yao
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kinashangaza sana!, kina katiba, yenye taratibu zote za nidhamu, lakini kwanini zinaendelea kufanya maamuzi kwa a kangaroo court?!.
  1. Hatua ya kwanza ni kwa Said Issa Mohammed kuandikiwa barua ya kusimamishwa uanachama kwa maandishi ya mashitaka, yenye tuhuma mahsus na kutakiwa kujibu kwa maandishi ndani ya siku 14
  2. Ndipo kinaitishwa kikao cha nidhamu, na kumpa fursa ya kusikilizwa.
  3. Baada ya hapo ndipo wanafikia maamuzi ya kumfukuza baada ya kuthibisha tuhuma
  4. Barua hiyo ya kumfukuza pia inamuonyesha kama hajaridhika na uamuzi huo, ana haki ya kukata rufaa kikao kinachofuatia.
  5. Walipowatimua wale madiwani wa Arusha, tuliwaeleza Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
  6. Walipomtimua Juliana Shonza, tuliwaeleza Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
  7. Walipowatimua Zitto, Kitila na Mwigamba, tuliwaeleza Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
  8. Walipowatimua wale 19, pia tukawaeleza, Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
  9. Mlipo mtimua Kafulila na kumuita Sisimiza tuliwaeleza Kafulila, hiyo sio njia sahihi ya kujenga chama chako cha NCCR- Mageuzi
  10. Na sasa ndio linakuja hili!, I thought Chadema ni smart enough kulijua hili jitu jinga, liko funded kuwapotezea muda, focus na concentrations, you should have done the right thing and do it right, au nyinyi mnaenjoy hizi courtroom drama?.
P
 
Hilo ndio imeisha
 
Back
Top Bottom