Saikolojia: Jinsi ya kuondokana na mawazo yanayoumiza au kuhuzunisha

Saikolojia: Jinsi ya kuondokana na mawazo yanayoumiza au kuhuzunisha

Niligundua nina hili tatizo toka mwaka 2013 hadi sasa bado inanitafuna slowly.

Nimeshindwa kuishi in present time muda mwingi nawaza yaliyopita na yajayo hata nikijifanya kujisahaulisha na company za washkaji na nini ila nikitulia tu peke yangu balaa linarudi palepale.

Na kama kitu kinawanyima watu usingizi basi ni over thinking unaweza ukajiuliza mtu kwa inakuaje anachelewa kulala na anawahi kuamka ni kutokana na hiyo kitu sometimes unashindwa kulala kabisa.

Ndugu zangu kwa wenye experience na tatizo au kama unajua namna ya kuliepuka tusaidiane maujuzi.
 
Suriya, shukrani mkuu inaweza kuwa ugumu wa maisha pia unachangia lakini haya yaliyopita mi nayawaza,
Kitu kingine niongee tu kipindi ambacho hii kitu inaanza ndo nilikua mtu kusali sana na najua ndo moja ya sababu ya kuniweka mbali na dini.
 
shukrani mkuu inaweza kua ugumu wa maisha pia unachangia lakini haya yaliyopita mi nayawaza,
Kitu kingine niongee tu kipindi ambacho hii kitu inaanza ndo nilikua mtu kusali sana na najua ndo moja ya sababu ya kuniweka mbali na dini
Nikwambie kitu dunia hii hakuna anawezae kubadili akili za mwanadamu isipokua Mungu tu.

Mwenye solution ya tatizo lako ni Mungu, mkimbilie yeye atasolve tatizo lako bila hata sent moja.

Lakin ukitaka psychological counseling ni lazima uyaweke wazi yanayokusumbua hapa.
 
Pole ndugu, usijali utakua sawa. Zipo njia nyingi tu. Kuna technique moja inaitwa replacement, kwa maana ya kutoa kitu na kuweka kingine bora zaidi. Replace muda na nguvu unayoitumia kuwekeza kwenye kufikiria kwa kufanya activities bora zaidi kama mazoezi ya viungo, kusoma vitabu, kuangalia movies, kufanya usafi n.k.

Zaidi socialize, socialize, socialize, jichanganye na watu bro, ukiweza fanya uoe kama bado. Kwa kufanya hivyo hutakuwa na muda wa kuwaza, badala yake utakuwa unafanya ya muhimu zaidi. It will not end over night, ila mdogo mdogo utatoboa freshi tu. Hali unayoipitia nimeipitia pia, naijua nje ndani ndani nje, kwa hiyo nikutie moyo tu kwamba utakua poa usijali kabisa, ila kwa kufanya kwa vitendo hayo niliyoyaelezea.
 
businessvillains-20200126-0004~2.jpg
 
Pole mkuu..
Jitahidi kufanya kitu unachokipenda ili kuifanya akili kuwa occupied na pia kupata positive vibes..

kuhusu kusahau vitu vilivyopita inategemeana na ukubwa wake na possibility ya kuvitatua..

Kama ni vya kawaida, just get busy na usiweke expectations kwa watu maana utakuwa dissapointed kila mara

kama vikubwa bhasi tafuta solution yake kwa ukubwa wake
 
Mimi nafikiri nambo mengi sana na nashindwa kujizuia. Mfano leo mchana nilikuwa napiga hesabu namna ya kulifanya JWTZ kuwa imara na la kisasa. Nikapanga mishahara, training na operation costs zitolewe na Idara ya Ulinzi ambayo ingeundwa. Kisha bajeti ya ulinzi iwe trilioni 2 ijitegemee kununua na kudhamini miradi ya kutengeneza silaha.

Nikapanga tununue fast attack boat 4 za Visby kutoka Sweden jumla trillioni 1. Tununue Mill Mi 28N gunship za Urusi, ziwe kumi zinacost jumla ya bilioni 500. Na tununue sniper riffles, body armours, MANPADS, smart guided bombs, field drones zile ndogo za recon na makorokoro ya kisasa madogo yacost bilioni 200.

Na vifaru vya T-90 vikiwa 30 vinacost around bilioni 300. Jumla ya vyote ni trilioni 2 bajeti ya mwaka, mwaka unaofuata ni kununua kwenye mlinganyo wa 3:2:1 ikiwa ni navy, airwing na army respectively. Hapa nishapiga hesabu za kilimo, teknolojia, elimu, afya na vyote.
 
Huu ni mwendelezo wa overthinking nishafikiria sekta zote na miaka michache ishapita. Bajeti ya jeshi haizidi 6% ya GDP
😂😂😂😂😂
Mfano mi kama ni manzi nimemuelewa kabla hata sijamsemesha wala contact zake sina huwa naanza ku calculate possibilities zote asilima za kupigwa chini au success nawaza mambo kibao akinikatalia itakuaje atanishushia heshima au akinikubalia vp atanipiga mizinga sana au kawaida au vip akija kugundua namcheat itakuaje in short kabla sijafanya maamuzi huwa nawaza sana
 
Mimi mwenyewe ni over thinker matata ndo maana nina waza hadi nimeshapanga jinsi nitakavyoishi maisha yangu yote mpaka uzeeni. Nikiona kama naanza ku over think sana najiweka busy kwa kusoma vitabu kuangalia videos etc.

Kitu kingine nilichokigundua ni kwamba kama nataka nisi over think kuhusu jambo fulani ninalotakiwa kulifanya nalifanya mapema kabla sijawa kichaa.

Na pia hii ni side effect moja wapo ya kuwa introvert.
 
Ufumbuzi wake inabidi kuhusisha njia mbali mbali kwa wakati mmoja.

Matharani;
1. Uende vituo vya meditation na kufanya Medium

2. Ujitoe na kushiriki maombi na kupata mafundisho ya Neno la Mungu

3. Kufanya mazoezi ya viungo na kutembea kwa miguu

4. Kula chakula sahihi n.k

Kwa kuanzia ukiweza kuyafanya hao siriasi nakwambia hautajua ni lini au ni kipi hasa kilichojuponya Sifa na utukufu utampa Mungu maana anastahili.

Kule kwenye kupata mafundisho ya Neno la Mungu utajifunza Mengi ikiwemo swala kusamehe walokukosea, na wewe kwenda kuomba msamaha ulowakosea n.k

Kusimama kwenye ahadi za Mungu, mfano imewekwa “ alalapo mwenyehaki wa Mungu usingizi wake ni kama wa mtoto mchanga”


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom