Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Annael ningekuwa sikufahamu ningetishika kwelikweli,maana kwa jinsi unavyotete Lugumi utadhani wewe ndiye lugumi mwenyewe!! Halafu unaponiacha hoi ni hapo unapomwaga mkwara na kuita wengine MASIKINI!!!wakati hako kachina kenyewe ulimtapeli mshkaji!! Hahahahaa!! Na Anakutafuta ujue! Sasa Hivi unajificha kama LUGUMI!!hohohohooo
Unataka ujibiwe hoja wewe nani? Kama unaona umeonewa nenda kashitaki kuliko kubweka bweka humu kwenye mitandao. Upewe hoja wewe nani? kwanini?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama unaona hapa si sehemu sahihi kwani kaileta humu?.Wewe unatetea usifadi kwa manufaa ya nani?.Hawa wanaohoji ndiyo walipa kodi na wanataka kujua jinsi kodi yao ilivyotumika.
kuna vijana hulipwa hela ya chips ili kuweza kusheheresha mada hasahasa hizi zenye masirahi na umma mkuu
 
Kwanza kosa lililopo kuchukua hela wakati kazi hujamaliza na mlichochukua sio advanvce kwani ni zaidi ya 25% ya mkataba na mmefunga ngapi na kweli hizo machine zipo au nazo inawezekana ikawa hewa pia bado hazijaletwa nchini kuwa Tanzania sio kinga au ufahari
 
Ba
Hatimae kampuni ya LUGUMI imejitokeza na kuelezea taarifa mbalimbali zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuita taarifa hizo ni za uzushi.

Sehemu ya taarifa hii inasema nanukuu;

“Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS. Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.

Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.”

Pia kuna sehemu ya taarifa hii inazidi kuchanganua nanukuu;

“Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa. Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika. Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida”.

Soma zaidi kupitia viambatanisho hivi.

View attachment 340959

View attachment 340961

Barua hii hata yenye maudhui ya posa inauhafadhari; sasa na wewe umeona kuwa umeandika barua; hauna akili kabisa
 
Yaa
Kirahisi rahisi tu mnajibu tuhuma kubwa namna hii kwa barua kama ya wanafunzi wanaotakana kimahusiano?
Yaani mtu anatuhumiwa wizi anasema tu "tuhums hizo ni za uongo ni uzushi mzipuuze" basi? Kama maelezo hayo tu yanatosha kumuondolea mtu tuhuma nani angekuwa gerezani?
 
Yaa

Yaani mtu anatuhumiwa wizi anasema tu "tuhums hizo ni za uongo ni uzushi mzipuuze" basi? Kama maelezo hayo tu yanatosha kumuondolea mtu tuhuma nani angekuwa gerezani?

Mhuri wenyewe waliopiga ni hii ya kuchonga ambayo vibaraza vya posta inauzwa sh 2000, ubabaishaji wa namna hii ndio umefanya watu wakawa na uhasama mkubwa na serikali!
 
Huyo aliyeandika hiyo taarifa kwa vyombo vya habari kama ni shuleni mwalimu angempa maksi 1/100 maana hiyo insha yake ipo tofauti na kichwa cha habari alichopewa.Kaandika utumbo tu badala ya kujibu hoja ya alivyotekeleza mkataba na malipo vimeenda sawa!?
 
mkuu bongo tunaishi kwa ujanja ujanja mwingi. hata usishangae.

Nawaza tu kijinga kwamba asipotokea mtu akajitoa ufahamu akatupeleka mpela mpela at least kama Magu anavyotupeleka tulikwishafika pabaya! Magu ni kama dereva wa trekta aliyekabidhiwa basi lililokwama kwenye tope, muhimu ni kulipiga gia bila hata kujali kuibembeleza clutch hadi litoke liingie njia kuu, baada ya hapo ni kulipiga basi lenyewe maji halafu safari ya umalila inaendelea...hatuwezi kuwa dominated na wajanja wachache huku mamilioni ya watu wakizidi kuogelea kwenye ufukara!
 
Nadhani unatuchanganya hapa. This time sio walioingia kwenye mkataba wanalalamika ni mtu wa tatu anayeangalia the whole thing ilivyokwenda na ni yeye anataka maelezo.Its too simple.
Nafikiri hukutakiwa kujibu kama hoja zako ni hizi.
Ila serikali ya JPM itaangalia msema ukweli ni nani
 
Mbona huwajakanusha kuhusu wizi wa Sh.bil.37.Kwa hiyo kaiba,si ndiyo.Kihunzi cha Magufuli hataruka!
Hatimae kampuni ya LUGUMI imejitokeza na kuelezea taarifa mbalimbali zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuita taarifa hizo ni za uzushi.

Sehemu ya taarifa hii inasema nanukuu;

“Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS. Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.

Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.”

Pia kuna sehemu ya taarifa hii inazidi kuchanganua nanukuu;

“Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa. Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika. Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida”.

Soma zaidi kupitia viambatanisho hivi.

View attachment 340959

View attachment 340961
 
Lugumi ndio nini? kama watendaji wakuu wa kampuni hii ndio vilaza namna hii mpaka kufikia kuandika ripoti mbovu isiyokuwa na mashiko kama hiyo hapo juu sitashangaa kusikia kuwa walikula hela na kulala mbele bila kudeliver kazi waliyokubaliana
 
Back
Top Bottom