Waliosema Saidi Lugumi katoroka nchi nahisi ni hivyo hivyo vyombo vya ulinzi na usalama.Jana au juzi niliwasikia takukuru wakisema wakimaliza uchunguzi wao watalifikisha suala hili mahakamani.Sasa aliekurupuka toka ofisi ya Lugumi na kuandika hiyo barua ambayo sidhani kama ina tarehe wala reference no na wala cheo cha mwandishi kwenye kampuni hiyo ni nani?Muda wote toka yaibuke haya walikuwa wanajipanga tu jinsi ya kuandika barua na kukanusha?Mbona barua haitaji idadi ya mashine waliyotakiwa kuuza,idadi iliyowasilishwa na kiasi cha malipo waliyopokea?Najua wapo watetezi watakaokuja na hoja kuwa vyote vipo kwenye mkataba na kama huo ni utetezi ya nini barua tena?kwa maana kama ni mkurugenzi kuwepo nchini tungearifiwa na polisi na sio mfanyakazi wa ofisi ya Lugumi.Mihuri na hata hizo headed paper unaweza kutayarishiwa ndani ya lisaa limoja pale mnazi mmoja ukitaka.Tunajuaje uhalali wa barua hii.Toka 2011 hadi 2016 kabla ya mambo haya kuwekwa hadharani kwa nini hawakutujuza au wanatafuta utetezi na kinga kwa mtumbua majipu?Najua uzito wa jipu hili kwa mtumbuaji kwani linahusisha pia vigogo wakubwa linahitaji moyo wa kujitoa kwani linahusu mabillioni ya shilingi kama hasara kwa taifa.Na hata hivyo sitashangaa kama uchunguzi wa sakata hili ukimclear Lugumi au dpp kushauri haipo haja ya kulifikisha mahakamani suala hili na bila hata kutoa sababu yoyote.Sheria za nchi hii ya ajabu zinamruhusu. AJABU!!!!!!