Lugumi alisema mwenyewe kasafiri usiku kupitia airport ambayo inalindwa na wala hakukuwa na tatizo, msemaji wa kampuni anasema ni uzushi.
Kusafiri kwa mkurungezi ni maisha yake binafsi na kazi yake na wala siyo hoja inayoshindaniwa hapa.
Msemaji anataka watu wanyamaze kwa sababu eti mkataba wake ulitaka kama kuna dissatisfaction yeye ama jeshi la polisi ndio tu wana nafasi ya kuraise concern. Anasahau kwamba Jeshi la polisi na yeye walikuwa wanaogelea kwenye fedha za walipa kodi wa TAnzanai ambao ni zaidi ya polisi na lugumi. Anasahau kwamba fedha yoyote ya umma katika mikataba haiishiii kwa hao wabia tu bali ina mkono wa tatu unaowakilisha umma. Yeys Lugumi hataki!. Tanzania!!!!!!!!!!!
Anasema uzushi mtupu na uwongo wa kupuuzwa. Ni upi uzushi? Kama msemaji wa Lugumi angelikuwa hatetemiki, asingetufokea tunyamaze na kutuambia tupuuze habar zinazoashiria kuwa chanzo cha mateso na maumivu vikiwemo vifo vya ndugu zetu wengi Watanzania. Tumepoteza ndugu zetu kwa kukos ahuduma za afya, misongo ya mawazo na maisha magumu kwa ajili ya mfumo fisadi ambao lugumi anataka tuupuze.
Katika hali ya kawaida, nilitgemea Lugumi angekathibitisha kwamba hakpata tenda kwa favoritism kwa sababu ni mkwe wa aliyekuw IGP na kwamba kazi ilitangazwa kweny eTender board, alitenda na kuwashinda wenzake kihalali.
Alitakiwa athbithishe kwamba fedha alizopewa ndiyo thamani halisi ya mradi huo na kwamba billion 5 za training ya viongozi watano ama ni gharama halisi ya mafunzo hayo; au haikuw abillioni tano bali ilikuw akadhaa, ama waliokwenda mafunzo hawakuwa watano bali walikuwa atu kadhaa.
Nilitegemea msemaji wa lugumi aseme kwamba kazi hiyo ilifanyika kama mkaaba ulivyotaka na kumalizika ndani ya muda sahihi kwa gharama na kiwango sahihi na kwamba mashine hizo zilikaguliwa na kuwa ziko katika ubora unaotakiwa kabla hajalipwa fedha zote.
Kusema tu "Tulishirikiana na wabia wetu wote kama ilivyo katika kutekeleza mkataba ili utekelezeke bla bla ..... hakuna kati yetu aliyelalamika....", ni mzaha kwa Watanzania wanaoteseka sana kwa sabbu ya ufisadi. ananikumbusha na msemo wake kwamba "siyo kia jipu linatumbuliwa".
Ninaomba tu Watanzania kwa ajli y ahii scenario, tuingalie kwa mtazamo wa kupima thamani ya elimu ya Tanzania dhidi ya elimu sahihi. Awamu ya nne ilipoua elimu and kuojiondolea kabisa ufahamu juu ya maana wala faida ya kuwa na elimu bora, sijui ilikuwa inalenga kuwa na taifa la aina gani.
Lakini hii ya Lugumi ndiyo taswara sahihi na halisi ya :BRN, na taifa lililokuwa likitengenezwa na awamu yanne ambayo haijaelewa hata kukubali kwamba muda wake sasa umekwisha na hautakaa urudi tena. Good bye BRN.