Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Hapa naona hii taarifa imekanusha kwamba LUGUMI haja toroka na pia hajakamatwa nje ya nchi.
Kiukweli sioni kama hii taarifa ya mleta uzi imekamilika na kujitosheleza hata kuweza kuwa hadaa wadanganyika kwa hili saga la LUGUMI.
Sasa siutuletee taarifa ambayo sio ya upotoshaji na vithibitisho kadhaa ili tuache kumchafua huyo LUGUMI...
 
Unataka ujibiwe hoja wewe nani? Kama unaona umeonewa nenda kashitaki kuliko kubweka bweka humu kwenye mitandao. Upewe hoja wewe nani? kwanini?
Kama unaona hapa si sehemu sahihi kwani kaileta humu?.Wewe unatetea usifadi kwa manufaa ya nani?.Hawa wanaohoji ndiyo walipa kodi na wanataka kujua jinsi kodi yao ilivyotumika.
 
Tuliwaambia wanalindana, tayari wameshapata ''ulinzi''

Hawaelezi tenda waliipata lini, kwanini wamelipwa 100% kazi ikiwa bado n.k.

Hawa CCM na Watumbua majipu ni wale wale, wanalindana ndio maana mafisadi wanatamba. Hii serikali haiwezi kuwa tofauti na zingine

Wanalindana! kesho anatumbuliwa Anne K Watanzania wanashangilia

Wameshawalinda tayari, kama ilivyo kwa kashafa nyingine
 
Kwa mtindo huu kila ufisadi ungekanushwa kwa vijitaarifa kama hivyo basi kusingekuwa na ufisadi wowote nchini.
 
Kama sikosei huyu Juma Moshy Sabury aliyesaini hiyo press release ni miongoni mwa wamiliki wa Lugumi Enterprises, wapo yeye na Lugumi according to Brela.
 
Kwa mbali barua hii inafanana na ile ya kukanusha umiliki wa UDA baada ya magazeti kuihusisha na mtoto mmoja wa kiume!
Ukiondoa hii tender ya billion 37, kazi ambazo hii kampuni imeshapewa ni nyingi na za thamani kubwa na malipo yao yanatoka huko huko serikalini. Hivyo ku-clear doubt wangeitisha japo press conference na kuruhusu maswali hata 100 ili kila mwenye mashaka aridhike. Lakini kuja na karatasi zisizo na tarehe wala cheo, Wallah wameongeza maswali hata yaliyokuwa hayajadhaniawa! ...lakini jamani, mbona watz wengi wanajua hii kitu!!!!
Kwani Lukindo aliyekwambia katika umiliki wa Lugumi mtoto wa kiume hayupo ni nani?Nikikumbuka vizuri alitajwa mapema ndio kwanza sakata limetolewa uwanjani.Hofu yetu hapa ni kupuuzwa na kumalizika kimya kimya kwani hili sakata linawahusisha wakubwa wengi waliopo serikalini na wastaafu.Wote hao bado wana ushawishi mkuwa serikalini na hata kwa dpp na hawatakubali kijana wao aumbuke na.siri nyingi zifichuke. Asante kwa like.
 
Kwani wewe ni Mtanzania? Mbona tunakujua kabisa kuwa wewe ni Mkenya?
Mkuu unaweza kutuambia haya masalia yenu ya mafisadi Magu anaweza kumaliza? Naona kila upande yowe na wote wahusika ni CCM na vibaraka vyake
 
Unapoona mtu anajibu bila kutoa takwimu ujue hiyo ni ngonjela na sio majibu ya hoja. Nimeona maandishi yapo kwenye karatasi rasmi lakini sijaona point hata moja. Jibuni hoja kama mnataka
 
Hivi kwa nn sheria ya kunyonga haitekelezwi? Mtu kama Lugumi niwa kunyongelea mbali haraka iwezekanavyo, halafu anasema eti tuzipuuze hizo taarifa zinazoenezwa ni uzushi tuendelee kulijenga taiafa? yaani sisi tujenge wakati wewe unabomoa?
TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI NA AKINA LUGUMI NI WACHUMAJI...RAISI HIVI HILI JIPU HULIONI? JWA NINI CHARLES KITWANGA ALICHELEWA KUPELEKA NA KUJAZA FORM ZA MAADILI WAKATI HAKUWA NA SHUGHURI YOYOTE ILE.
 
Cc Annael
Ili mimi binafsi nipuuze taarifa zinazosambazwa naomba kujua kama pesa hizo kweli mmelipwa kiasi gani na mnadai kiasi gani na tayari mmfunga machine ngapi na bado ngapi na mnategemea kumaliza lini na mkataba uliwataka kumaliza lini baaaasi.. Then nitapuuza
 
Lizaboni hebu njoo umjibu huyu!anauliza maswali ya ajabu ajabu yale tuliyokatazwaga kuuliza kule kwetu.
Wameshafunga mashine au bado, kama bado je wameshachukua pesa (wameshalipwa) kama wamelipwa kabla ya kufanya kazi hapo ndipo mgogoro na mwenye fedha unapoanzia, kwa maana wakala wa mwenye fedha "polisi" amekula njama na Lugumi kuchota mapesa yetu kinyume na taratibu za manunuzi.

Kutuelekeza kakipengele ka jinsi ya kushughulikia mgogoro ikiwa utajitokeza ni ishara ya kuwepo mgogoro kiukwelikweli.

Huyo mkurugenzi wa Lugumi kutembea na ma body guards kumzidi Donald Trump inatengeneza picha kuwa anatumia kutoka kwenye matumizi asiyostahili (Limbukeni)
 
naona mwandishi kaamua kwa makusudi kabisa kuweka jina(fake) la saidi lugumi ili hii mada iingizwe kwenye udini zaidi.kama wanavyojaribu kuifanya issue ya aliekua DG wa ule mfuko wa hifadhi ya jamii ionekane ni ya kidini..nice move
 
Back
Top Bottom