Saidi Lugumi kuringishia Magari yake, Ni Ulimbukeni au Utajiri?

Saidi Lugumi kuringishia Magari yake, Ni Ulimbukeni au Utajiri?

View attachment 3135806

Kuna clip inatembea kwenye magroup ya WhatsApp. Anaonekana Said Lugumi akimkabidhi hela Chief Godlove na kumuonyesha garage ya magari ya kisasa ambayo Lugumi anamiliki kama G-Wagon, Bentley etc.

Huyu mtu ali TREND sana wakati Magufuli alitaka kuuza nyumba zake kwa sababu ya kutomaliza zabuni ya ugavi wa vifaa vya kieletroniki kwa Jeshi la Polisi.

Ameibuka upya kwa namna hiyo. Najiuliza huu ni ULIMBUKENI au ni utajiri ??
Punguza roho mbaya kaka....katika moja ya vitu vilivyonifanya nimchukie magufuri ni kuwachukia wasomi Na matajiri..
 
View attachment 3135806

Kuna clip inatembea kwenye magroup ya WhatsApp. Anaonekana Said Lugumi akimkabidhi hela Chief Godlove na kumuonyesha garage ya magari ya kisasa ambayo Lugumi anamiliki kama G-Wagon, Bentley etc.

Huyu mtu ali TREND sana wakati Magufuli alitaka kuuza nyumba zake kwa sababu ya kutomaliza zabuni ya ugavi wa vifaa vya kieletroniki kwa Jeshi la Polisi.

Ameibuka upya kwa namna hiyo. Najiuliza huu ni ULIMBUKENI au ni utajiri ??
Ila lugumi pesa ipo na hana kelele kama wale wajinga akina Doto magari na yule mwenzake isa tambuu wenye hela za mawazo
 
Juzi kati alikuwa Europe na baadhi ya makanali wa jeshi la wananchi wa Tanzania walikuwa kwenye mission ya kununua silaha kwa ajili ya jeshi la wananchi (JWTZ). Hii ni syndicate kubwa sana wako vigogo wakubwa nyuma ya lugumi. JWT, Police na baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu na baadhi ya wakurugenzi wizara ya fedha. Baada ya IGP Said Mwema kuanzisha hili deal na Lugumi na baadhi ya maofisa wa police procurement team,naona deal limeenda mpaka jeshi letu pendwa. Hii ni kashifa kubwa sana kwa jeshi letu. Lugumi ni darasa la Saba. Kazi yake ilikuwa shoeshine hapo Mwanza hotel jijini Mwanza kabla ya kumupataa mke wake mdogo wake Said Mwema (IGP). Hivyo mambo anayofanya Lugumi ni kwa sababu ya Elimu yake ndogo anataka kuwakomoa wasomi waonekane takataka na kwamba shule haina maana.

Kuna wakati ili mambo yaende, inabidi kuwa mjinga na kujifanya uongo wanaousema ndio ukweli. Ila muda una tabia nzuri. lazima ukweli na uongo ujitenge ili dunia iendelee kuzunguka.
Na huwa unaanzisha mambo yake pale inapoonekana ni budi. It can even take very long. But it will happen. Kwa maana hiyo, tuwe wakweli.
sababu ya kutumia third parties kwenye baadhi ya manunuzi ni kurahisha namna migao itakavyo kwenda. Maana pia hatukatazwi kununua moja kwa mopja kutoka kwa suppliers. Unless tumewekewa vikwazo, na tunataka kuvikwepa
 
Mafukara bwana 😂😂

Sio kweli pesa ni kila kitu. Unalala kitanda kimoja, unakula chakula kama wanadamu wengine, unaendesha gari sawa na wengine hata kama gari lina mambp yote unayoyasema yapo.
Na mwisho, wwote tunakufa. Kuzikwa ni maamuzi yako utazikiwa wapi, ila lazima pia utazikwa. kafa Lenin na Bolshevik yake. Kafa Stalin na kaiacha USSR ambayo aliifanya mali binafsi. Kafa Hitler na mazagazaga yake...sembuse sisi ambao tunasema hela ndio kila kitu?
Labda wenye hela wanakunya dhahabu...that I have to find out
 
Sisi ngozi nyeusi shids sana ukipata senti kidogo utataka mpaka sisimizi waju! Wenzetu wahindi wao wakipata wanawekeza kwenye vitu vya maana sisi unakimbilia vitu vya anasa ambavyo havizalishi ! maskini Lugumii !
Pesa nitafute mimi tena kwa taabu halafu wakati wa kutumia unipangie wewe, pengine vyote unavyodhania sijafanya nilishafanya kitambo na hili ni mojawapo ya hitaji langu.
 
Nimeona video ya masikini wakidiscuss magari ya tajiri mwenzangu said lugumi baada ya Mimi kumtembelea mara wanamuita limbukeni Sasa masikini wa humu Kwa njaa zao zinavyowapiga wanaona hasira zao wamalizie kumtukana tajiri mwenzangu Sasa napenda kuwaambia nyie mafukara tafuteni hela acheni ujinga yaani unakuta dume Zima linadiscuss Mali za mwanaume mwenzie tutawalia sana wake zenu
Ukute hata bando umesongesha.
 
Ni banana republic tu utawaona watu kama hawa!
Kafanya ufisadi wa kufa mtu! Kalindwa na yuko mitaani akiwaringishia raia wanaokuwa mlo mmoja kwa siku! Na dola hata HAIMGUSI!
 
Hata wewe utakufa ubaya unakufa na haujaenjoy maisha kutokana na umasikini wako
Wewe una enjoy nini kwani kunizidi? Si nafuu niwe na hela yangu ndogo lakini sina masharti ya kuitumia!! Utakuta una hela halafu unalala stoo kwenye maboksi ya nyumba yako!! Huo ni ufala
 
Lakini ni wachache sana wanafanya hivyo. Ila nigger akikamata hata laki tano mshahara kwa mwezi yani ni fujo kitaa.

Mkuu kweli huo mzigo parking ni hatarii. Range ya mwaka huu. Nimepiga hesabu haraka haraka thamani ya huo mzigo ni billion tano au zaidi.
Kwao masikini kibao kisha anakusanya mabati anayajaza nyumbani. Nyerere alisema hayo ni mabati na plastic na vyuma vilivyopakwa rangi. Nyerere alisema asset alisema ni miti tu iiyojazana tabora ila imepigwa msasa ulaya na kupakwa rangi so kwa nini ubabaike kiasi uagize kutoka nje ? jibu kuwa ni upungufu wa akili.
Mtanzania ametukuza kila kitu na hatomae kapoteza utu wake. Wengine huko magari ni usafiri kwetu na USA magari ni utajjiri. Waafrika sijui tutaamka lini. Gari la milioni 600 linafaida gano ? Ni bora hata angekuwa amekusanya malori ambayo ni kama
kiwanda. Ila TZ ujinga huwa unakuzwa na kufanywa ujanja.
Kuna mwanasaokolojia nomemskia akisema ujinga ukkubalika na wengi huwa unageuka kuwa fact. Car collection imegeuka kuwa fact na ujanja.
Tujiulize kungekuwa na viwanda vya magari hapa TZ mtu angekusanya hayo magari na kujifanya tajiri wakati kuna watu wao wanayazalisha kwa maelfu ? Unagundua umasikini wa kichwa ndio unatusumbua.
Wengine tunawaza jinsi gani tutaanza kuyeyusha mabati tupate magari kuna we gine akili zao wanawaza kuyakusanya hayo mabati na kuyajaza nyumbani ili watoto wao waje warithi scraper.
Jamani tufunguke akili. Wajapani wanarithishana viwanda sio uchafu.
 
Back
Top Bottom