Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
mkalamo

Ndugu waandishi wa habari , nimewaita hapa leo ili niweze kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa kwa niaba ya Kampuni yetu ya LUGUMI ENTERPRISES LTD, kwa siku kadhaa kumekuwa na habari mbali mbali za kuchafua na kudhalilisha Kampuni yetu pamoja na Mimi Said Lugumi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu.

Nitafafanua mambo yafuatayo kama majibu ya kadhia ambayo sisi na Washirika wenzetu katika shughuli zetu za kibiashara tumekutana nayo ,

Kampuni ya LUGUMI ENTERPRISES LTD ilipewa zabuni ya kufunga na kusambaza mitambo ya kuhakiki alama za vidole mnamo mwaka 2011 na kazi tuliifanya kwa kushirikiana na Washirika wenzetu wa kibiashara nje ya Nchi Kampuni za BIOMETRICA LLC (USA) na BIOLINK (RUSSIA) , tumefanikiwa kufunga na kusambaza mfumo wa alama za vidole (AUTOMATED FINGER PRINTS IDENTIFICATION SYSTEM – AFIS ) katika maeneo yote ya Nchi yetu na kwa uadilifu kama ambavyo mkataba ulivyohitaji.

Pamoja na kashfa nyingi dhidi ya Kampuni yetu na hususan Mimi binafsi , ukweli ni kwamba hakuna ufisadi wala wizi uliofanyika katika biashara hii muhimu na ya siri , kazi au biashara zinazohusu mambo ya ndani ya usalama wa Nchi zina mashariti yake na itifaki yake , ndio sababu taarifa hii inakusudia kuwatoa wasiwasi ndugu zetu , marafiki zetu na washirika wenzetu na sio kusema hadharani mienendo ya shughuli na zabuni za kazi za namna hii.

Ni uhakika kwamba Rais wetu Mh Dr John Pombe Magufuli , amedhiirisha pasipo hofu uwezo wake wa kupambana na ufisadi , wizi , utovu wa nidhamu katika utawala wake , hivyo basi kazi hii niliyoifanya na Jeshi la Polisi inaniweka Mimi na Kampuni yangu kwenye wakati rahisi wa kukamatwa na kuhojiwa juu ya tuhuma za kuibia taasisi iliyopewa mamlaka ya kupambana na uhalifu Nchini , sifikiri wala sidhani kama uhalifu wangu unasubiri Kamati ya Bunge kuthibitishwa , ni rahisi sana kwa Jeshi la Polisi kujua je vifaa hivi viko kwenye vituo vya Polisi au haviko ? na kama haviko kwanini Kampuni yangu ililipwa ? na kama nimelipwa kwa kazi ambayo sikuifanya , wale wote walio husika na mchakato wote wa kuhakiki kuwa kazi imefanyika na kuidhinisha malipo kwa kazi hiyo , wanasitahili kuwa wapi ?

Ninaona hii ni vita ya kibiashara dhidi yha Kampuni yangu , ndio sababu wengine wanahoji vitu vyepesi visivyo na ufahamu , kuwa imekuwaje mimi kupata kazi kubwa kama hii ? Ndoto yangu katika biashara zangu , hii kazi kwangu bado ni ndogo , nimefika hapa kwa kupitia maisha magumu sana , kuna wakati niliishi bila kula na bila kuwa na kazi , lakini siku zote nimekuwa nikiwaza kufanikiwa katika maisha na hapa nilipofika nimefika kwa sababu ya BIDII , MAARIFA , UTHUBUTU NA UJASIRI na safari yangu ya maisha inakwenda mbele zaidi ya hapa.

Mengi yametajwa kuhusu mahusiano yangu na Mh Riziwan Kikwete na wengine kudai kuwa ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Lugumi . Ukweli ni kwamba hana hata hisa moja katika biashara zangu ila Riziwan ni rafiki yangu , wengine wanasema kuwa yeye ndio amefanikisha shughuli zangu hizi zote , ukweli ni kwamba sio kweli kama inavyosemwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti mbali mbali , lakini hata kama angekuwa amesaidia kwa namna moja au nyingine kufika hapa nilipo fika kibiashara , je ningekuwa nimevunja utaratibu na sheria za Nchi ?

Kwa bahati mbaya katika Nchi yetu shughuli za biashara kubwa zinaonekana kuwa ni za Watu na makundi maalumu na sio za Watanzania kama LUGUMI , ndio sababu hoja zote kwenye mitandao ya Jamii na magazeti zinahoji ninawezaje kufanikiwa katika kiwango hiki wakati Mimi ni Mtoto wa masikini ? Jibu ni rahisi , NACHUKIA UMASIKINI .

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Charles Kitwanga anajua ukweli wa jambo hili , kwani Kampuni yake ya INFOSYS ndiyo ilipewa dhamana kiufundi ya kuunganisha mitambo yote tuliyoisamabaza katika vituo vyote vya Polisi kama tulivyoelekezwa kwenye mkataba na Jeshi la Polisi , Je sio rahisi sana kwa Waziri kulisidia Bunge ili kupunguza gharama za utafiti na kuchafuana kwa kiwango hiki kunako endelea ?

Katika Vyombo vya habari mbali mbali imeripotiwa kuwa vituo vilivyofungwa mfumo havizidi kumi na tano , jambo ambalo , Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) anaweza kuwa na majibu mazuri kuliko Mimi , nawashauri mkamuulize , ila ripoti kutoka ofisini kwetu ambayo imesainiwa na Maafisa mbali mbali waandamizi wa Jeshi la Polisi , inathibitisha kuwa kazi hii imeshafanyika kwa asilimia zaidi ya 99%.

Mwisho , kasi ya Rais wetu katika utumishi wake ni nzuri ila wako Watu wanataka kuitumia vibaya ili kudhalilisha wengine na hatimaye kuwapora haki zao . Tunamuomba Mh Rais awe makini sana katika falsafa yake ya utumbuaji majipu , kwani wengine wanatafuta namna ya kulipa visasi.


Asanteni sana kwa kunisikiliza

Said Lugumi (MD)

LUGUMI ENTERPRISES LTD

==================================

Hatimae kampuni ya LUGUMI imejitokeza na kuelezea taarifa mbalimbali zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuita taarifa hizo ni za uzushi.

Sehemu ya taarifa hii inasema nanukuu;

“Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS. Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.

Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.”


Pia kuna sehemu ya taarifa hii inazidi kuchanganua nanukuu;

“Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa. Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika. Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida”.

Soma zaidi kupitia viambatanisho hivi.

20160420023316.jpg


20160420023326.jpg


=========================
 
Tanzania bana kila mtu ni shushushu yaani ukuda kila sehem.yaani hamna usiri watanzania hata kama ni siri yako peke yako iko siku utaisema.inshort hatuna guts ya kukaa kimya kwa jambo lolote dogo au kubwa lenye maslah na ww na lisokukuhusu utalishadadia tu.hahaha hii ndo tz bana kisiwa cha ukuda
 
wawape izo kakaratasi TAKUKURU basi..hapo nilichoona akijakosewa ni muhuri tuu..
 
Ili mimi binafsi nipuuze taarifa zinazosambazwa naomba kujua kama pesa hizo kweli mmelipwa kiasi gani na mnadai kiasi gani na tayari mmfunga machine ngapi na bado ngapi na mnategemea kumaliza lini na mkataba uliwataka kumaliza lini baaaasi.. Then nitapuuza
 
Kirahisi rahisi tu mnajibu tuhuma kubwa namna hii kwa barua kama ya wanafunzi wanaotakana kimahusiano?
Mkuu hata mimi nashindwa kuwaelewa!!! Wanataka kusema nini? Kwamba kwa kuwa Wizara ya mambo ya ndani haijalalamikia chochote kuhusu mkataba huo basi hata taarifa ya ukaguzi hazina maana au?
 
ivi ulikuwa ni UZUSHiiiii au ni analysis zilizofanywa na CAG pamoja na kudhibitishwa na kamati ya bunge?mbona kama hill jipu linajitoa ufahamu.au watakuwa wameishapima kina cha maji cha sakata hili na wamehisi ni kifupi na sasa wameamua kuja na kanusho la pegi 2 kudefend mtumbuaji wa majib mzee wetu mpendwa
 
Hii Press release haikujibu kiu ya watanzania maana haielezi mradi ulikamilika kwa kiwango gani na hela ililipwa kwa kiasi gani? Swala la kulalamika kwa mwana sharia mkuu wa serikali halina mantiki maana kuna pande zote mbili zilikuwa na maslahi binafsi hatutegemei malalamiko hayo hata kama mradi haukutekelezwa ipasavyo kama ilivyo sasa!!!!!!.
as such looks kuna conspiracy between Lugumi and Police top brass allowing them to swindle the money without delivering the intended products.

PCCB and Kamati za Bunge stand firm and unearth every stone related to this shameful scandal.
 
This is an insult.....

Hakuna maelezo kuhusu kinacholalamikiwa na wengi, machine 14?!

Badala yake wameona petty issue ya director wao kukimbia nchi!!!
 
Wameshafunga mashine au bado, kama bado je wameshachukua pesa (wameshalipwa) kama wamelipwa kabla ya kufanya kazi hapo ndipo mgogoro na mwenye fedha unapoanzia, kwa maana wakala wa mwenye fedha "polisi" amekula njama na Lugumi kuchota mapesa yetu kinyume na taratibu za manunuzi.

Kutuelekeza kakipengele ka jinsi ya kushughulikia mgogoro ikiwa utajitokeza ni ishara ya kuwepo mgogoro kiukwelikweli.

Huyo mkurugenzi wa Lugumi kutembea na ma body guards kumzidi Donald Trump inatengeneza picha kuwa anatumia kutoka kwenye matumizi asiyostahili (Limbukeni)
 
Back
Top Bottom